Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumlaumu Mangula labda kwa udhaifu wake wa kutokemea hadharani ufisadi...
Na hii Mkuu Share ni dhambi kubwa sana ambayo uzito wake unaweza kulingana na waliofanya ufisadi. Alikuwa na nafasi ya kukemea maovu lakini akaamua kunyamaza na kuwaangalia watanzania wenzake wanaumizwa
Mchango wangu kwa Mzee Mangula ni kwamba ninamshauri akae kimya ili historia iweze kumhukumu badala ya kuanza kujieleza kwa yale ambayo yeye alipaswa kuyafanya huko nyuma akiwa kiongozi mkuu kwenye chama kilichoshika serikali. Hayo yote ambayo anayalalamikia ni uzao wa yale aliyoyalea wakati wa uongozi wao. Ili aeleweke vizuri angetubu makosa yake aliyoyafanya kama kiongozi badala ya kulalamika kama ambavyo anafanya sasa hivi.
Your motto , mkuu Mpita Njia, answers it all: That is; The aim of an argument or discussion should not be victory, but progress Happy New Year 2009 mkuu.
aachwe aseme. anaweza kuwa na mengi ya busara na maana ambayo tunaweza kuyatumia kupunguza matatizo tuliyonayo.
tunapokuwa na matatizo tuombe na tupokee michango ya mawazo ya kila mtu na kila kundi. tuyatafakari na tukiona yana maana tuyafanyie kazi
kwamba hakukemea akiwa madarakani inaweza kuwa ni kwasabau ya kumuogopa aliyemweka pale.
lakini kuna wengine huona zaidi uhalisia wa mambo wanapokuwa pembeni.
Mangula: CCM yahitaji Sokoine mwingine
Tatizo linalokipata chama chetu, ni kwamba wajumbe hawa wa mikoa, wanaoomba soda kutoka kwa wagombea, ndio hao hao wanakwenda kushiriki katika chaguzi za ngazi ya taifa.
Huko pia hujifunza kutokana na rafu wanazozifanya viongozi wanaowania uongozi wa kitaifa. Wanarudi na dhambi ya kutaka soda kwenye maeneo yao. Huu ni ugonjwa. anasema.
Hii ni hatari kubwa na viongozi wa dini mnaokipigia debe CCM mulione hili. Ama kweli leo nimeamini kuwa Watanzania tuko tabuni kwani hawa ndio wateule kutuongoza. Kauli kama hizi za Mangula zinatisha kwani zinaonyesha jinsi wenye madaraka wanavyokaa kimya wakiona na kushiriki vitendo viovu na huamuwa kuviweka wazi pale tu wanapokosa madaraka.
Swali kwa Mangula; Unataka kurudi kwenye uongozi wa CCM unayosema wewe mwenyewe kuwa ina vitendo vichafu, Kwanini? Kama ulishindwa kukemea na kukisafisha CCM ukiwa Katibu Mkuu utaweza kufanya hivyo kwa nafasi ya chini? Au ni hivyo tena kipofu haachi mkongojo wake, unataka urudi ukafaidi hicho kamchezo?