Sina uthibitisho lakini kinachosemwa ni kuwa kutokana na ujasiri wake katika kuwatumikia watu hususan wa hali ya chini bila ya woga, Sokoinealijijengea umaarufu mkubwa na alionekana ni mkombozi wa wanyonge na mtetezi makini wa maslahi ya taifa.
Jambo hilo liliwakera vigogo waasisi wa nchi kama akina Kawawa, Msuya, Malecela nk waliokuwa na uchu wa kuchukua hatamu baada ya nyerere kung'atuka. Baya zaidi Nyerere alionyesha kumhusudu sokoine kwa staili yake ya uongozi na kutatua matatizo ya nchi bila ya woga , kiasi cha kujulikana katika circles za kiserikali kuwa alikuwa akimwandaa kuwa mrithi wake.
Inavumishwa kuwa hao waheshimiwa waliokuwa wanajiona wanastahili kuwa warithi watarajiwa halali, wakaona haiwezekani mtoto mdogo kama yeye ambaye hakuwa hata na historia ndefu ya kupigania uhuru, akamrithi mwalimu wakati wao, ambao walishiriki kwa kiasi kikubwa zaidi ktk kupigania uhuru, wakiwa hai, na wakiangalia tu!!! . mpango ukasukwa, kwa kushirikiana na wahujumu uchumi ambao sokoine aliwapelekesha puta.. ...na hatimaye jambo likatokea.
NB; ni uvumi uliovuma miaka hiyo ambayo ni vigumu kwangu kuuthibitisha