Mtukwao,
Ndugu yangu hiyo 95 nilikuwepo Bongo haikuwa hivyo kwa sababu mzee Mwl. alikuwa bado hai na tetesi zinavyoelekea hata kifo chake kimetokana na ukweli kwamba Mkapa asingekamata awamu ya pili kama mwl. angekuwa hai. Ni nyerere aliyeyafanya makosa yoteee! ktk teuzi zake za warithi hilo wazi na ndoo maana mwl hakuwa mzuri hata uchaguzi wake wa wanawake. Heeee heee hee!
Hata hivyo haimfanyi yeye kuwa mjinga, kiongozi mbaya ama mpumbavu. Mwaka 2000 pia nilikuwepo na kama wewe upo ktk vijiwe vyetu utakumbuka kuwa niliwahi kuandika mengi ya wakati ule kule bcstimes. Kwa hiyo haya nayoyaona leo ni mageni kabisa. Mkapa alikuwa na nguvu kubwa sana kama rais na hakuna maamuzi yasiyokuwa na mkono wake ikiwa ni pamoja na mikataba yote.
Leo hii migawanyo ya mali zote imeisha kamilika, kila kiongozi ana nafasi yake ktk miundombinu, vitega uchumi na kadhalika. Vodafone kashika Rostam na Lowassa, mpumbavu kama mimi huwezi tena kuleta shirika la kupinga unyonywaji wa wananchi ktk muundombinu huo, haikuwa hivyo miaka mitano iliyopita. Umeyasikia ya Citywater, Richmond, n.k ni mambo ambayo yametengenezwa miaka mitano tu ya utawala wa Mkapa na leo hii ndio matunda tunayaona na lawama zetu zinaanzia kwa JK.
Kwa hiyo brother, nambie jingine mji naujua vizuri kwa kila mishen zinazotembea mjini... mwaka 95 nyumba za Kariakoo zilikuwa zikuzwa kwa dollar elfu 20 tu leo hii bila Laki 2 hujaitoa kibanda tena ktk mtaa usiokuwa maarufu....Manji kununua Coco beach ni swala ambao halikuwezekana miaka mitano iliyopita... kwa hiyo uuzaji unaozungumzia wewe ni ule wa kuuza mali za serikali ikiwa ni pamoja na viwanda, mashirika ya Umma n.k. Huko wameisha maliza sasa hivi ni ARDHI... umilikaji wa ardhi ni sheria ambayo imetungwa baaada ya wao kushika majumba yote muhimu mijini... Urithi usiokuwa na nasaba!..lakini wajomba nyie bado tunatazama huduma za serikali hii kama ndio chimbuko la rushwa zote.
Hizo hoja za ufujaji wa mali za serikali na utumiaji mbaya wa madaraka kwa baadhi ya viongozi ni mchanga wa macho mnatupiwa ili akili zenu zianze kufikiria nje ya urithi huu unavyogawanywa. At the end of the day kila mlalahoi hatakuwa na kitu zaidi ya kibanda huko Kitunda, Yombo na Mbagala.
Hata hivyo bado nitasema uwanja upo wazi sana.. tusikate tamaa kwa haya yote pamoja na kuwa mafia inayotawala nchi ni kubwa kuliko uwezo wa JK. JK kashindwa kabisa ku deliver kwa sababu hana ubavu kabisa!...Atasema kila analoweza kusema kama rais lakini kuwa watu untouchable!... He knows that na hakuna cha sheria ya rushwa wala mjomba wake itakayo wagusa.
Majuzi tu umesikia waziri akisimama bungeni na kupinga Bunge kuhoji ama kupitia mikataba kwa mara ya nne!..Na hakuna hata mbunge mmoja anayeweza kusimama na kuipeleka hoja hii kwa rais kama ni SAUTI ya WANANCHI. Tunacholilia ni kuwepo kwa sheria ya rushwa ambayo kirahisi sana inaweza kutenguliwa na bakshish (commission) . Nikiwa na maana kama kisheria nimepewa commission ya 2 mil kwa ununuzi wa Rada basi mimi sikufanya rushwa. Na ikiwa nitatumia fedha zaidi kupata tender fulani (takrima) sidhani kama mpokeaji atakuwa kapokea rushwa kulingana na mapendekezo ya wengi.
Mtu kwao Bongo imeharibika vibaya sana na kila kona kuna kula ya watu, huwezi kuja na vijisheria vyako kuziba riziki za watu. Nitaandika mengi sana zaidi nitakapo rudi kwa uwazi zaidi.. lakini bob Bongo leo hii kiuchumi ni sawa na nchi yeyote yenye vita kasoro yake ni kwamba hakuna mitutu ya bunduki. Bongo ni ghali kuliko nchi yeyote ya magharibi imefikia hata chakula. Mayai tray moja dollar 3.50 kwa mayai 30, kuku hao wenu wa kizungu elfu 4.5. Kuku ambao wa nyama hawawezi kutaga mayai na wale wa mayai hawawezi ku kutotoa vifaranga na wale wanaoweza kutotoa vifaranga ni kuku maalum. Jamani kweli umewahi kusikia viumbe wa namna hii? Cancer ndio inatumaliza! Samaki kama sato (tilapia) ni sh 3200 kwa kilo.
Mengineyo mtajaza wenyewe nakuachieni Bongo mjomba samahani sana!
Mzee Mwanakijiji nitwangie simu mjomba tuongee mengi kwa kirefu zaidi.