Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

- Mangula akubali tu yaishe, sisi huku taifa ngoma inogile maneno yote Kisutu, Sokoine hakupeleka mtu yoyote mzito Kisutu zaidi tu wauza Colgate, sasa CCM tunapeleka Kisutu mawaziri wa zamani ambao yeye alipokuwa katibu mkuu wao wa CCM hakuyaona madhambi yao, under current CCM waziri mkuu na mawaziri wawili wamelazimika kujiuzulu kukwepa sheria na sasa wako njiani kufika Kisutu pia, Mangula hajaona haya?

- Mkapa mkuu wa Mangula, ndio hivyo mguu mmoja ndani na mwingine nje kuelekea Kisutu, labda tuwaombe serikali waangalie nini mchango wa Mangula kwenye wizi wa Mkapa maana definetely he knows and did something as patner in crime!

Mangula jaribu kuja mjini sometimes maana unaonekana kupitwa sana na yanayojiri Kisutu, CCM at this point and time tunahitaji ushahidi kama wake Mangula kumharakisha Mkapa Kisutu sio maneno ya Sokoine maana ya sasa Sokoine cha mtoto, Feleshi noma tupu hata Sokione kasingiziwa sasa tunamsubiri Mama Meghji next, Mangula miaka 10 CCM hakuna lolote zaidi tu ya kulia lia huko pembeni, debe tupu bwana kwa kelele tu!

Wakulu Invisible na Halisi, tupeni dataz vipi wiki hiii zamu ya nani Kisutu?


Mkuu FMES heshima mbele, Tunapochangia hapa tufikirie kwamba Mangula aliyasema haya maneno mwaka 2007 baada ya uchaguzi mkuu wa CCM. Kisutu ni ya 2008 hebu tumtendee haki huyu bwana pia.
 
Bad System can Bit Good People.

Mangula amaekaa ndani ya CCM kwa muda mrefu sana tangu enzi Marehemu Nyerere akiwa rais. Yeye ni sehemu ya matatizo ya CCM leo hii, si mtoaji wala mpokeaji rushwa, lakini ni mkaa kimya ili mradi wake ufanikiwe. Kuliko kukikosoa chama ni vema akae kimya.

Jah People au MR Sanga aliyeshinda wapinzani wake na kuwa Mweneyekiti wa CCM ni tajiri haramia mwenye mgari ya mizigo(semi's) lukuki aliyejiosha mikono nakujifanya msafi pale Makambako.

Aliyoyasema ni kweli, lakini kulalamika pale tu wewe ukipigwa ngwala si jambo jema.

Mangula alikuwa na jukwaa zito la kusimama na kusema kwa ukali mkubwa alipokuwa Katibu mkuu wa CCM. Kwa sababu azijuazo yeye alinyamaza na kumezea kutetea watu wengi walo banwa na utaraibu mchafu wa CCM.

Mangula nyamaza kimya, endeleza kilimo cha Viazi maana ni sehemu ya itikadi ya CCM.
 
Mkuu FMES heshima mbele, Tunapochangia hapa tufikirie kwamba Mangula aliyasema haya maneno mwaka 2007 baada ya uchaguzi mkuu wa CCM. Kisutu ni ya 2008 hebu tumtendee haki huyu bwana pia.

- Kwa hiyo una maana tunajadili habari ya mwaka 2007 huu mwaka 2009?
 
Mangula baada ya kupigwa chini na mtandao ndiyo anajifanya ana machungu na nchi.Hana lolote huyu mzee anatapatapa tu.Kwa mfano kikwete angempa ubalozi fulani kama mwenzake Mapuri au angeshinda ule uchaguzi wa Iringa angepiga hizi kelele za kumtaka Sokoine CCM?
 
Share,
Mang'ula kama mlinzi wa benki ikitokea wizi ni lazima yeye akubali makosa sio lazima naye awe ameshiriki kuiba.

Kama alijua kuna matatizo kama haya na kashindwa kuwa Sokoine kama alivyosema MiratKad then hana sababu ya kusema yote haya kwani alipewa nafasi na uwezo wa kulinda,
 
Nimekuwa nikalaumu sana humu ndani kwa kuturejeshea mada za kale hapa pasipo kuarifiana mapema kuwa tumeirudisha kwa sababu fulani fulani.

Watu wanamchamba mkuu mangula kana kwamba haya yamejiri leo kumbe hapana!!!
 
Nimekuwa nikalaumu sana humu ndani kwa kuturejeshea mada za kale hapa pasipo kuarifiana mapema kuwa tumeirudisha kwa sababu fulani fulani.

Watu wanamchamba mkuu mangula kana kwamba haya yamejiri leo kumbe hapana!!!
 
Sijaipenda kabisa kumbe ni ya October 31,2007. mbaya sana! nilijua Mangula karopoka kabla ya mwaka mpya 2009 kumbe ya zamani za kale kabla hata EPA hawajatinga kizimbani,mkuu Mgonja,Yona na Mramba hawajafikishwa mbele ya sheria! nini hii??
 
Nimekuwa nikalaumu sana humu ndani kwa kuturejeshea mada za kale hapa pasipo kuarifiana mapema kuwa tumeirudisha kwa sababu fulani fulani.

Watu wanamchamba mkuu mangula kana kwamba haya yamejiri leo kumbe hapana!!!

Duh, hata mimi nimepigwa bao. Mchezo mchafu huu.

Anyway, Mangula anajiliza kwa vile kapigwa chini. Kesho alirudishwa kuwenye ulaji hutamsiki katu!!!!!!!!!!! Ajue kuwa ni zamu za akina Masha, Mathayo, Nchimbi, Membe n.k.
 
Wakuu, heri za sikukuu ya Pasaka.... Leo katika pitapita zangu nimeikuta hii kule kwa ndugu yetu Issa Michuzi, ni kumbukumbu ya miaka 25 tangu Waziri Mkuu wetu wa wakati huo Hayati Edward Moring Sokoine alipotutoka kwa ajali ya gari.

Kama mwanaJF, jamii ya wapenda mabadiliko, naamini kwamba Sokoine alikuwa ni mmoja wa watu ambao walileta mabadiliko sana nchi Tanzania haswa katika yafuatayo:

1. Fagio la chuma - uzembe kazini
2. Wahujumu wa uchumi - mafisadi wakubwa kwa wadogo
3. Na mambo mengi ambayo aliweza kuyafanya katika kuhakikisha kwamba jamii ya waTanzania inaishi kwa raha na kuwapatia maendeleo wananchi wenzake.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake. Edward Moringe Sokoine, waTanzania tunakukumbuka! Pumzika kwa amani baba!
 
Asante sana kwa kutukumbusha , huyo ni mmoja wa watu muhimu sana waliokuwa na uchungu na Taifa letu. Mungu ailaze pema roho yake. Tungekuwa mbali sana hadi leo hii angekuwa hai.
 
Kwa uadilifu na kutoweka masilahi yake mbele hataweza kamwe kulinganishwa na kiongozi yoyote aliyewahi kushika wadhifa wa u-PM, labda Mwalimu pekee. Baada ya miaka 21 kulikuja Edward mwingine, aliyedai kuwa kabila hilo hilo la mwana wa watu, lakini tofauti za hawa wawili zilikuwa kama vile usiku na mchana.

Yule wa awali baada ya kuingia tu akaanza kwa dhati kuwasumbua mafisadi (wahujumu uchumi), huyu wa baadae, baada ya kuingia tu akakung'uta ulaji mmoja kababmbe wa kihistoria -- Richmond ambao ulimuondoa!
 
Katika soma yangu jf nimeona kuna watu mbalimbali sana na lazima kuna watu watakuwa wanajua walau nini kilichomtokea sokoine.

Kuna njia kuu tatu zimekuwa zikitumika kuua viongozi africa ambazo zote zinasababisha na ajali ya gari
1. Kuchezea matairi mwenyewe akiwa hayupo (sio popular sana)
2. Kukata break pipe (hii ni nzuri sana kwa ajili kupata ushahidi ni shida lakini inahitaji timing ya hali ya juu sana sana mtu akiwa katikati ya safari akapumzika lodge, haitumiki sana)
3. Head on collision (hii ni popular sana kwa ajili inahitaji simu tu) na ndio imekua ikiua watu wengi sana africa..

Turudi kwenye mada yetu ya sokoine
sokoine alipopata ajali alikuwa na muandishi wake wa habari kiti kimoja. Mwandishi wake alikuwa anaitwa acagoda chiledi, huyu jamaa alikuwa ni mmakonde wa msumbiji lakini alibobea tz.

Acagoda chiledi alivyorudi nyumbani shati lake lilikua limejaa damu akaulizwa nini akasema sokoine amepata ajali na amefariki, kwa hiyo katika kumsaidi ndio damu zikawa zimetapakaa kwenye shati lake.
Chiledi alikuwa amekaa nae kiti kimoja kama ilivyokuwa kawaida yake, je inawezekanaje sokoine atokwe na damu kihasi hicho alafu yeye hata kuhumia kidogo.

Maisha ya acagoda baada ya ajali ya sokoine
1. Alikuwa na mke na watoto wa tano, mke wake alikuwa anafanya kazi redio tanzania kama sikosei ni mhasibu sijui wa level gani.

2. Haukupita mda jamaa alienda zimbabwe kufanya kazi ya uwandishi wa habari na hakurudi mpaka baada ya miaka miwili.

3. Na alivyorudi hakukaa kabisa
4. Na kuanzia hapo akawa anakuja baada ya mda mrefu sana na hakai hata wiki moja

5. Alivyokuwa akija holiday alikuwa ni mtu mashaka sana hatulii na anabadilisha mode of transport kila mara ie( gari, miguu, taxi, basi). Alikuwa anaishi maisha ya ujanja ujanja kama mzee mmoja alikuwa anaitwa chiume (alikuwa anatafutwa na banda).

6. Baadae akawa haji kabisa tz, hata mazishi ya mke wake sikumbuki kama alihudhuria

kama kuna mtu ana jua lolote kuhusu sokoine na huyu mzee atudokezee
watu waliofanya nae shihata.
 
Hakuna chakujadili. The autopsy was conducted by Prof Shaba and after many years kuna siku alilewa chakari akaanza kuropoka akasema jamaa alikuwa na bullet holes. Sokoine was killed by the Stalin/Mao/Lennin side of our soon to be saint... U know WHO.. Simple as.

The Saint has ultimate power within the country at the time and no one could have acted without his knowledge or approaval. Thats what it is.
 
Hakuna chakujadili. The autopsy was conducted by Prof Shaba and after many years kuna siku alilewa chakari akaanza kuropoka akasema jamaa alikuwa na bullet holes. Sokoine was killed by the Stalin/Mao/Lennin side of our soon to be saint... U know WHO.. Simple as.. The Saint has ultimate power within the country at the time and no one could have acted without his knowledge or approaval. Thats what it is.

Kinyambisi... could you elaborate more pse? Why our 'soon to be saint' killed him? What was the motive?
 
Hakuna chakujadili. The autopsy was conducted by Prof Shaba and after many years kuna siku alilewa chakari akaanza kuropoka akasema jamaa alikuwa na bullet holes. Sokoine was killed by the Stalin/Mao/Lennin side of our soon to be saint... U know WHO.. Simple as.. The Saint has ultimate power within the country at the time and no one could have acted without his knowledge or approaval. Thats what it is.
why did the saint kill him?
did he killed him so that the precidency can go to mwinyi?
the saint was not going to stand in 1985, then why did he kill him?
 
Acheni speculations za ajabu ajabu Sokoine alikufa kwa ajali ya gari tu hakuna zaidi.

Hata Mwakyembe angekufa msingeacha kusema kuna mkono wa mtu huku dereva wake akijua dhahiri makosa yake ya kiuendeshaji.Sasa kila anayekufa kwa ajali ana sababu ya kusingiziwa kuuwawa tuu.Kwani siye waTz tukipingana au kuzidiana nguvu za hoja basi tunauana kwa ajali ooh kuserereka oooh safari za usiku n.k Je madereva hawa wanaouwa watu kibao kila kukicha basi zima watu kumi ,saba,hamuwasemi ila wa viongozi ndo tu wanasababishiwa vifo???

Tatizo lipo katika elimu ya barabarani kwa madereva wetu,wawe wa viongozi wawe wa magari ya abiria,malori n.k hakuna hata mmoja mwenye elimu ipasayo ya kuendesha magari. Achilia mbali wale wanajifunza katika chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT) ambapo ni ubabaishaji mtupu,Si lolote si chochote kwani hata hao wakufunzi wenyewe hawakuwahi kuendeshagari zaidi ya nadharia tuu.

Leo hii katika barabara za Jiji la Dar Es salaam mtembea kwa miguu hana uhakika wa kufika salama aendako kisa hofu ya kugongwa na wendawazimu hawa tunaowaita madereva!!! Hakuna dereva wa kweli hapa bongo wote ni walenga madaraja na wauwaji wa watu tuu!!! Elimu mathubuti inahitajika ili waendeshao vyombo vya moto, waendao kwa miguu na watumiaji wengine barabara wapate kupona.

Sokoine, Salome Mbatia na wengine waliokufa barabarani ni kwa uzembe wa madereva tu na wala si vinginevyo.
 
Dubisan Dube, yuko South African Railways. Inasemekana anakataa kuendesha gari lililomgonga Sokoine!!!? I can't say anything kuhusu hilo, isipokuwa mimi naamini ni ajari ndo iliyochukua maisha yake.Hayo mambo mengine kama yapo basi yatakuwa ni matatizo ya walo husika kuyafanya.

Naamini Sokoine alisimama imara kujaribu kuyaondoa matabaka yaliyojengwa kwa rushwa na ndilo ninalomkumbukia.
 
mimi naamini lisemwalo lipo
wenye data zaidi watuhabarishe kuhusu huyo saint
 
Back
Top Bottom