Tunamshukuru Waziri wa Ulinzi, Innocent Bashungwa kwa kuongelea ‘malengo’ ya ubinafsishaji wa bandari za Tanzania

Wadanganye wajinga
Hujamsoma mleta mada mpaka mwisho, ukianza kumsoma mwanzo namna alivyomsifia Bashungwa kwa kuelezea malengo ya uwekezaji, unaweza kudhani ndio aliishia hapo.

Lakini chini ameelezea vyema, lucha ya nia nzuri ya uwekezaji iliyonayo serikali, kama kuongeza ufanisi, na kupunguza gharama za uendeshaji kwa serikali, bado ule mkataba wa bandari una maeneo kadhaa yanayotiliwa shaka, ametoa mfano aa kifungu namba 2 (1) kuhusu aina na wigo wa mkataba wa uwekezaji kati ya Tanzania na Dubai.

Kwa kifupi ameleezea vizuri sana, kwa kuonesha vile nia nzuri ya serikali kwenye uwekezaji, inavyoweza kuharibiwa na uwepo wa mkataba mbovu kama ule wa bandari na waarabu, kama ambavyo ameonesha kwenye andiko lake kupitia terms za kwenye ule mkataba.
 
Wale wale hakuna jipya
 
Ahsante sana mama Amon.
Tanzania inaongozwa na wasioipenda.
Wakati mwingine huwa nakaa nafiikiria yanayoendelea nchini ni kana kwamba MAPINDUZI YALIFANYIKA kuiweka serikali iliyopo madarakani.
Maana haiwezekani kamwe kwa mtu ambaye umepokea tu utawala kwa kudra za Mwenyezi Mungu, kwenda kinyume na sera za mtangulizi wako kama kweli wewe na yeye mlikuwa kitu kimoja!
 
Siku hizi JF ina vilaza wengi!! Wavivu wa kusoma lakini wepesi wa kuandika utumbo. Kama hujasoma mada ya nini kuchangia??
Kweli hawajasoma madini ya mama Amon.
Ofcourse kwa mvivu wa kusoma, anaweza asimwelewe mama Amon, lakini kwa aliyesoma article nzima, nama wa watu kahitimisha vzr sana.
Tunawataka wazalendo kama kina nama Amon.
 
Hizi nadharia zako zipeleke darasani mwacheni Rais afanye kazi yake. Badala ya kupoteza muda wako katafute kazi ya kukuingizia kipato
 
Tumia akili, Bashugwa ni waziri ulitegemea aseme kinyume na maamuzi ya baraza la mawaziri ambayo mwekiti wake ni Rais? Tutumie akili sazingine.
 


Namba ya simu umesahau
 
Sawa, ila na hoja hizi pia zijibiwe....

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Bashungwa mdomo wake umepinda, uko tenge hasa akiwa anaongea propaganda
 
Nitakutafuta nikija Sumbawanga, umeongea Mambo ya Msingi Sana.
 
Amekutuma au wewe ni yeye? Anaongea pumba tupu halafu mnasifiana ujinga. Kumbaff

NImemsifia kwa kuongelea alengo mema ya ubinafsishaji wa bandari

NImekosoa mbinu haramu zinazotumika kwenye ubinafsishaji wa bandari kwa kuonyesha kuwa kinahoendelea pale ni ubinafsisiahji bila kufuata sheria ya PPP na kanuni zake

Kosa liko wapi?

Nasubiri jibu lako
 
Asante sana Mungu Kwa uumbaji na kipawa Cha akili na maarifa Cha huyu Mama Amon Desk 💞💞💞💞👋👋👋
 
Amekutuma au wewe ni yeye? Anaongea pumba tupu halafu mnasifiana ujinga. Kumbaff
Naimani hujasoma andiko hili la Mama Amon mpaka mwisho. Kiufupi hajamsifia huyo waziri wa Ulinzi Bashungwa bali ameonesha udhaifu wa maelezo ya waziri wa Ulinzi kuhusiana na mkataba huu.
Hii hali ya kuangalia bandiko limewekwa na nani na kuconclude tu kuwa litakuwa limeegemea mlengo fulani tuiache na tusome mpaka mwisho ili kujua hoja zimeegemea upande gani na kizichambua.
Nakusifu sana mleta mada kwa uchambuzi huu yakinifu na kuonesha mapungufu ya mkataba ambayo serikali na watendaji wake hawayaoni sijui makusudi au kwakuogopa kwenda kinyume na mama. Kiufupi huu mkataba ukiingia kwenye implementation bila mabadiriko ya vifungu ambavyo vipo wazi kabisa kuipokonya mamlaka serikali ya Tanzania juu ya rasilimali zake hakika baadae tutawatafuta mtaani hawa viongozi baada ya madhara yake kuanza kuonekana.
 
Wananchi wa wapi mliogoma?!!! Sisi watanzania tupo na mama na msimamamo wetu uwekezaji ufanyike......nyie vibaraka a.k.a mapimbi wa wapigaji hamtutishi kwa lolote.
Wewe unamuuliza mwenzio ni wananchi wa wapi waliogoma halafu na wewe unarudia kosa lile lile la uliyemkosoa la "sisi watanzania tupo"!!??
Nami nakuuliza kilaza wewe, ni watanzania gani ambao wapo na mama!!???
 
Bashungwa na bandari wapi na wapi?
Walio pewa dhamana ya kuendesha wizara ya uchukuzi kila kiongozi na jibu lake.
Upuuzi kabisa
Tunataka bandari zetu zirudi

Tusimpuuze Bashungwa kwa sababu zifuatazo:

1. Ni Waziri wa Ulinzi na hivyo anayo dhamana kubwa kuhusu usalama wa nchi, jambo linalomfanya kuwa miongoni mwa washauri wakuu wa Rais

2. Ni mchumi ngazi ya Masters na hivyo anaelewa vema nadharia ya ubinafsishaji

3. Amefanya kazi benki ya Dunia na hivyo anaelewa vema 'practice' ya ubinafsishaji

4. Kwa hulka yake ana kipaji cha kusikiliza na kujibu baada ya kuelewa, na baada ya kuelewa yuko radhi kukaa kimya kuliko kusema uwongo (mental reservation)

Mtu mwenye sifa hizi tunapaswa kumshirikisha dukuduku zetu kwa hoja bila kejeli, masiango wala matusi.

Uandishi wa uzi huu umezingatia yote haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…