Mkuu usiingize Siasa kwenye uchumi, monetary policy ipi imebadilika ghafla? Kipindi Cha 2020-21 JPM ndio alitoa mkopo wa Trillion 1 kwa mabenki yaani Trillion nzima iliingizwa kwenye mzunguko..... Funny enough ndio alishusha bank rate, reserve requirement na masharti ya agency banking, M Pesa Ili kuongeza mzunguko wa pesa. So linapokuja suala la monetary policy Wala hazikubadilika mwaka 2021-22!!
Kingine Mfumuko wa bei ni kutokana na vita ya Ukraine kiufupi mfumuko ni dunia nzima lakini vile vile kukosekana ubunifu serikalini wao wanajua tozo tu na makodi wanashindwa kubuni vyanzo vipya.
Ilipaswa wakate matumizi yasiyo ya lazima ikiwezekana kususpend Miradi isiyo na priority Ili hiyo pesa iwekwe kwenye kusubsidize Bei za vyakula Ili gharama ya maisha ishuke.
All in all wakulaumu sio Samia tu ni CCM nzima kuanzia bunge linalopitisha matozo na baraza la mawaziri linalofanya kazi kwa mazoea tu. Kuna wakati unatamani hata baraza la mawaziri ukodishe nchi za wenzetu wafanye consultancy ya miezi 6 pengine tunaweza ona matokeo chanya!!