Hivi ukiwa na wabunge wenye mambo ya kitoto kama wale pale Dodoma unawezaje kumlaumu Rais ambaye amewakuta na ikamlazimu kuwaangalia wanavyodmka na kuruka sarakasi kwenye maiki Bungeni.
Bunge la hovyo haliwezi kumshauri Rais unless awe dikteta ambaye bunge halina umuhimu wowote.
Kwa Katiba tuliyonayo na wabunge tulionao huyu Rais hatafanikiwa kirahisi kwani katiba tuliyonayo ni ya Kidikteta na inasimamiwa Kidikteta na maamuzi ya Kidikteta.
Ili Mama yetu SSH afanikiwe ni lazima akubaliane na wazalendo waliokua wamepambana na majizi tangu awamu ya pili na wanaomshauri alete katiba mpya inayoruhusu mifumo kujiendesha yenyewe na wapiga DILI kuchujwa na kukaa pembeni. Wateule wake wengi hawana usafi Kwa historia Hali inayowafanya watu wote kutafuta namna ya kula hata Kwa kukata kamba. Wanaona kama vile Kuna fursa ya kula Mali za umma imeruhusiwa.
Hii sio katiba ya kidemokrasia hivyo kuitumia katiba hii Kistarabu ni sawa na kumwekea pumba Nguruwe na Kondoo kwenye zizi Moja. Tahadhari ya kumfuga NGURUWE haiwezi kuwa sawa na Kondoo.
Bunge limeonyesha wazi kuwa lipo pale Kwa lengo la kupata pesa tuu. Ndio maana Kuna Wabunge 19 waliokua wameshindwa kwenye majimbo yao na wakaamua kujipeleka Bungeni na kushirikiana na Ndugai Kwa kumpa zile walizokuwa wanatoa kwa wakubwa zao.
Hawana Chama lakini wapo Kwa lengo Moja tu la Kupiga pesa za umma na wapigaji wenzao.
Kama Bunge linaruhisu wabunge HARAMU kulipwa mamilioni ya pesa iweje serikali ilaumiwe na wakati ule ni mihimili.? Kama mahakama nayo inatumiwa na wapigaji kuendelea Kupiga pesa za Bunge bila kuwa na Chama huoni kuwa hii nchi INAPASWA kuongozwa kidikteta full ili iwe kama Rwanda chini ya Kagame .
Ujinga wa kuchezea Mali za umma ndio unaoturudisha nyuma na kusingizia Vita. Mpaka asali nayo Nyuki wamegoma kutengeneza Kwa sababu ya Vita. Ajabu kabisa. Watu wanazuia watu kumwagilia mashamba yao eti maji yaende kwenye mabwawa ya umeme Karne hii. ,,