TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Imani inaweza kutoa matokeo chanya lakini papo hapo imani inaweza kuvunja matokeo uliyoyapata.
Jana waislamu leo wasabato na baadaye ni mchanganyiko wa makanisa kuiombea nchi dhidi ya janga la corona, unadhani Mungu anaweza kuponya taifa ingali lipo wazi?
Hapa tunacheza na imani, imani iliyonenwa kwenye misahafu haiwezi kutokea wakati huu ambapo mtu anafanya maasi alafu anamtaja Mungu, hii haiwezekani hasirani.
Makanisani waumini wamekuwa bendera fuata upepo, wanamsikiliza sheikh, mchungaji hama askofu akitoa kauli ya uzima/kuchukua hatua stahiki za kujikinga na corona kesho wanamsikia baba mwenye nyumba anasema achana na hizo kauli za kiongozi wako wa dini.
Hali inazidi kuwa mbaya; moja ya marumbano haya hayawezi kuleta majibu chanya zaidi ya kuvunja imani waliyonayo wanao ongozwa.
Hili taifa kwa sasa linajizolea sifa za kujulikana huko na kule kwa taarifa mbaya za kutochukua hatua dhidi ya covid, ukumbuke hatua stahiki zinatokana na kiongozi mkuu kutoa tamko na si mwanachi mmoja mmoja kujichukulia hatua, HAPANA.
Kwa maombi na kufunga hakutaondoa covid hata siku moja ingali taifa lipo wazi kila anayetaka kuja na aje, wengine si watalii, wala watafiti ila wanatumwa kuja kufanya uhuni mkubwa sana unaoweza kupelekea madhara ambayo tutayajutia huko mbele.
Bado serikali inapaswa kuwa makini na wageni wanao ingia nchini, kwa kisingizio cha kuja kutalii ilihali wakifika airport wanapimwa joto na kuruhusiwa kuzama ndani bila bugudha.
Namalizia tena, tunamuomba Mungu huku tukiwa uchi, unategemea nani atazuia macho yake yasikuone?
Alamsiki.