Tunamuomba Mungu atukinge na Corona, kesho watalii wanatua KIA, AKIA, JNIA huku nchi ikiwa wazi mipakani

Tunamuomba Mungu atukinge na Corona, kesho watalii wanatua KIA, AKIA, JNIA huku nchi ikiwa wazi mipakani

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Imani inaweza kutoa matokeo chanya lakini papo hapo imani inaweza kuvunja matokeo uliyoyapata.

Jana waislamu leo wasabato na baadaye ni mchanganyiko wa makanisa kuiombea nchi dhidi ya janga la corona, unadhani Mungu anaweza kuponya taifa ingali lipo wazi?

Hapa tunacheza na imani, imani iliyonenwa kwenye misahafu haiwezi kutokea wakati huu ambapo mtu anafanya maasi alafu anamtaja Mungu, hii haiwezekani hasirani.

Makanisani waumini wamekuwa bendera fuata upepo, wanamsikiliza sheikh, mchungaji hama askofu akitoa kauli ya uzima/kuchukua hatua stahiki za kujikinga na corona kesho wanamsikia baba mwenye nyumba anasema achana na hizo kauli za kiongozi wako wa dini.

Hali inazidi kuwa mbaya; moja ya marumbano haya hayawezi kuleta majibu chanya zaidi ya kuvunja imani waliyonayo wanao ongozwa.

Hili taifa kwa sasa linajizolea sifa za kujulikana huko na kule kwa taarifa mbaya za kutochukua hatua dhidi ya covid, ukumbuke hatua stahiki zinatokana na kiongozi mkuu kutoa tamko na si mwanachi mmoja mmoja kujichukulia hatua, HAPANA.

Kwa maombi na kufunga hakutaondoa covid hata siku moja ingali taifa lipo wazi kila anayetaka kuja na aje, wengine si watalii, wala watafiti ila wanatumwa kuja kufanya uhuni mkubwa sana unaoweza kupelekea madhara ambayo tutayajutia huko mbele.

Bado serikali inapaswa kuwa makini na wageni wanao ingia nchini, kwa kisingizio cha kuja kutalii ilihali wakifika airport wanapimwa joto na kuruhusiwa kuzama ndani bila bugudha.

Namalizia tena, tunamuomba Mungu huku tukiwa uchi, unategemea nani atazuia macho yake yasikuone?

Alamsiki.
 
Nimekumbuka stori ya nyoka wa shaba ambaye Musa aliagizwa na Mungu amtengeneze jangwani iwe uponyaji kwa wale wote waliomtazama nyoka huyo baada ya kung'atwa na nyoka.

Sijui kwa nini Mungu hakuwaondoa nyoka, bali akaagiza nyoka wa shaba atengenezwe.
 
Aya unganisha na hii hapa👇🏾;
"Mwenyezi Mungu ana kazi nyingi za kufanya. Anaangalia dunia nzima. Hawezi akawa hapa Uganda tu akiwaangalia wajinga (punguani)".

Ni kauli ya rais Museveni akiwatahadharisha Waganda wanaokiuka miongozo ya Serikali dhidi ya Corona.
 
Kama uliandikiwa na kupangiwa utapata Corona hata ufanyejee

Bora mkono unakwenda kinywani na unaqunyer ni jambo jema na la kumshukuru Mungu.
 
Kama uliandikiwa na kupangiwa utapata Corona hata ufanyejee

Bora mkono unakwenda kinywani na unaqunyer ni jambo jema na la kumshukuru Mungu.
Wewe peke ako ndo umeongea la maana.

Watu wanajisahau kuwa kila kifo hakiji bure bali ni kwa mpango wa Mungu.

Na ikumbukwe kwamba kuna malaika maalumu wa idara ya kutoa roho,.

Roho haitoki yenyewe yenyewe tu.
 
ndio maana hadi leo hii wapo wanao ambukizwa virusi vya ukimwi sio kwamba hawajui njia zinazo sababisha maambukizi ya ukimwi, wanazijua!!!
 
Kama uliandikiwa na kupangiwa utapata Corona hata ufanyejee

Bora mkono unakwenda kinywani na unaqunyer ni jambo jema na la kumshukuru Mungu.
Wewe peke ako ndo umeongea la maana.
Watu wanajisahau kuwa kila kifo hakiji bure bali ni kwa mpango wa Mungu.

Na ikumbukwe kwamba kuna malaika maalumu wa idara ya kutoa roho,.
Roho haitoki yenyewe yenyewe tu.
Aseee😲!.
Nimeshangazwa sana na komenti zenu do!.

Yaani kwa sababu umehaidiwa kufa na malaria basi uache mbu wakung'ate, umeandikiwa utakufa kwa njaa basi uache nzige wamalize mazao shamba, kisa kifo hakiji bure.

Nadhani hamjaelewa andiko kwa undani, mmesoma kwa speed mkijandaa kwenda kanisani, mkirudi msome mkiwa mmetulia asee!
 
Wewe peke ako ndo umeongea la maana.

Watu wanajisahau kuwa kila kifo hakiji bure bali ni kwa mpango wa Mungu.

Na ikumbukwe kwamba kuna malaika maalumu wa idara ya kutoa roho,.

Roho haitoki yenyewe yenyewe tu.
Nyie ndio mitaji ya manabii na mapastor fake, yaan hamtakagi kutumia hata chembe ya akili zenu kureason mnamtegemea tu nabii/pastor
Unaacha kujilinda unasema kama uliandikiwa kufa kwa corona utakufa😀😀

Ulishawahi kujiuliza kwa nini unafunga mlango nyumbani? kwa nini unatumia neti?, kwa nini ukivuka barabara unaangalia kushoto na kulia n.k. kwa nn usiache kutumia net uumwe na mbu kama haijaandikwa ufe kwa maralia hautokufa.

Kama Mungu ameandika sababu ya mtu kufa hukumu isingekuepo, iweje uandike mtu atakufa kwa magonjwa ya zinaa alafu badae umuhukumu kwa kuzini?
Walokole mnashida sana mtu akifail au kushindwa chochote anasingizia Mungu kapanga/ kaandikiwa😀😀😀😀

Imeandikwa tutakufa lakini utakufaje na kifo gani ni aina ya maisha yako.

"WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA" huu mstari unawahusu.
 
Tatizo kuna watu hawaamini uwepo wa qadar wamefikia hatua ya kusema kama mungu wenu yupo kweli basi mungu wenu atakuwa katili sn, wayahudi walifikia hatua ya maneno ya dhiaka juu ya uwepo wa mungu mwisho wa siku walikipata walichokitafuta. wapo watu katika huu ulimwengu pumzi zinawaada ila muda si kidogo watajua tu time will tell
Kama uliandikiwa na kupangiwa utapata Corona hata ufanyejee

Bora mkono unakwenda kinywani na unaqunyer ni jambo jema na la kumshukuru Mungu.
 
NA SIJUI SABABU KUBWA YA KUBISHIA KUHUSU UWEPO WA KORONA NA KUBISHIA KUHUSU NJIA ZA KISAYANSI DHIDI YA KORONA.
SIJUI UBISHI HUU UNATOKANA NA NINI. MBONA MAGONJWA MENGINE HATUBISHI?
Hapa kuna mtu anataka kuonyesha kuwa yeye ni nani dhidi ya walio wengi.

Unaposema magonjwa mengine yapo na hakuna ubishi ni kwa sababu hayo magonjwa chanjo zake zinatoolewa na hazipingwi na hata anayepinga hii chanjo alipokuja duniani aliikuta ipo na akachomwa as kinga.

Iweje leo unaniambia siamini hizo chanjo wakati unatumia zile nyingine?
 
tusiigeuze corona Kama wimbo wa taifa.Tanzania tuna mengi ya kufanya.ilikuja ,itaondoka.hakuna Jambo lisilokuwa na e dot(.)
 
Aya unganisha na hii hapa👇🏾;
"Mwenyezi Mungu ana kazi nyingi za kufanya. Anaangalia dunia nzima. Hawezi akawa hapa Uganda tu akiwaangalia wajinga (punguani)".

Ni kauli ya rais Museveni akiwatahadharisha Waganda wanaokiuka miongozo ya Serikali dhidi ya Corona.
sasa tufanye suluhisho liwe lipi
 
Daah hapo kwa watalii namim nadhani pana walakin serikal inabidi itimie jicho la tatu wachunguze na mabegi yao wasijeleta tuvirusi
Hapa hakuna kumzuia mtu kisa corona, hujasikia kuna mechi ya mamelody, na warabu wanakuja kucheza hapa?waarabu wameogopa virusi vipya vya south!!wameomba mechi ichezwe TZ?Na wamekubaliwa?!!hapa hata kupima ni geresha tu,
 
Back
Top Bottom