Pre GE2025 Tunamuomba Rais Samia atembeze kipigo cha mbwa koko kwa wote wanaotaka kuandamana

Pre GE2025 Tunamuomba Rais Samia atembeze kipigo cha mbwa koko kwa wote wanaotaka kuandamana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna cinema ya ‘South Korea’ kwenye chaguzi zao kuna vyama viwili vikuu cha kikomunisti na kingine cha kibepari.

Ukikaribia uchaguzi kile chama cha kibepari wana jamaa yao wa usalama ‘North Korea’ yupo karibu na raisi. Basi zikianza kampeni wanaanza kuponda sera za ukomonunisti na kuiponda ‘North Korea’ kama dictator state.

Wakati majukwaani wanaiponda ‘North Korea’ na ukomonusti nyuma ya pazia wanamwita jamaa yao wa North Korea na kumshawishi amwambie raisi wao atishie kuivamia ‘South Korea’ na kufanya mazoezi ya kurusha makombora ili wawatishe wananchi wao halafu watamlipa hela ili wapate kura za uchaguzi.

Uchaguzi ukipita usikii tena habari za North Korea, kutaka kuivamia South Korea.

Ndio CHADEMA kama maigizo kwenda mbele ukata ukiwapiga washajua ‘Bi Tozo’ anawamwagia kichele watulie na Mbowe ndio mnufaika mkubwa.

Huu upuuzi wa kulipana hela ndio Magufuli alikuwa autaki mambo ambayo Mbowe na Zitto hawajazoea kukosa maokoto ya bure bure.

What a pity
Kwenye maandishi,kwa mujibu wa walimu wangu, kama unakosea hata "a" na "h", huwezi kuaminika.

Kumfananisha Mbowe na Zitto ni kuonyesha jinsi usivyo timamu kwenye sehemu zinazopaswa kuwa timamu.
Kisheria tunaita " null & void".
 
Kama una akili vizuri, hapo unamwambia Rais aanzishe vurugu 🤣🤣🤣🤣🤣
Utaratibu wa kuleta vurugu na maandamano ili kuvunja amani na kuleta mifarakano isiyo ya lazima haikubaliki na ni lazima raisi asimame kidete kwa watu wanaotaka kuleta fujo na vurugu.

Hali ngumu sio Tanzania tu, Nenda Kenya kaulize kuhusu garama za maisha je zipo chini? Hawa si wana tume huru, simatokeo yao yanahojiwa mahakamani, mshindi lazm apate 50%+1

Nadhani tufuate njia ya mazungumzo,maridhiano na kuvumiliana.

Ubabe haujawahi kushinda hata Raila Odinga huko kenya kaandamana watu wamekufa ,then wakarudi kuzungumza.

nasema wavunja amani Raisi asicheke nao hata kidogo
 
Kwenye maandishi,kwa mujibu wa walimu wangu, kama unakosea hata "a" na "h", huwezi kuaminika.

Kumfananisha Mbowe na Zitto ni kuonyesha jinsi usivyo timamu kwenye sehemu zinazopaswa kuwa timamu.
Kisheria tunaita " null & void".
Mwambie Mwalimu wako akufundishe ku analyse, evaluate, explain and writing structure; huko ndio kuna 90% ya marking, grammar 5% na referencing 5%.

Usikadhane na writing, hata best sellers wana editors, magazeti yana wahariri kupitia texts zinazoandikwa na professionals.

Spelling ni sehemu ndogo sana ya academia.

Ingekuwa writing skills ndio kigezo cha marking waafrika wengi sana wasingekuwa wanafaulu ulaya, wengi kuandika kizungu shida hasa watanzania.

Back to the topic at hand, Mbowe ni msanii; hiyo mikwara tu ya kurushiwa maokoto.

Mambo anayopenda Mbowe ni yale ya mchango wa kanisa badala ya raisi kuutoa moja kwa moja nyumba ya mungu anataka ipitie kwake.

Kuna makanisa mangapi Tanzania why raisi achangie la Hai na msaada wenyewe upitie kwa Mbowe.

Hiyo ni tishia toto anataka apewe hela za kutuliza mzuka uchwara wa CDM.
 
Bado hujaropoka. Kauli moja ya maandamano chawa mmeamka kutoka pangoni.
Wewe subiri Mbowe aanzishe harambee zake uchwara, huyo huyo asiemuini atakwambia kachangia millioni 200 ambazo zitakapoenda hujui na wala utouliza.
 
Back
Top Bottom