Tunaokolewa kwa Imani sio kwa kufuata Sheria

Tunaokolewa kwa Imani sio kwa kufuata Sheria

Sasa tumalize

endelea kujifunza biblia uelewa wako ni mdogo sana ba hao walimu uliokuwa nao ni waongo

tumalize kwa kusema nakushauri muamini yesu na pamoja na kuzishika amri zake kwa pamoja tangu umesema kuwa amri zake sio mbaya zinakatza mambo mabaya na machafu zishike utaokolewa mara moja kama vile ndoto yako ilivyo.
Sheria ilikuja kwa mkono wa Musa na inamapungufu, Lakini neema na Kweli imekuja kwa mkono wa Kristo.

Unachagua kukaa na nani, Kiti cha Musa cha sheria au utakalia kiti cha Neema na Yesu ?
 
H
Kile kinachozidi akili si lazima kiwe uongo. Mara nyingi ndicho kinachothibitisha mipaka ya mwanadamu na kutufundisha kwamba kuna nguvu kubwa kuliko sisi. Imani ya kweli inajulikana kwa matunda yake na msingi wake katika historia, si kwa kuitwa hekaya za kufikirika.
Haya nipe sasa matunda ya hizo hekaya unazonadi na msingi wake katika historia
 
B
Hii inamaanisha kumpenda Yesu si maneno ya mdomoni pekee. Kama mtu anaendelea kuishi ndani ya dhambi bila majuto wala kupambana nayo, basi ule “upendo” wake ni maneno, si upendo wa kweli.

Pia kuna tofauti kati ya mtu anayejikuta akianguka kwa udhaifu, lakini ndani yake anajuta na kupambana kuacha, na mtu anayekaa kwa makusudi kwenye dhambi huku akijidai “anamfuata Yesu.” Wa kwanza bado ana nafasi kubwa ya msaada wa neema ya Kristo; wa pili yupo kwenye hali ya hatari, maana amezoea dhambi.

Kama tungeokolewa kwa matendo yetu, hakuna anayeweza kusimama. Lakini kupitia imani kwa Yesu, mtu anapata msamaha na nguvu ya kushinda tamaa ya dhambi. Hata wale wanaodai wanampenda Yesu lakini bado wako ndani ya dhambi suluhisho lao si kujificha kwenye dini, bali ni kutubu kweli na kuruhusu Yesu abadilishe maisha yao.

Kwa hiyo, wako wengi wanaosema wanampenda Yesu lakini bado wako utumwani mwa dhambi, hata kwenye madhabahu. Hii inaonyesha upendo wao bado ni wa maneno tu. Upendo wa kweli kwa Yesu huonekana pale mtu anapopokea neema yake, kutubu, na kujikuta akiacha dhambi kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Bado wanadi hekaya zisizo na mashiko?
 
Tunaokolewa kwa imani katika Yesu Kristo na sio kwa kufuata SHERIA.

Tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo na si kwa matendo ya sheria. Wokovu ni kwa neema kupitia imani ya Yesu Kristo, si kwa jitihada za kufuata sheria.

YESU ANASEMA MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU.

KUSHIKA AMRI KIKAMILIFU KUNAKUJA BAADA YA KUMPENDA YESU

KAZI YA SHERIA
1. Sheria huonyesha dhambi, ila haiondoi dhambi
2. Mtu mwenye dhambi hawezi kusamehewa kwa kuanza kufuata sheria bali ataepuka dhambi mpya huku akiwa na zile dhambi za mwanzo.

Yesu ndiye njia ya kweli na uzima. Na moja ya uzima ndio pamoja na uzima katika mwili yaani kuangamiza tamaa zote za mwili ambazo ni uzinzi, uuaji, uasherati, ibaada za sanamu, uongo, wizi, ujambazi, ulevi, fitina, ubinafsi, uchawi, mawazo mabaya, tamaa mbaya, uchafu, ufisadi, ugomvi, wivu, hasira, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo.

Basi ukisha kuwa na imani katika Yesu Kristo anakupatia kiongozi yaani Roho Mtakatifu atakaye kuongoza katika upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi kwasababu upo ndani ya Kristo Yesu yaani tumeusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake mbaya.

True! Ahsante Sana Kwa kuweka huu msisitizo na MUNGU akubariki.
 
na wewe ni wale wa kusema Kama Mungu yupo thibitisha uwepo wake ?
Siwezi kuwa na akili mbovu ya hivyo ya kupingana na nature,mfano wako..mm namuamini Allah kawa muumba wa vyote,asiye na mshirika,amnaye hajazaa wala kuzaliwa na hafanani na chochote.. na naamini katika dini ya haki ya uislam inayoendana na maumbile na asili ya mwanadamu
 
Tunaokolewa kwa imani katika Yesu Kristo na sio kwa kufuata SHERIA.

Tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo na si kwa matendo ya sheria. Wokovu ni kwa neema kupitia imani ya Yesu Kristo, si kwa jitihada za kufuata sheria.

YESU ANASEMA MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU.

KUSHIKA AMRI KIKAMILIFU KUNAKUJA BAADA YA KUMPENDA YESU

KAZI YA SHERIA
1. Sheria huonyesha dhambi, ila haiondoi dhambi
2. Mtu mwenye dhambi hawezi kusamehewa kwa kuanza kufuata sheria bali ataepuka dhambi mpya huku akiwa na zile dhambi za mwanzo.

Yesu ndiye njia ya kweli na uzima. Na moja ya uzima ndio pamoja na uzima katika mwili yaani kuangamiza tamaa zote za mwili ambazo ni uzinzi, uuaji, uasherati, ibaada za sanamu, uongo, wizi, ujambazi, ulevi, fitina, ubinafsi, uchawi, mawazo mabaya, tamaa mbaya, uchafu, ufisadi, ugomvi, wivu, hasira, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo.

Basi ukisha kuwa na imani katika Yesu Kristo anakupatia kiongozi yaani Roho Mtakatifu atakaye kuongoza katika upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi kwasababu upo ndani ya Kristo Yesu yaani tumeusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake mbaya.
Mwafrika anaamini na kutegemea "Mungu na Maraika" Waingilie Mambo ya hapa duniani, kama wanafunzi, kufaulu, kupata kazi, kuoa, na, kuolewa, kuwa, bilionea,
Ila wazungu, wanatumia sayansi, Facebook, iphone, insta, LC 300,lincoln navigator, boieng, hazikutengenezwa kwa maombi! Watu walitumia bongo zao, wakishinda workshop, wakiumia vichwa!
Vitu vyote vizuri tunavyovitumia Afrika, katengeneza mzungu, hakushinda kanisani na bible akiomba na kufunga,
TV, flat screen, magari, train, ndege, tiba za, kisasa,google, insta, havikuja kwa maombi ni akili ilitotumika workshop usiku kucha, sio kufunga na kuomba, miujiza ya kujaza gesi, wala, kuongea kwa lugha.
 
Kumbe mvaa madela 😁
 
Magari, simu, dawa za kisasa, ndege, mitandao ya kijamii na teknolojia nyingine zote kubwa ni matokeo ya sera za nchi zinazowekeza kwenye elimu, tafiti, sayansi, teknolojia na viwanda. Hizo hazitokani moja kwa moja na dini. Nchi zilizopiga hatua ziliweka kipaumbele kwenye elimu bora, vyuo vya utafiti, maabara na warsha, na zikahimiza wananchi wao kutumia akili na maarifa yao.

Kwa hiyo, tatizo kubwa si kwamba “Afrika inaomba sana,” bali kwamba mara nyingi tumekosa sera thabiti na uwekezaji mkubwa kwenye elimu na sayansi. Kama tungeweka nguvu zetu pale, hata sisi tungekuwa tunatengeneza simu, magari na dawa zetu wenyewe.

Dini yenyewe haijakataza mtu kutumia akili au kugundua mambo mapya. Kinyume chake, dini inajenga maadili, nidhamu na uthubutu wa kutumia maarifa vizuri. Hata katika historia ya Ulaya, wanasayansi wengi waliokuwa waanzilishi wa fizikia, kemia na tiba walikuwa watu wa imani, waliamini kwamba akili zao na uwezo wa kuchunguza ulimwengu umetoka kwa Mungu.

Kwa hiyo siyo kwamba “maombi ni kinyume cha maendeleo,” bali maombi bila kuchukua hatua za vitendo na kutumia akili hayataleta matokeo. Biblia yenyewe inasema: Imani bila matendo imekufa.

Kosa kubwa tunalofanya Afrika ni kugawanya mambo: au tunaomba bila kufanya kazi, au tunaona kazi pekee bila imani. Lakini ukweli ni kwamba maombi yanatoa mwongozo na maadili, akili na elimu zinatoa mbinu na uvumbuzi. Mchanganyiko wa vyote viwili ndio uliofanya Ulaya na Marekani zipige hatua kubwa.

Wale unaosema “wazungu” ndio pia wanaoongoza hata kwenye kumwabudu Mungu. Makanisa makubwa, ibada za hadhara, maombi ya kila siku, na nyimbo nyingi nzuri za gospel zinazogusa ulimwengu mzima zinatoka kwao. Hii inaonyesha kwamba maendeleo ya sayansi na ibada ya Mungu havipingani. Walichofanya wao ni kuunganisha imani + akili + kazi.

Na mwisho kabisa nikukumbushe jambo moja muhimu: taasisi za kidini ndizo zimechangia pakubwa kwenye maendeleo ya jamii barani Afrika, hususani Tanzania. Ukizungumzia elimu na afya, taasisi hizi zimekuwa mstari wa mbele. Kwa mfano:

Shule na vyuo: Sekondari za Kanisa Katoliki kama St. Joseph, St. Francis, Marian Girls, Don Bosco, Montfort na zingine ndizo zinazotajwa kuwa bora zaidi nchini. Kuna pia vyuo vikuu kama St. Augustine University of Tanzania (SAUT), Ruaha Catholic University (RUCU), na TUMA (Teofilo Kisanji University) vinavyomilikiwa na taasisi za dini.

Hospitali: Hospitali kubwa na zenye huduma bora pia nyingi ni za kidini, kama Bugando Medical Centre (Katoliki, Mwanza), KCMC (Kilimanjaro Christian Medical Centre, KKKT), Huruma Hospital (Same), na Peramiho Hospital (Songea).

Hii inaonyesha wazi kuwa dini haijakaa kando ya maendeleo, bali ndiyo imewekeza zaidi kwenye sekta muhimu zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Kwa hiyo, kama sera za nchi zingeruhusu na kuhimiza taasisi hizi kuwekeza pia kwenye viwanda na teknolojia, leo tungekuwa na mashirika makubwa ya uzalishaji yanayomilikiwa na makanisa na misikiti, sambamba na shule na hospitali zao. Hilo lingesaidia sana kupunguza utegemezi kutoka nje na kuimarisha uchumi wa ndani.
 
Wewe jamaa ni mbumbumbu sana hii ni kwa mujibu wa biblia au kwa muujibu wa mchungaji wako ?

ndivyo biblia imesema hivyo ?

biblia inasema watakao okolewa ni wale wazishikao amri za mungu

Soma taratibu ili upate kuelewa vizuri. Mungu akusaidie katika jina la Yesu:

Warumi 3:28
“Kwa maana twaona ya kuwa mtu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria."

Wagalatia 2:16
Tukijua ya kwamba mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi nasi tumemwamini Kristo Yesu, tupate kuhesabiwa haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; kwa sababu kwa matendo ya sheria hapana mwenye mwili atakayehesabiwa haki.”

Wagalatia 3:11
“Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu kwa sheria; kwa sababu, Mwenye haki ataishi kwa imani.”

Wagalatia 3:24
“Kwa hiyo sheria imekuwa mlinzi wetu mpaka Kristo aje, ili tuhesabiwe haki kwa imani.”

Waefeso 2:8-9
“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”

Warumi 4:5
“Bali kwake yeye asiye na matendo, bali anamwamini yeye mwenye kumhesabia haki asiyekuwa na Mungu, imani yake huhesabiwa kuwa haki.”

Warumi 10:9-10
“Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kwamba Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”
 
Unajua yesu ndio mungu na mkuu wa sheria hizo ?

Je yesu alizishika sheria hizo ? jibu ni ndio alizishika kwani kuzishika sheria unaelewaje mfano sheria jnasema usizini wewe usipo zini unakuwa umeshika amri ya hiyo moja kwa moja ambayo ni tabia ya mungu kwa kweli yesu hakuwai kuzini, wala hakuwai kuiba wala hakuwa wai kusema uongo, aliwaheshimu wazazi wake.

Hivyo kwa kufuata nyayo za yesu tayari unafuata sheria automatic na sio hazipo kabisa kwani matendo yako ni yale yale ya yesu sio hakuna sheria kabisa unazo zifuata.

Hapa ndipo tunarudi kwenye maandiko mengine ili kutafuta maana ya maneno yako hatuwezi kutegemea maneno machache tu wakati mwengine yanasema tuzishike amri za mungu tunakuwa tunakosea.

Hivyo nafikiri huu mjadara wako wa kuziongelea sheria zinazokataza mambo mabaya hauna msingi wowote.
 
Dunian tunaishi kwa sheria na kanuni na ata imani hufuata sheria na kanuni na huwezi tenganisha imani, sheria na kanuni.
 
Tunaokolewa kwa imani katika Yesu Kristo na sio kwa kufuata SHERIA.

Tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo na si kwa matendo ya sheria. Wokovu ni kwa neema kupitia imani ya Yesu Kristo, si kwa jitihada za kufuata sheria.

YESU ANASEMA MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU.

KUSHIKA AMRI KIKAMILIFU KUNAKUJA BAADA YA KUMPENDA YESU

KAZI YA SHERIA
1. Sheria huonyesha dhambi, ila haiondoi dhambi
2. Mtu mwenye dhambi hawezi kusamehewa kwa kuanza kufuata sheria bali ataepuka dhambi mpya huku akiwa na zile dhambi za mwanzo.

Yesu ndiye njia ya kweli na uzima. Na moja ya uzima ndio pamoja na uzima katika mwili yaani kuangamiza tamaa zote za mwili ambazo ni uzinzi, uuaji, uasherati, ibaada za sanamu, uongo, wizi, ujambazi, ulevi, fitina, ubinafsi, uchawi, mawazo mabaya, tamaa mbaya, uchafu, ufisadi, ugomvi, wivu, hasira, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo.

Basi ukisha kuwa na imani katika Yesu Kristo anakupatia kiongozi yaani Roho Mtakatifu atakaye kuongoza katika upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi kwasababu upo ndani ya Kristo Yesu yaani tumeusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake mbaya.
With all due respect Meneja Wa Makampuni naomba kuleta mtazamo tofauti kidogo kuhusu hii mada.

Ukisoma biblia kwa uangalifu utaona kuwa Yesu hakusema kuwa tutaokolewa kwa imani tu bali kutii sheria ni njia ya kupata wokovu na ndiyo kwanza Yesu mwenyewe alisema tuzitii hizo sheria.

Hebu tuangalie Mathayo 5:17
"Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza".

Hapa tunaona Yesu anasema yeye hakuja kuondoa hizo sheria bali amekuja kuzitimiliza. Maana yake hizo sheria bado zipo na zitaendelea kuwepo

Ukiendelea ule mstari unaofuata Mathayo 5:18
"Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie."

Hapa Yesu mwenyewe anasisitiza umuhimu wa sheria na kwamba hata nukta haitabadilika mpaka yote yatimie.

Aidha Mathayo 5:19 inasema hivi:
"Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni."

Ukivunja amri yoyote wewe utakuwa mdogo sana mbele ya ufalme wa Mbinguni na yule anayeitii ataitwa mkubwa katika ufalme huo.

Tukiachana na hiyo hebu tuangalie tena Mathayo 19:16-22 Yesu alipokutana na kijana tajiri:

16 Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?

17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.

18 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo,

19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

20 Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena?

21 Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.

22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Katika jibu la Yesu kuhusu nini cha kufanya ili arithi ufalme wa Mbinguni alimwambia kuwa azishike amri. Lakini tunavyoona huyo kijana tajiri yeye alikuwa akizishika amri hivyo kwake hilo halikuwa tatizo, cha ziada Yesu alimwambia akauze mali zake na hapo ndipo pakawa pagumu kwa kijana yule tajiri.

Hata hivyo hakuna sehemu Yesu alimwambia yule Kijana kuwa awe na imani juu yake tu na kwa njia hiyo atarithi ufalme wa mbinguni.

Hivyo nachotaka kusisiti ni kuwa sheria bado zipo na zitaendelea kuwepo hivyo tuzishike na kuzitii ili turithi ufalme wa Mungu.

I Submit.🙏🏾
 
Tunaokolewa kwa imani katika Yesu Kristo na sio kwa kufuata SHERIA.

Tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo na si kwa matendo ya sheria. Wokovu ni kwa neema kupitia imani ya Yesu Kristo, si kwa jitihada za kufuata sheria.

YESU ANASEMA MKINIPENDA MTAZISHIKA AMRI ZANGU.

KUSHIKA AMRI KIKAMILIFU KUNAKUJA BAADA YA KUMPENDA YESU

KAZI YA SHERIA
1. Sheria huonyesha dhambi, ila haiondoi dhambi
2. Mtu mwenye dhambi hawezi kusamehewa kwa kuanza kufuata sheria bali ataepuka dhambi mpya huku akiwa na zile dhambi za mwanzo.

Yesu ndiye njia ya kweli na uzima. Na moja ya uzima ndio pamoja na uzima katika mwili yaani kuangamiza tamaa zote za mwili ambazo ni uzinzi, uuaji, uasherati, ibaada za sanamu, uongo, wizi, ujambazi, ulevi, fitina, ubinafsi, uchawi, mawazo mabaya, tamaa mbaya, uchafu, ufisadi, ugomvi, wivu, hasira, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo.

Basi ukisha kuwa na imani katika Yesu Kristo anakupatia kiongozi yaani Roho Mtakatifu atakaye kuongoza katika upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi kwasababu upo ndani ya Kristo Yesu yaani tumeusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake mbaya.
Siku ukielewa vizuri ulichoandika utakuwa HURU kwelikweli!
 
Ni kweli Yesu alisema mkinipenda mtazishika amri zangu. Sasa unavyojiuliza ‘I don’t know how to love,’ fahamu kwamba kumpenda Yesu si jambo la hisia pekee, bali ni kumwamini na kumkubali katika maisha yako. Upendo kwa Yesu unamaanisha imani ya kweli kwake, na imani hiyo ndiyo inayozaa nguvu ya kuacha dhambi zile zilizo katwazwa na sheria.

Unaposema moyoni unampenda Yesu kwa sababu ni Mkombozi wako, hiyo ni hatua nzuri sana. Lakini shida ni kwamba unajikuta bado unasumbuliwa na uasherati. Hapa ujue huendi kinyume na maneno ya Yesu, bali unaonyesha kwamba bado unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu. Kwa sababu kwa nguvu zako binafsi huwezi kuacha, lakini ukimruhusu Yesu akuongoze, anakupa nguvu ya kushinda.

Mfano mdogo: mtoto mdogo anapompenda mzazi wake, si lazima akazunguke kila siku akisema ‘nakupenda.’ Badala yake, upendo wake unaonekana kwa vitendo kusikiliza na kufanya anachoambiwa. Lakini mtoto huyo hawezi kufanikiwa peke yake, mzazi wake humsaidia, humwelekeza na hata kumsamehe anapokosea. Ndivyo ilivyo kwa Yesu: upendo wetu kwake siyo maneno tu, bali ni imani inayojitokeza katika matendo mapya na matendo hayo hutokea kwa msaada wake.

Kwa hiyo, usiogope wala kujiita hujui kumpenda. Ukimpenda Yesu kwa moyo wa dhati, amri zake unajikuta unazifuata kwa hiari, si kwa kulazimishwa. Hata hilo tatizo la uasherati, kadri unavyomkaribia Yesu, ndivyo unavyozidi kupata nguvu ya kuachana nalo. Sio mara moja, bali hatua kwa hatua. Upendo wa kweli kwa Yesu unabadilisha tabia yako, hadi unajikuta unaacha yale uliyoshindwa kuyaacha kwa nguvu zako.
Unaweza kufikia hatua mbaya ya uasherati mpaka unaogopa kwenda kanisani? That's who I am, najitahidi Kwa kadiri ninavyoweza kupoteza kumbukumbu za wanawake niliowahi kusex nao lakini inashindikana.

Nimejaribu kupunguza cycle ya wanawake, nimeweza lakini ni Kwa kutokuongeza ila cycle niliyotengeneza kabla, siyo ya mahusiano ya kudumu ni cycle sijui niseme ni urafiki au nini lakini tunaweza kusex mda wowote atakao hitaji au Mimi, ni zaidi ya wanawake watano ambao nimeshindwa kumudu kuwahandle kwasababu ya tabia niliyowazoesha.

Ni changamoto sana.
 
Ukimpenda Yesu inawezekana ndani ya siku moja tu. Usifuate sheria mpende Yesu. Ndani ya Yesu kuna utimilifu wa hizo sheria zote.
 
Back
Top Bottom