DOKEZO Tunaomba Msaada: Tumedhulumiwa na LE MARAHEB RESTAURANT & more mishahara yetu na kubambikiwa kesi ya jinai na mwajiri wetu mwarabu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Watanzania wanaonewa sio Kwa sababu waajiri ni waonevu Bali ni kwasababu wao ndio wanaruhusu kuonewa
 
Huu uonevu

Ungewalipua huo mgahawa kwa kuitaja jina tu

Hivi humu jf si kuna mawakili,kwanini wasiangalie namna ya kuwasaidia hawa au mawakili humu ni watu wa dili

Ova
 
Poleni mkuu. Haya mambo kuna kaandiko langu niliongelea umuhimu wa mikataba. Haka hapa 👇🏻👇🏻

Thread 'Umuhimu wa Mikataba na faida za kusimamia mikataba katika utendaji nchini' SoC 2022 - Umuhimu wa Mikataba na faida za kusimamia mikataba katika utendaji nchini



Mkuu kwa ushauri nyie kwa pamoja nendeni kwenye vyombo vya kisheria. Maana hwa matajiri wananyanyasa saana watu hususani ukiwa huna mktaba na wanafanya hivyo kuwanyima mikataba wafanyakazi.ili waweze kuwafukuza au kuwaondoa kwa urahisi hili jambo liangaliwe kwa upana zaidi kwa faida ya pande zote.
 
Okay Jina La Mgahawa ni “Le Maraheb Restaurant & More” upo Masaki/ Chole Road.

Nimeambatanisha Picha za Mgahawa hapo Chini👇🏽

Tukio Lilitokea January Mwishoni, Osterbay Police Askari wengi wanajua Mkasa wetu, pale Osterbay Police ukisema tu kesi ya wale Vijana 12 walionyimwa Mishahara yao na Bosi wao Mwarabu mwenye Mgahawa Masaki Chole Wanakumbuka!
 

Attachments

  • F015870E-19B4-4DF3-A679-958435E9E6A3.jpeg
    39.9 KB · Views: 4
  • FDF9484B-4FCA-4E8D-AF01-7FA564E6A30E.jpeg
    63.4 KB · Views: 4
Wewe Taja mgahawa Acha uoga.

Unakumbuka kuna demu mnaigeria alisema amebakwa Zanzibar? Hotel ghafla Tu ikashuka ratings kutokana na kelele za watu.

Hichi ndo kinatakiwa kufanyika hapo. Taja mgahawa Sisi twende nao sambamba au ndo ule Le Maraheb?
Ndio huohuo Mkuu nimeambatanisha na Picha za Mgahawa. Waliofanya Kazi Pale ndo Watakua Mashahidi Siku wakiwa Exposed kwenye Media. Wengi wamedhulumiwa hadi Wapishi wa Kibongo. Kutwa watu wanaacha kazi Pale
 
Kwanza pole Sana,haya ndio maisha ya watz kwasasa mwenye pesa ndio Kila kitu,sasa unganisheni nguvu zenu wote 12,shirikisha wanasiasa sasa kwa mkuu wa wilaya,kwa das,kwa RC,barua wizarani Kama zote,yupo tuu ataogopa kumwagiwa ugari wake atasimama na nyinyi mtapata tuu,naongea kwa ushaidi niliwahi kufanya kazi kampuni flani tunakatwa nssf wakti huo kwenye mfuko hakuna kitu inawekwa,tukienda kuliza nssf danadana Kama zote,tulikaa chini tukawaza tukaja na andiko Kali Sana,nakala kwa Kama zote mbona jaamaa aliona kuwapoza wote hawa Bora watupe ela yetuu.utakuja kunishukiru kiongozi.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Aiseeee Mimi huwa sivumiliagi huo Ujinga, Kuna NGO iliwahi kuwa kubwa sana sana Tanza-nia, nilichowafanya.......basi niishie hapa.
Hahahahaha!! Kumbe wewe ndo uliwapasua wale jamaa? Yule aliekua CoP hadi leo anazurura, hana pa kupata kazi sema wakubwa wenzie wizarani wanamtupia vi consultancy vya hapa na pale ndo anaishi.
 
Askari magereza wa kike alisoma hati ya mashtaka mbele ya mheshimiwa hakimu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…