Nimeuliza mwenye Masters ya education atafanya nini Cha ajabu sana compared to mwenye degree ya education?
Unamanisha nini unaposema atafanya nini Mkuu wangu?
Unataka kusema kuwa Competence ya mtu mwenye Masters inaweza kuwa sawa na mtu mwenye Bachelor?
Kama mtu mwenye Masters kwa Bongo hana utofauti na mwenye Bachelor kwenye field ya Education basi tufanye mapitio upya ya structure yetu ya Elimu kwa Bongo.
Mie kwa ufahamu wangu, mtu mwenye Masters yoyote hawezi kuwa sawa na mtu mwenye Bachelor kwenye field yoyote.
Kadri unavyosoma ndivyo unavyoongeza ubora wako ktk eneo hilo. Ubora katika nyanja karibia zote. Iwe critical thinking, writing skills, communication skills, analytical skills, leadership skills nk.
Mie sijasoma Education wala sijasoma Masters Bongo. Ila sitaki kuamini kuwa Masters ya Education kwa Bongo haimfanyi mtu kuwa na impacts kwenye career yake. Sitaki kuamini hilo. Labda iwe Masters za mchongo mnazosema watu wanaandikiwa mpaka Thesis na wanatoa rushwa ili wamalize shule.
Ila kama kasoma mwenyewe na akafaulu kabisa. Hawezi kubakia kama alivyokuwa wakati akiwa na Bachelor. Hata kwenye ufundishaji wake ( endapo ataendelea kufundisha huko Secondary) ni lazima uwe wa tofauti. Usipokuwa wa tofauti basi alipata Masters ya Mchongo.
Ni hayo tu mkuu.