Kama unachosema ni kweli, basi tupitie upya mfumo wa Elimu ya Bongo..
Na kwanini mwenye Bachelor awe na uwezo mkubwa kuliko mwenye Masters? Kwani kabla, si hata mwenye Masters alianza kuwa na Bachelor kwanza? Kwahiyo unataka kusema mfumo wa Elimu Bongo unamfanya mtu awe incompetent kadri anavyosoma zaidi, si ndio?
Mie sijasoma Masters Bongo, ila Bachelor nilisoma Bongo. Kwahiyo sifahamu kwa undani zaidi kinachofundishwa kwenye Masters kwa Bongo. Nikijilinganisha sasa na nilivyokuwa na Bachelor najiona tofauti. Tofauti kwenye ku-argue, writing skills, communication skills, analytical skills, critical thinking, time management pamoja na soft skills nyingine nyingi tu.
Zaidi ya yote, kwenye career yangu, kwenye Mastes nimejifunza vitu vingi sana ambavyo sikuwahi kuvijua wakati nina Bachelor. Naweza kusema, utendaji wangu wa kazi kwa sasa hauwezi kulingana na ule wa kipindi kile nina Bachelor.