Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 253
- 360
Bajeti ya mwaka 2021/2022 iliyopitishwa na Bunge ukiondoa masuala ya kulipa deni la taifa na matumizi ya serikali ikiwemo kulipa mishahara ya Watumishi, kiasi cha Shilingi Trillion 4 zilitengwa kwaajili ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa na vituo vya afya.
Baadaye tukapata msaada wa Shilingi Trilioni 1.3 kwaajili ya kupambana na Uviko 19 ambazo Rais Samia akazielekeza kwenye ujenzi wa madarasa pamoja na vituo vya afya tu. Hizi pesa ziliwekewa msisitizo kwamba ole wake atakayezifyonza atakiona cha moto, msisitizo ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba mpaka usimamizi wa zile 4Trilioni za kwetu haukusikika tena.
Likaja suala la Tozo za miamala ya simu, tozo hizi zikiwa na lengo la kuelekezwa kwenye ujenzi wa madarasa kwa mara nyingine tena na licha ya wananchi kulia kwa machozi ya damu lakini bado kauli ilitolewa kwamba asiyetaka kulipa tozo 'ahamie Burundi.' Ripoti ya mwezi wa kwanza wa makusanyo ya tozo ilikuwa ni Sh48.5 bilioni.
Swali ni moja tu kwa waziri; Je, Sh. 4 Trilioni, Sh. 1.3Trilioni na mfululizo wa makusanyo ya tozo za miamala ambazo kwa wastani wa tathimini ya makusanyo ya mwezi mmoja ni zaidi ya Sh. 40 bilioni. Hizi zote zimefanya nini?