Tunaomba Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu afafanue hizi pesa zimefanya nini?

Mada mfano wa hii lazima ipotee kwa sababu haina wachangiaji na hata kama tupo we haven't to share sababu akili zimefungwa.

Nchi yetu imekosa mijadara ya kitaifa bali wengi wa wenye upeo wameishia kubeba filimbi vifuani kwa kukosa pumzi za kupulizia.

Makusanyo toka kwa raia yameongezeka nje ya kodi na serikali ikiojiwa, kiongozi mkubwa anajibu kwa nyodo hama nchi, ahahahaaa...
 
Wakati huo Nape yupo hewani kuzurula nchi nzima kwa chopa eti kukagua na kuhamasisha anwani za makazi, mradi ambao hauna bajeti watu wanachangishwa.!

Kweli kabisa, Serikali inayo matumizi ya anasa....

Badala Serikali kubana matumizi, Serikali inakamua wananchi...mara Tozo, mara Kodi, mara Mafuta...

Kila Lita Moja ya mafuta, Serikali unachukua Shs 800 .

Kwa Nini Serikali isitoe hapo Shs 200 tu Kwa Lita?

Halafu ikapunguza Posho za maafisa ngazi za juu, na V8 kupumzika kuzunguka.

Mfano, badala ya kwenda airport, au safari fupi Kwa V8, unaenda na rav 4
 

800.!!! Una uhakika mkuu ni 800? Mbona ni kubwa sana kuliko hata faida ya mwenye mtaji kwa lita!!
 
Misukule ya dikteta tulieni, hayo maswali kaiulizeni mizimu ya Chatttle,

Kutwa mnamtukana Samia,Mara kwann kachukua hela za Covid19, nyie hamna haki ya kuhoji kabisa, wehu nyie
Badala ya kujibu hoja, unaleta makasiriko unadhani hiyo itasaidia nini? Ukweli utabaki ukweli na blah blah zitabaki kuwa uzushi. Jibu hoja iliyopo mezani acha kurukaruka!
 
mkuu ccm ni mchwa huwa hawashibi, hawa ni majizi wote. ukiona manyoya ujue kaliwa maana swali lako ndo jibu lako over.
 
Jamani Kodi ya kwenye mafuta ni kubwa Sana Tsh 800, kwa Nini isiwe Tsh 200, hata kwenye TOZO hivyo hivyo Voda Kodi na faida Tsh 600 lakini TOZO Tsh 1,000. Mtatua Wananchi, na wakati michanga ya dhahabu inaondoka BURE kwa malipo kiduchu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…