Tunaomjua Mwamba wa Lusaka (Chama) na makubwa aliyoyafanya katika ligi hii lazima tutafakari tuhuma alizopewa kuwa ni mtovu wa nidhamu

Tunaomjua Mwamba wa Lusaka (Chama) na makubwa aliyoyafanya katika ligi hii lazima tutafakari tuhuma alizopewa kuwa ni mtovu wa nidhamu

Mashabiki huwa mnaanzishaga sintofahamu sana kwenye club yetu ya simba muwa mnafanya kwa kiasi, mambo ya kuhisi au kuvuruga club haipendezi
 
ALIDENGUA AU ALIKUA ANAHOJI MASLAHI YA MKATABA??

KWA NINI HAMPENDI MCHEZAJI KUOMBA KUONGEZEWA MASLAHI YA MKATABA??

HIYO IPO PANDE ZOTE MBILI IWE YANGA AMA SIMBA UKIGUSA MASUALA YA MKATABA LAZIMA UAMBIWE MTOVU WA NIDHAMU.
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko team, Chama anao wafuasi wengi kwa mambo aliyoyafanya Simba lakini simuoni Benchikha akiingia katika mfumo wa Chama, kocha ni mkubwa sana kuliko mchezaji na anaungwa mkono na Mo Dewji anayemlipa mshahara na kumpa mamlaka ya kufanya analotaka kwa faida ya timu.
 
Unataka ufahamu ili iweje? Sio kila jambo linaenda public,

Umepewa taarifa hata kama hutamuona uwanjani ujue ana changamoto.

Sababu nyingine unaweza kuweka wazi zikawa na madhara zaidi ya tatizo lilipo alafu mkarudi tena hapa kulaumu.

Simba kuna watu wazima punguzeni chokochoko.
UNAKUMBUKA NELSON OKWA ALISHAWI KUSEMA VIONGOZI WANAPANGA VIKOSI KUWEKA WACHEZAJI WANAOWATAKA WAO??

MBONA HAMTAKI KUKUBALI KUWA VIONGOZI WA TIMU ZA KARIAKOO WANAUDHAIFU.
 
Wekeni sababu za kubuni hata laki moja lkn uongozi wa simba hauwezi kuhangaika na nyinyi sana sana ni kupoteza mda tu.
 
Pale mchezaji anapokuwa mkubwa kuliko club, kazi kwenu mlitusakama sana kwa swala la Fei baada ya kusema ili yy arudi basi Rais aondoke, haya kazi kweni na ana miaka miwili hapo kasaini juzi tu hapo.
 
Baada ya kushinda dhidi ya wydad mashabiki wa simba mmeanza kumkataa chama.
Wakati nyie mashabiki kipindi chama akiwekwa benchi mlikuwa mnatukana vibaya sana.kweli nyie ni Mbumbumbu,onana ni upepo tu mechi ya KMC mtamkataa na kuanza kumlaumu mangungu
 
Pale mchezaji anapokuwa mkubwa kuliko club, kazi kwenu mlitusakama sana kwa swala la Fei baada ya kusema ili yy arudi basi Rais aondoke, haya kazi kweni na ana miaka miwili hapo kasaini juzi tu hapo.
Ni wakati sasa kwa mashabiki kuhoji huo utovu wa nidhamu wa Clotus Chama na huyo mwenzake, ni utovu gani huo wa nidhamu!!

Kama walitoroka kambini, waseme! Na kama walidai posho walizoahidiwa; waambiwe pia. Ujanja ujanja hautakiwi.
 
Timu za kariakoo (Simba sc na Yanga Sc) Hawa mapacha huwa wanakasumba sana haswa Hawa viongozi wanapoulizwa kuhusu suala la masilahi.

Nimemshuhudia Chama (kipenzi Cha mashabiki) akicheza mpira katika ligi yetu hii kwa nidhamu kubwa kwa misimu kadhaa bila kusikia kakwaruzana na mchezaji mwenzie au kiongozi mwenzake je leo hii Kuna Nini kwa Chama?

Tulizoea kusikia Mkude kafanya hivi au Benard Morson kafanya kile hapo nzungumzia wakiwa Simba sc acha Yanga Sc kwa Bernard morsoni watu Kama Hawa mwisho wa siku mashabiki tulizoea kutokana na utundu wao.

Aliachwa Saidoo ntibazonkiza pale Yanga Sc juu juu tu hakuna sababu ya maana iliyoelezwa, hii ni kasumba kwa timu yetu/timu zetu za Kariakoo na hii hutokana na viongozi kutoa ahadi zisizo na vitendo na wachezaji wakihoji wanaonekana ni watovu wa Nidhamu.

Maoni Yangu: ifike hatua timu za kariakoo ziache janja janja haswa kwenye masilahi/posho za wachezaji.

Hakuna shabiki wa Simba sc na Yanga Sc asiyejua kuwa Chama kwenye Suala la nidhamu yupo vizuri Ila janja janja za viongozi wa kariakoo huwa zinatengeneza hadithi za kumtoa mtu kwenye Reli.

Nawasilisha hoja.
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu anayoitumikia.
 
Labda ugomvi wa kugombania kile kitu cha Katikati pamoja na mabosi wake.
Halafu wamiliki wa hicho kitu wakishamkamata mchezaji wanaemtaka lazima Kiwango kiporomoke.
Dar ni jiji maarufu kwa starehe .
 
Ni wakati sasa kwa mashabiki kuhoji huo utovu wa nidhamu wa Clotus Chama na huyo mwenzake, ni utovu gani huo wa nidhamu!!

Kama walitoroka kambini, waseme! Na kama walidai posho walizoahidiwa; waambiwe pia. Ujanja ujanja hautakiwi.
Kweli kabisa Mkuu.
 
Mipira ya kiafrika shida sana unaambiwa utovu wa nidhamu halafu huelezwi alichofanya mnabaki mitandaoni mnalumbana bila kujua chochote.
Kwani mkuu wewe unajua kilichofanya Jadon Sancho asimamishwe mpaka leo au walieleza zaidi ya Ten Hag kusema Sancho anajua cha kufanya ili arudi kwenye team?

Kwahiyo usibeze u - Africa sana.
 
Unahoji kuhusu malipo yako,unaambiwa mtovu wa nidhamu,awaburuze FIFA,waache ujanjaujanja.
 
Hoja yako umeielezea upande mmoja tu wa Chama.

Chama kila kipindi cha usajili huwa anakuja na drama zake.

Nitajie mwaka gani ambao msimu wa usajili umefika hujasikia longolongo za Chama

Akifakisha achukuliwe hatua na hiyo ndio inapaswa kuwa nidhamu endelevu, wachezaji wajue kuheshimu mamlaka.

Sisi mashabiki na sisi tutambue kuwa wachezaji wetu tunaowapenda tuna fursa ya muda mdogo sana ya kumuona mchezaji.

Katika huo muda ni awapo kiwanjani tu, na akiwa hapo hutamuona akiongea.

Maana yake kuna mengi yanayofanyika akiwa eneo ambalo sisi mashabiki hatupo.

Eneo hilo ndio sehemu anayopata fursa ya kuongea na kufanya mambo mengi ambayo mengine pengine hata sisi mashabiki tungepata fursa ya kuyaona kama si kupunguza mahaba yetu basi tungeweza kumchukia mazima.

Sasa kama huko ndio anafanya mambo yanayokiuka sheria, sisi mashabiki hatuwezi kuwa na guts za kuwalaumu viongozi kwa adhabu watayotoa kisa tu ni mchezaji kipenzi.
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu, Morison alikuwa akisajiliwa msimu mzima anacheza mechi haizidi 6 ,zote anacheza hovyo, ikifika mda wa kusajili anaanza kuonyesha kiwango, huyu chama aliyecheza hizi mechi za mwisho kimataifa utadhani siyo kama yule wa kwenye ligi, hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu na asizingue akitaka kwenda upande wa pili au popote aende

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu za kariakoo (Simba sc na Yanga Sc) Hawa mapacha huwa wanakasumba sana haswa Hawa viongozi wanapoulizwa kuhusu suala la masilahi.

Nimemshuhudia Chama (kipenzi Cha mashabiki) akicheza mpira katika ligi yetu hii kwa nidhamu kubwa kwa misimu kadhaa bila kusikia kakwaruzana na mchezaji mwenzie au kiongozi mwenzake je leo hii Kuna Nini kwa Chama?

Tulizoea kusikia Mkude kafanya hivi au Benard Morson kafanya kile hapo nzungumzia wakiwa Simba sc acha Yanga Sc kwa Bernard morsoni watu Kama Hawa mwisho wa siku mashabiki tulizoea kutokana na utundu wao.

Aliachwa Saidoo ntibazonkiza pale Yanga Sc juu juu tu hakuna sababu ya maana iliyoelezwa, hii ni kasumba kwa timu yetu/timu zetu za Kariakoo na hii hutokana na viongozi kutoa ahadi zisizo na vitendo na wachezaji wakihoji wanaonekana ni watovu wa Nidhamu.

Maoni Yangu: ifike hatua timu za kariakoo ziache janja janja haswa kwenye masilahi/posho za wachezaji.

Hakuna shabiki wa Simba sc na Yanga Sc asiyejua kuwa Chama kwenye Suala la nidhamu yupo vizuri Ila janja janja za viongozi wa kariakoo huwa zinatengeneza hadithi za kumtoa mtu kwenye Reli.

Nawasilisha hoja.
kipindi cha pre season edo alitabiri haya,alisumbua kwenda na timu uturuki mpk alipwe chake edo alisema aombe awe form ila akicheza chini ya kiwango atajuta jinsi viongoi watakavyomfanya sasa anatafutiwa zengwe la kuachwa usishangae hata hili dirisha dogo wakampa thank you...

watu pekee watakaomsaidia ni viongozi wa yanga km wakionesha kumtaka ndo simba wanaweza kufikiria mara mbili kumuacha...wakifikiria zile 5 halafu game ya pili wanakuta na mziki huu
6:aucho
7:chama
8😛acome
9sankara
10:ki
11:max
mbona itfungwa goli mpk pomoni...
 
Back
Top Bottom