Habari za weekend wakuu
Changamoto yangu haswa kubwa ni hii
Mimi ni binti wa kwanza kwa mama yangu tumezaliwa wawili, tumelelewa single parent Ila kwenye extended family.
Tatizo linakuja mma yangu mzazi kabisa kanilea kanisomesha hadi nimemaliza form 4, (primary kayumba secondary za momy am going).
Kuingia chuo hapo kati nikaanza vibiashara vidogo dogo pia nilikua na boyfriend (x bf) alikua akinisaidia sana kwenye mambo mengi haswa elimu, miaka yote mitatu ya chuo kuhusu kula, mavazi na malazi ilikua juu yangu sio mama wala familia yangu sikua tegemezi na hadi sasa.
Bado sijabahitika kupata kazi ila najimudu maana kuna vibiashara vinanikeep busy kidogo na kunisaidia vitu vya hapa na pale.
Hiyo ni habari yangu kwa ufupi, changamoto inakuja mama yangu hajawahi kunipa baraka yoyote ile hata kusema Mungu akusaidie mwanangu, cha zaidi yeye ni kuniomba hela tu na nikisema sina ni kosa nitasemwa hapo hadi kutolewa radhi!!! Muda mwingine namwambia mm bado sijapata ajira na sijakaa sawa kimtaji hiki kidogo wacha nikizungushe wee ni balaa nitasemwa hapo wiki nzima hadi nitampa.
Muda kidogo, alinambia kuna viwanja vinauzwa nitume hela anunue nikatuma, Leo hii nikiuliza naambiwa nenda Ili hali sijui hata ni wapi ila alisema ni bagamoyo, bado vicoba nishatuma hela sana na bado za miradi hewa hapo kati remind you muda huo bado niko chuo.
Nikitaka kufanya kitu nikimshirikisha ataomba hela nampa nikimdai naambiwa sitafanikiwa na nitadhulumiwa[emoji17]
Kuna siku nilimwambia kiutani tu kua nashukuru Mungu nimemaliza kadiploma salama sasa nitafute hela ya kwenda degree nilichojibiwa ni kua ungeendaje hiyo dip bila cheti cha form4 na ambayo nimekusomesha mm, jamani hata kunisapoti ya kinafki tu hapo chuo nimejisomesha mwenyewe sijui stationary kuumwa mitihani ada, kodi, nauli maana nimesoma mkoani
Nimefupisha mambo ni mengi sana, Mimi hadi sipendi kuishi nyumbani nakaaga mkoa mwingine kabisa kuepusha makelele ila bado nikiwa na huko nitaombwa hela ya marejesho na hazirudi!!!
Hapa juzi kati nilimtumia mzigo nikamwambia uza hela utakayoipata ni ya kwako huo mzigo faida yake ni laki5 Alhamdulillah aliuza, kuna kitambaa cha kushona nilimuomba mita moja na robo tu akanijibu sitaki we si mchoyo (kisa aliniomba hela ya marejesho nikamwambia sina watu bado hawajanilipa ngoja sikukuu ipite) nikamwambia mm mchoyo kisa nimekuambia sina? Sinimekutumia vitu na nimekupa hela ubaki nayo, akanijibu sikukuomba[emoji17]
Hivi ni mm tu au kuna wezangu tunapitia changamoto hii tupeane ushauri maana nikimfikiria sipati jibu neno asante kwake sijawahi kulisikia wala Mungu akubariki Mwanangu sijawahi
Kuna siku nipo chuo kipindi cha final akaniomba laki6 nikamwambia sina ila nitakupa laki3, kesho naanza final nikitoka jioni nitakutumia, nilikua na mitihani miwili wa saa2 na saa6, nilipigiwa simu balaa na bahati mbaya sikuweka silence ikabidi niitwe kuzima simu nikaizima remind you hata kuambiwa mtihani mwema sikuambiwa!!! Nilivyotoka nawasha simu tu nakutana na msg zake za lawama nimemzimia simu sitaki kumpa hiyo hela ningemwambia mapema wakati nilimwambia nitakutumia jioni maana aliniomba usiku na kwa wakala ni mbali nikasema nikimaliza paper najua itakua kwenye mida ya saa10 nitamtumia tu, ikawa kesi
Hivi Leo tu kuna kesi, kwangu kupewa radhi imekua kitu cha kawaida maana nishaambiwa maneno mengi mabaya,
Nimetype kwa uchungu sana ee Mungu anione jamani kwann napitia mitihani hii
Samahanini kwa mwandiko mbovu na essay ndefu (hapo sijaweka vitu vingi sana)
Maoni yako ni muhimu, nifanyaje au ww uliyepitia kama yangu haya ulifanyaje?
Kuna muda nilifikiria kuolewa ila sitaki kukurupuka