Tunaotegemea kugombea ubunge 2025 njooni tuweke mikakati yetu hapa binafsi nagombea jimbo la Mbozi

Tunaotegemea kugombea ubunge 2025 njooni tuweke mikakati yetu hapa binafsi nagombea jimbo la Mbozi

Najua katika jukwaa hili wapo watanzania wenzetu wanaotarajia kugombea ubunge 2025.

Kugombea nafasi yeyote sio jambo baya bali ni jambo la kimaendeleo ambalo kila mtanzania anapaswa kulifahamu.

Kila mtanzania anahaki ya kugombea nafasi ya ubunge na nafasi zingine katika taifa letu.

Hivyo watanzania wenzangu wenye nia kama hiyo msiogope.

Mkiendelea kuogopa taifa letu haliwezi kupata maendeleo mnayoyataka.

Mkiogopa mambo hayawezi kuwa vile mnavyotaka.

Mabadiliko ya kweli yanatakiwa yaanze nawewe mwenyewe.

Hivyo nimeandika mada hii nikiwa mwenye nia thabiti ya kugombea ubunge jimbo la Mbozi.

Kama Kuna wengine pia wanaogombea naomba tukae hapa tujadili mikakati, changamoto na faida mbalimbali za kugombea ubunge.

Tujadili ni jinsi gani tunaweza kupambana na changamoto hizo na kwa kutumia mikakati ipi.

Lakini tusisahu faida tutakazo zipata mara baada ya kugombea.

Lakini pia ni changamoto zipi wanazopitia wabunge huko bungeni.
Ndugu mtia nia,
nakuombea Baraka na Neema za Mungu katika haja yako ya kutaka kuwatumikia wanainchi na waTanzania kwa ujumla.

Utumishi ni wito.
Mungu akujaze na kukutia nguvu,
Kila la kheri 🐒
 
kwa mfano,
Ndugu mtia nia, Jimbo lako lina taarafa ngap?

Lakini pia lina kata ngap?

vip vijiji na vitongij viko vingap🐒

idadi ya watu je kulingana na sensa ya majuzi 🐒

vip idadi ya wapiga kura ikoje, rejea uchaguzi ulopita na zingatia maboresho ya daftari la kudumu la wapga kura wakati huu🐒

This is the homework.

Plz build the foundation for your mjengoni journey2025 on this platform 🐒
 
Ndio ni waganga njaa wa kuleta mabadiliko.

Ni waganga njaa kujinufaisha wenyewe kutokana na masurufu ya ubunge...

Kama ni mabadiliko, kila mwananchi ana nafasi na wajibu wa kuleta mabadiliko...

Hata nikikuuliza, wewe kama ukiwa mbunge ni nini utafanya tofauti na ulivyo sasa, hutakuwa na majawabu ya maana...
 
Back
Top Bottom