Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Pole sana mkuu,uko sawa na Mimi ila tujipe moyo na tupambane ipo siku yatakuwa sawa
 
Kupanga ni kuchagua mkuu, pia usikubali kufanya kitu ambacho kiko nje ya plans zako. Una plans nzuri, hakikisha unazitekeleza.

SIyo lazima sana kuwapeleka watoto English Medium, kama hicho unachokifanya kina manufaa zaidi kwao, basi shilikilia hapo hapo.

ila pambana zaidi uweze kupata hela nyingi, uwapeleke English Medium pamoja na kuwajengengea nyumba vyote kea pamoja
 
nimepata nafasi diamond na olympio, tatizo ni umbali, naishi makongo juu mkuu, gari la olympio linaishia Mlimani City, na linafika saa kumi na moja na dakika 20 so inabidi watoto waamke saa kumi na nusu kila siku then saa kumi na moja bajaj iwapeleke mlimani city kuwahi gari la shule. still naona itakuwa kuwasumbua watoto kuwaamsha saa kumi na nusu usiku kila siku. nimeona wasome tu kayumba then nitawatafutia mwalimu wa kiingereza...
 
Sababu ya kukataa school bus kuwapeleka asubuhi ilikuwa swala muda huo huo wa kuja kuwachukua, saa 11.30 asubuhi.

Uzuri shughuli zangu ni maeneo ya posta hivyo inakuwa rahisi kuwa drop saa moja na mimi kuendelea na yangu.

Jioni wanarudi na school bus mpaka kituoni ambapo ni mwendo wa dk 5 mpaka nyumbani. Naishi tabata.
 
ndo maana nimeamua wasome hapa hapa kayumba wanaamka saa kumi na mbili na nusu saa wanafanya maandalizi saa moja na nusu wapo shule
 
Mimi mwenyewe wanangu wanasoma shule za St.Kayumba.Haya Maisha haitakiwi kukomplikati sana,Wakati nasoma Chuo kikuu asilimia kubwa ya Vijana waliokuwa wanafanya Vizuri darasani na kuongoza,ni wale wa St.Kayumba.
 
kabisa mkuu, shule za EM gharama ni kubwa sana , kama uchumi umeyumba watoto ndio wanao teseka kukaa nyumbani mwezi mzima bila kwenda shule
kwa sababu ya kudaiwa school fees
 
ndo maana nimeamua wasome hapa hapa kayumba wanaamka saa kumi na mbili na nusu saa wanafanya maandalizi saa moja na nusu wapo shule
Naamini kikubwa ni ufuatiliaji.
Waweke karibu walimu wao kwa occasional vi elfu 5. Itakusaidia kujua maendeleo yao halisi.

By the way hao kina Diamond ni kayumba waliochangamka tu hakuna walichokosa.
 
Naamini kikubwa ni ufuatiliaji.
Waweke karibu walimu wao kwa occasional vi elfu 5. Itakusaidia kujua maendeleo yao halisi.

By the way hao kina Diamond ni kayumba waliochangamka tu hakuna walichokosa.
"By the way hao kina Diamond ni kayumba waliochangamka tu hakuna walichokosa." kweli? how?
 
Mkuu kwann usitafute shule ya bei rahisi hata chini ya 1m, secondary haina shida as washapata msingi mzuri chini
 
Mkuu kwann usitafute shule ya bei rahisi hata chini ya 1m, secondary haina shida as washapata msingi mzuri chini
shule ya chini ya mil moja ni worse kwa sababu inakuwa haina viwango. diamond, olympio ni laki nne kwa mwaka lakini zipo mbali sana inabidi mtoto aamke saa kumi usiku jambo ambalo si zuri, so bora asome tu ya kiswahili. anaamka saa kumi na mbili na nusu shuleni anafika saa moja na nusu
 
"By the way hao kina Diamond ni kayumba waliochangamka tu hakuna walichokosa." kweli? how?
Darasa moja watoto mia na ushee, jitihada yako mzazi kufuatilia maendeleo ya mtoto ndio ita determine ufanisi wake, japo inajinasibu kama English medium walimu English yao ya kuunga unga.

In short ni Kayumba iliyopo Upanga tu.
 
Hivi kama hamna uwezo huwa mnazaa kutafuta nini? Au ndo mnaamini kila mtoto huja na ridhiki yake?
 
Pa1 mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…