Hizi shule nyingi wanafundishwa kwa kingereza lakn watoto wengi hawajui kuongea kingereza.Katika pitapita zangu nimepitia shule hizi nyingi nikitaka kujua kama kweli watoto wanajua kiingereza hata cha kawaida tu. Nichokikuta ni kituko na ubabaishaji tu, watoto hawajui kuongea kiingereza fasaha, wanaongea kama walimu wao ambao wengi ni hawahawa ngumbaru wasiojua kikutafuna kiingereza vizuri. Walimu wao hawana misamiati ya kutosha kuweza kufundisha kiingereza fasaha. Walimu wenyewe ni form six plus diploma na wengine ni form four plus certificate ya ualimu, wapi wamejua kuongea lugha ya kiingereza? Ni ubabaishaji tu unaofanyika kwenye shule hizo za kiingereza. Wazazi wengi wenyewe tu lugha ya kiingereza hawaijui wanafikiri watoto wao wakijua kutamka dady, mom ndiyo tayari wamejua kiingereza. Wanaojua kiingereza ni wale wanachokitumia muda mwingi hata wakiwa nje ya shule
Zile shule Fee Zaid 3M kdgo watoto wanajitahidi.