Kwani barua, posa, na mahari ni vitu vitatu tofauti au [emoji848]
barua inaandikwa kuomba kumposa bint husika ambapo hutumwa mshenga huwaga aina ulazima kwenda na ndugu ila inapendeza kwenda na mtani wa hilo kabila kutia UDAMBWIUDAMBWI wa kitamaduni
barua ikikubaliwa inatwaja mahali pamoja na taratibu zingine ambazo zitahitajika kukamilisha mahali
sasa ile siku ya kwenda kulipa mahali sisi watu wa pwani tunasema TUNAENDA KUFUNGA PAVU
hapa inapendeza uende na ndugu haswa wajomba baba wadogo shangazi ama mama wadogo/wakubwa au hata kam kuna kaka au dadazako waliolewa inakuwa bomba zaidi bila kusahau mtani / mzee machachari mana kwenye kutoa mahari kunakuwa na ukauzu flani hivi ukifanya masihara mnaweza kurudi na mahali zenu
sasa hii ndio inaitwa kwenda KUMPOSA
ila inakuwa inavutia sana kwenye POSA baada mlaluano wa maneno some time mpk wengine kususa wanatoka NJE kabisa basi hufuata vicheko na misosi haswa yule alokuwa mtata ndo anakuwa poa sana mda huo hizi ndio taratibu zetu watanzania hufanya wengi ndoa zidumu na kufurahia 7bu UDUGU uanzia hapo sasa
So taratibu za mahali zikikamilika ambazo zinaaambatana na taratibu za mila na desturi za kabila husika
sasa hapo unakuwa tayari USHAMPOSA bint husika na anakuwa mchumba wako
kwa maana mshafahamiana pande zote zinatambua watu wawili ni wachumba
kuna makabila mengine zikitoka baraka za wazazi unaweza kumchukua mwanamke na mkaishi huku
mkisubiri kufunga NDOA KIKANISA/KISERIKALI
lakini kwa upande wa DINI ya kiislam kisheria hakuna POSA na wala haina UCHUMBA
sheria ya uislam ni ni mahari kisha NDOA then ndo unaruhusiwa kuchukua MKE nadhani hata UKIRSTO upo hvyo pia
So taratibu za POSA ni kimila zaidi kwa karibu 9O% ya makabira yote TANZANIA pengine hata DUNIANI labda