Tunapopoteza Matajiri 5 ndani ya wiki 1

Tunapopoteza Matajiri 5 ndani ya wiki 1

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ndani ya siku 7 vibopa hawa wa ukweli hatuko nao:

1. Hamoud Mohammed Sumry (aliyekuwa na mabasi ya Sumry)
2. Tonil Somaiya (Shivacom)
3. John Lamba (mwenye Traventine Hotel Dar es Salaam)
4. Mathias Manga (mwenye Gold Crest Hotel)
5. Mzee Asas (Mwenyekiti ASAS group)

Kina yakhe wangapi wameondoka kimya kimya?

Serikali iko kimya kipaumbele chake kusimamisha uchumi.

Mikusanyiko ya watu bila tahadhari iko pale pale.

Angalizo: Chanjo ya Corona si dawa ya kutibu Corona wala nyenzo pekee ya dhahabu itakayotuepusha na gonjwa hili.
 
Leo tuko pamoja mtu wangu wa nguvu.

Hapo umemsahau Keenja na mkewe. Hapo Ar Uliwa wa Matchmaker anazikwa saa hii.

Huko dsm vifo havina hesabu.

Haya tuseme hawajachanja au hizo sindano za chanjo hazichemshwi vzr.

Mungu atuokoe tu.
 
Zaburi 91
1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

2 Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.

3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.

4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,

6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,

7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.

9 Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.

10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.

11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.

15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;

16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
 
Leo tuko pamoja mtu wangu wa nguvu.

Hapo umemsahau Keenja na mkewe. Hapo Ar Uliwa wa Matchmaker anazikwa saa hii.

Huko dsm vifo havina hesabu.

Haya tuseme hawajachanja au hizo sindano za chanjo hazichemshwi vzr.

Mungu atuokoe tu.

Inasikitisha sana.

Charles Keenja na mkewe walifariki 5 Aug. Pia si matajiri vibopa kama hawa.

Consistently siku 7, leo inclusive zimezingatiwa mtu wangu.
 
Hata hivyo ukiangalia ulaya walivyoathirika na covid huwezi kufananisha na huku
Covid haina nguvu huku kwetu
Ulaya ilipurusa mpaka wakaa sawa ile ni tauni aiseh
 
Back
Top Bottom