Tunapopoteza Matajiri 5 ndani ya wiki 1

Tunapopoteza Matajiri 5 ndani ya wiki 1

bado wewe your next

IMG_20210814_225102_731.jpg
 
Sasa hao matajiri kabisa na uCEO ina maana hawajui kujikinga na Covid hadi uje kuilamu serikali? By the way, kwani matajiri wao hawafi hadi uone ajabu?
 
Mwaka huu nchi imepoteza mtu mmoja Tu wa maana naye ni JPJM aka Jiwe...!!
Watu wengi wamepotea na "taka taka" moja iliyokuwa inanuka uvundo wa ajabu.nadhani hata huko aliko uongozi wa malaika hajaupata!
 
Ndani ya siku 7 vibopa hawa wa ukweli hatuko nao:

1. Hamoud Mohammed Sumry (aliyekuwa na mabasi ya Sumry)
2. Tonil Somaiya (Shivacom)
3. John Lamba (mwenye Traventine Hotel Dar es Salaam)
4. Mathias Manga (mwenye Gold Crest Hotel)
5. Mzee Asas (Mwenyekiti ASAS group)

Kina yakhe wangapi wameondoka kimya kimya?

Serikali iko kimya kipaumbele chake kusimamisha uchumi.

Mikusanyiko ya watu bila tahadhari iko pale pale.

Angalizo: Chanjo ya Corona si dawa ya kutibu Corona wala nyenzo pekee ya dhahabu itakayotuepusha na gonjwa hili.
DAAAH

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Sasa hao matajiri kabisa na uCEO ina maana hawajui kujikinga na Covid hadi uje kuilamu serikali? By the way, kwani matajiri wao hawafi hadi uone ajabu?

Corona si ukimwi. Imeondoka na marais hata makamu wao wa nchi, wakilindwa na mabunduki hadi magari ya ku disable networks. Wenye misafara ya ulinzi na chopper juu.

Corona imeondoka na madaktari bingwa, madaktari na wauguzi?

Kumbe kwako wanaokufa au kuugua Corona ni kwa upumbavu wao?!

"By the way, kwani matajiri wao hawafi hadi uone ajabu?"

Kauli yako hii inafanana sana na wajulikanao katika jitihada za kuficha takwimu na taarifa sahihi kuuhusu ugonjwa huu.

Wewe ni mmoja wao?
 
Na Deo Haule mmiliki wa kampuni kubwa ya utalii ya Earthlife ya Arusha katutoka leo hii kwa Uviko 19.
Tahadhari ni lazima ,dude linaua hili.
 
Back
Top Bottom