Tunaposema Haki tunazungumzia haki kwa wote. Serikali nanyi mnaihitaji haki kama sio leo basi ipo siku

Tunaposema Haki tunazungumzia haki kwa wote. Serikali nanyi mnaihitaji haki kama sio leo basi ipo siku

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo Wote!

1. Sisi Watibeli tunapopigania Haki hatupiganii haki ya kundi fulani au kundi moja pekee. Tunapigania Haki kwa wote. Kwani Haki ni jambo la binadamu wote.

2. Huenda jambo hilo huweza kuchukuliwa ndivyo sivyo na baadhi ya watu kwa kuona labda tunatetea upande fulani au tuna kile kiitwacho unafiki. Jambo ambalo sio kweli.

3. Watibeli tunakubali ukweli kuwa kila mtu anastahili haki bila kujali yupo kundi gani. Bila kujali ni mwema sana au muovu sana.

4. Muovu naye huhitaji haki katika uovu wake. Alipwe kwa haki bila kuonewa. Kuwa mwema haikufanyi umuonee muovu kwa kutomlipa Haki yake inavyostahili.

5. Ingawaje wakati mwingine ni ngumu kumlipa inavyostahili mtu muovu hasa kama muuaji aliyemuua mpendwa wako. Hasira na chuki zilizopitiliza zinaweza kukufanya ukamhukumu na kumpa adhabu kupitiliza nawe ukaingia kwenye mkumbo wa waovu na wanaoonea.

6. Serikali inaombwa Haki sio kwa sababu yenyewe ndio inatoa hizo haki. Bali kwa sababu nayo inaitegemea haki hiyo kujiendesha na kutawala watu.

7. Serikali yoyote duniani haiwezi kujiendesha bila kuitegemea HAKI. Kwani serikali inahitaji haki ili kutawala watu wake na kupata maendeleo.

8. Bila Haki serikali haiwezi kuheshimiwa. Bila haki viongozi wa serikali wataonekana kama katuni, vioja na hawatapata haki ya kuheshimiwa.

9. Bila Haki watawala huishi kwa hofu na mashaka makubwa. Na gharama za ulinzi na usalama huwa ziko juu sana. Kiongozi hawezi kuwa na amani ikiwa haki haitendeki.

10. Ripoti ya CNN haikuja na jambo jipya sana. Imetoa taarifa ambazo tunazijua kwa kuziona mtandaoni na nyingine tukiwa mashuhuda.

11. Je Ripoti hiyo imezingatia Haki au kuitendea HAKI serikali ya Tanzania? Kwa upande wa wahanga ripoti hiyo inaweza kuwa imetenda haki kwa sehemu kubwa. Lakini kwa upande wa pili imesigina Haki kutoka upande unaolalamikiwa. Ambayo ni serikali.

12. Msemaji wa Serikali, amelalamikia HAKI Kutotendeka. Jambo lilelile ambalo linalomilikiwa na waandamanaji. HAKI.

13. Kikawaida HAKI hulalamikiwa na wanyonge. Mpaka serikali kufikia kulalamika kutotendewa haki hapa itakuwa imeplay part kama mnyonge au mhanga. Na haina chochote cha kufanya kwa CNN.

14. Maumivu hayohayo ya kutokuwa na chakufanya na kugeuka kulalamika ndio kilio cha waandamanaji ambao hawana nguvu yoyote, hawana silaha lakini wanahitaji Haki.

15. Haki ya Kuishi hasa kwa wanaharakati na wanasiasa ambao wamekuwa wakosoaji wakubwa wa serikali.

16. Haki ya tume huru ya uchaguzi ambayo itavipa vyama vyote usawa katika kushiriki uchaguzi.

17. Haki ya Katiba mpya ambayo kila mtu itampasa awajibike mbele ya sheria akiwemo Rais na viongozi wote.

18. Ni muhimu haki hizo zitolewe kwa Amani na mazungumzo. Kwa sababu hakuna namna yoyote ya kuzizuia kwani kadiri siku ziendavyo ndivyo degree ya kuzipigania inaongezeka.

19. Ni muhimu kwa sababu serikali nayo itanufaika na haki hizo. Kuliko kuzizuia.

20. Tunapozizuia kwa nguvu haki fulani na degree zaa kuzidai zinaongezeka tunatengeneza hatari ya siku za mbeleni serikali nayo kudai haki zake zile kubwa kubwa. Na hakuna atakayekuwa anajali.

21. Haki na ukweli kiasili inatabia ya kujilipia na inakuja na Riba. Haki inayochelewa au kucheleweshwa huja na riba maradufu. Na anayelipia riba hizo ni mdaiwa, mlalamikiwa.

22. Kama taifa tunaweza kuyaangalia haya mambo kwa jicho la kiusalama na maslahi ya taifa. Ili tusichelewe sana kwani ni hakika haki inakujaga na riba

23. Haki inatabia ya kutoa adhabu hata kwa wasiohusika lakini walinyamaza ikiwa kama sehemu ya ushiriki wao.
Kwenye HAKI kunyamazia uovu ni kushiriki uovu.

24. Hata hivyo wapo watu hutumia HAKI kama agenda ya mbele huku nyuma yao wakiwa na agenda nyingine ya kutaka utawala.

25. Sio kwamba wao ni Watenda Haki au wapenda haki. Au watetezi wa haki bali huitumia haki kama chambo cha kupata kile wanachokitaka kwa siri.

26. Watu hawa wengi wao wapo kwenye siasa. Ni watu hatari sana na wanafanan kwa ukaribu na walalamikiwa.

27. Baadhi ya watu hao tuliwaona wakiwa vyama vya upinzani. Miaka 20 wanaitukana CCM kwamba sio chama cha Haki. Wanailalamikia alafu mwisho wa siku wanahama na kujiunga na chama hichohicho.

28. Watu waongo, wanafiki, wageuza maneno ni hatari sana kwa usalama wa jamii na taifa. Leo anaongea hivi kesho anaongea vile kupinga jambo lilelile.

29. Jamii lazima ijifunze kuwa na macho ya kuangalia watafuta fursa za madaraka wenye uchu wa madaraka ambao hutumia haki kama mwavuli kupata maslahi yao.

30. Maslahi ya jamii na taifa hasa kipengele cha haki hakitokei tuu vaap! Ni suala linaloanzia ndani ya familia.

31. Mume na mke na watoto. Taasisi ya familia ndio msingi wa Haki katika jamii na taifa.

32. TaikonMaster mara kwa mara ninazungumzia kuhusu mahusiano ya kifamilia na wengi huona kama nazungumzia ishu ndogo isiyo na maana lakini wanashindwa kuelewa msingi wa maisha ya jamii na mzizi wake ni ngazi ya familia.

33. Kama Mke na mume wakiwa wapenda na watetezi wa haki. Watoto wakajifunza. Huku juu huwezi sikia wadhulumaji, wauaji, mashoga, wachawi, watekaji, mafisadi, n.k.

34. Ndio ile kauli isemayo, Mlee mtoto katika njia impasayo nayo hataiacha mpaka atakapokuwa mzee.

35. Taikon inamaanisha wanaofanya hivyo hawajalelewa vizuri? Hilo sio swali hilo ni jibu kamili.

36. Wazazi wanathamini mali kuliko kitu chochote. Baba anajenga nyumba kwa dhulma. Analisha watoto kwa pesa za dhulma.
Mfano Baba ni Fundi ujenzi, au fundi nguo anaibia wateja wake. Kila siku kesi nyumbani kwake.

37. Mwalimu hafundishi vizuri shuleni. Hafanyi wajibu wake. Anadhulumu watoto wa watu. Mwisho wa mwezi anapokea mshahara kwa kazi ambayo hakuifanya vizuri. Hiyo ni dhulma. Na lazima watoto wake nao hivyo hivyo.

38. Daktari naye hafanyi wajibu wake kazi kutanguliza pesa mbele. Niliwahi toa mfano hapahapa JF. Unabagua wenye pesa na wasio na pesa. Unapendelea wenye pesa unaacha maskini. Hiyo ni dhulma.

39. Mchungaji huna unachofundisha zaidi ya mafunzo ya tamaa tamaa. Hufundishi kweli yote. Hufundishi Haki, hufundishi upendo, unadanganya watu na mafundisho ya uongo uongo ya mbinguni wakati watu wanaishi duniani. Biblia na Quran ni vitabu vya namna ya kuishi Duniani sio namna ya kuishi au kwenda mbinguni. Hamsemi ukweli.

40. Polisi, Askari, majeshi na vyombo ya ulinzi na usalama. Badala ya kutenda wajibu wenu kulinda watu, kulinda nchi. Mnafanya nusunusu kwa maslahi yenu. Mnawajali matajiri na viongozi zaidi kuliko haki na wajibu wenu. Mnapewa mishahara mnakula na familia zenu. Hiyo ni dhulma.

41. Kunyoosheana vidole. Unanyooshea kidole wenzako sijui wanasiasa na watawala. Wewe upande wako unafanya HAKI?

Acha nikalale Mimi

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Maelezo marefu unaandika Nonsense ,Kijana jiangalie Mungu hadhiakiwi .
 
Back
Top Bottom