Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Duh, hawa jamaa wana tamaa zaidi ya fisi! Yaani bado tuna machungu ujue... ohooh 😑!
 
Hakuna mtu atakayekucheka ukikubali kuwa magufuli alikuwa sahihi kwenye utawala wake, kama mwenyewe unakili kuwa wapigaji wameanza kurudi taratibu.
 
Mleta hoja ndiye anaonyesha hawa ni wapigaji, mimi nimekubaliana naye kuwa ni wapigaji nje ya wapigaji wa sukuma gang.
Hakuna mtu atakayekucheka ukikubali kuwa magufuli alikuwa sahihi kwenye utawala wake, kama mwenyewe unakili kuwa wapigaji wameanza kurudi taratibu.
 
Hivi kwanini tusiruhusu mashirika huru ya umeme kuanzishwa ili kuondokana na tatizo la umeme nchini?
maana kiukweli TANESCO ni wamezidiwa ile mbaya.
Ukiweka mashirika huru yatakuchaji umeme kwa bei kubwa.

TANESCO isibinafsishwe
 
Sio kweli kusema hivyo hata kidogo ndugu Shellohi, Mashirika kama Tanesco, hospitali, Rialways, ni mashirika ya huduma na yanapaswa kuendeshwa na serikali hata kidogo. Nchi nyingine zimebinasfisha hivi mashirika kama haya ila uangalifu maalumu na usimamizi huhitajika toka serikalini kisera. Ila kuyaendesha Magereza, police, Zimamoto?? ni kazi ya serikali, hata hili zimamoto nchi nyingine wamebinafsisha Mifano ipo Dar es Salaam walikuwepo siku chache za nyuma hapa sijui kama wapo hadi sasa.
 
Ile model ya PUMA au Airtel na kwingineko, kwa mtazamo wangu ndio perfect model. Lazima anayeendesha awe huru kuendesha kibiashara, na awe accountable kwa wananchi kwa jinsi anavyoendesha ikiwemo kugawa gawio.
Makampuni ya umma sababu ya kuwa ya umma, kuna mentality za watu kuwa very unproductive, with notcreativity. Ila wanalipwa na kwenda kulala nyumbani kwa amani tu.
Bepari au beberu hatakubali huo ujinga. Tuamke tuanze kufanya kazi kweli kweli ili tuijenge nchi yetu. Huku kujidanganya wenyewe kwa kufanya deals na kutafuta shortcut, kutatugharimu. Tena sisi wote
 
Unabinafsisha kwa hisa yaani plc,mwenye Shea nyingi ndio muamuzi kwa hiyo serikali itakuwa muamuzi
 
Makamba na Zitto msijaribu hata kidogo kubinafsisha tanesco

na
kumbuka dunia inapokwenda inaenda wapi......lau tungebaki na ttcl yetu je izi smartphone tungekuwa nazo leo hii
 
Kwanini wabinafishe Tanesco ?

Kwanini kama wanaweza na rahisi wasifungue Tanesco zao nyingine ili zicompete na hii Tanesco ?

Kuna vitu vinaitwa Commanding Heights of the Economy..., and these should remain with the State for everyone's benefit
 
Tulia zako kidogo,hao wawekezaji wakija wanaweza kubuni njia mbadala ya kupitishia waya chini ya ardhi........ila uko baadae teknolojia inapoelekea sasaivi uko ulaya wanabuni umeme wa wireless kama ilivyo mawasiliano ya simu je hapo napo serikali lazima waje kupata ushindani,ukiangalia tulipotoka kwenye ttcl hadi kuja makampuni kama tigo,voda na halotel je ulitegemea tungefika katika hali iyo
 
Kwanini wabinafishe Tanesco ?

Kwanini kama wanaweza na rahisi wasifungue Tanesco zao nyingine ili zicompete na hii Tanesco ?

Kuna vitu vinaitwa Commanding Heights of the Economy..., and these should remain with the State for everyone's benefit
Dunia ndio inapoelekea uko,huoni ushindani uliopo kwenye mitandao ya simu,je wewe hapo ulipo unaweza kuwa na mtandao na wa Ttcl,ngoja serikali wafungue milango kwa makampuni binafsi uwone kitakachotokea kama hao Tanesco watakuwepo
 
Kuna sehemu umesema uongo, umeme wa gas sio cheapest hata kidogo kulinganisha na umeme wa maji.
Mengine unaweza kuwa sawa

..gharama za umeme kwa MLAJI zinategemea mambo mengi ikiwemo chanzo cha nishati iliyotumika kuzalisha umeme.

..Umeme wa maji pamoja na ukweli kwamba ni wa gharama nafuu " kuuzalisha " uliwahi kutuletea matatizo makubwa sana hapa nchini.

..Changamoto za umeme wa maji ndizo zilizopelekea Tz kufikiria vyanzo vingine vya kuzalisha umeme ikiwemo gesi, upepo, n.k.

..Sasa hivi kuna tatizo kubwa la MIUNDOMBINU ya kusambaza umeme. Kwa kiasi kikubwa imechakaa na inasababisha upotevu wa umeme.

..Uchakavu wa miundombinu unasababisha GHARAMA za umeme kwa mtumiaji kuwa kubwa. Sasa hiyo haijalishi umeme huo unazalishwa kutokana na maji, gesi, upepo, etc.

..Jambo lingine ni MIKATABA ya kinyonyaji ambayo serikali imeingia ktk sekta ya umeme. Mikataba hiyo nayo ina athari zake ktk gharama za umeme unaotufikia majumbani na viwandani.

..Kwa maoni yangu hoja ya gharama za umeme inapaswa kuangaliwa kwa mapana yake.
 
Sijaelewa, yaani January juzi tu kateuliwa, alafu atake au anataka TANESCO IBINAFSISHWE? πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΉπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘ΊπŸ‘Ί
 
January kabla hajafika mbali atupe mrejesho wa kiwanda Cha chai Mponde kilicho Bumbuli.
 
Hiyo ndo agenda ya waliomteua. Si wanaona wenzao wa nchi jirani? Ni bahati mbaya Jeshi halitaki kuchukuwa nchi maana utaona wote wanaficha majina ya watoto wao.
Wanataka shares TANESCO
Wanataka shares shirika la reli
Wanataka shares ATC
 


Basi uzianene ndege za ATCL kwa bei ya chuma chakafu kama ambavyo mlishawahi fanya huko nyuma kwenye mashirika yaliyokuwa ya Umma kwa mbeleko inayoitwa ubinafsishaji. Maana Watanzania wameumbiwa na Mungu mioyo ya kondoo mwaweza waswaga mtakavyo.
 
Issue ni waruhusu watu binafsi wafanye biashara ya umeme wakiwa huru kwa kuzalisha na usambazaji na waondoe monopoly ya TANESCO, hiyo TANESCO kaeni nayo tuu hakuna mtu anaitaka
 
Issue ni waruhusu watu binafsi wafanye biashara ya umeme wakiwa huru kwa kuzalisha na usambazaji na waondoe monopoly ya TANESCO, hiyo TANESCO kaeni nayo tuu hakuna mtu anaitaka

Hata jeshi wakitaka wanaweza kubinafsisha. USA kule Iraq na Afghanistan walikuwa na majeshi ya watu binafsi miongoni mwa wamiliki wa hao makandarasi ni maafisa wastaafu wa jeshi lao, wakipewa kandarasi mbalimbali za uwanja wa mapambano ya vita na ulinzi wa watu muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…