Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Rugemalira si yupo?
 
Tatizo la Tanesco ni kuwa linaendeshwa kisiasa zaidi. Fikiria gharama za kuunganisha umeme za Tzs 27,000 kwenye kibanda chenye kuwasha bulb moja au mbili. Hizo gharama zitarudi baada ya karne ngapi?
 
Tatizo ni monopoly ya TANESCO hawana mshindani na uwajibikaji zero wanaishi na kuiba kwa ruzuku za serikali, waruhusu sekta binafsi zifanye biashara ya umeme sio uzalishe na uwauzie TANESCO kwa bei wanayotaka wao, turuhusu uzalishaji na usambazaji kwa sekta binafsi na serikali kama inatka kusaidia iwape ruzuku wananchi wanaotumia huduma
 
Hivi kwanini tusiruhusu mashirika huru ya umeme kuanzishwa ili kuondokana na tatizo la umeme nchini?
maana kiukweli TANESCO ni wamezidiwa ile mbaya.
Mkuu Tanesco haijazidiwa, ila Serikali ndo wamezidiwa,tena uhai wa kama aslimia 10 wa tanesco nimeona ndani ya 5yrs.
Ukiwa nashida walikuwa wanawahi sana lakini hili shirika utapeli wa wafanyakazi na rushwa,maana ukifuata utaratibu kujakupata umeme urasota sana. Serikali waje na mpango kabambe wakuliwezesha shirika,
Kumbuka tanesco wanatoa huduma na siyo beneficially oriented,ndo maana linapewa ruzuku na serikali.
 
Serikali kwendelea kuhodhi shirika hili ni kupoteza mapato na kushindwa kufika malengo yetu kama Nchi!!..unajua Shirika hili Lina madeni yasiyoweza kulipika?!!..Hebu Angali vyanzo vyetu vya umeme lakini bado tunanunua Kwa watu binafsi!!..
Vyanzo ni srikali anawajibika siyo shirika,ndo maana wanajenga vyanzo.
 
kmbwembwe TANESCO lazima ibinafsishwe ili kuongeza ufanisi na sio lazima gharama za umeme zipande sababu ya ubinafsishwaji.

Hivi sasa Tanesco inapoteza mapato mengi sana kwa sababu kadha wa kadha ambazo zinazuilika na ufanisi wake ni almost sifuri. Tanesco wanaona kawaida sababu serikali bails them out everytime, ubinafsishaji utaongeza uwajibikaji.

Aidha kuna magereza ya biashara tembea ujionee au jisomee online. US ina magereza kibao tu for profit.
 
Mkuu kwa katiba hii na sheria hizi tukibinafisisha sijui usimamizi utakuwa je. Maana upigaji bongo ni mwingi sana.
 
kumbuka dunia inapokwenda inaenda wapi......lau tungebaki na ttcl yetu je izi smartphone tungekuwa nazo leo hii
Wa kwetu let me tell you mitambo ya buzz na celtel(celnet) ilinunuliwa na ttcl na sera za kijinga za ubinafsishaji mitambo hiyo wakapewa mobitel na celtel.Kwa hiyo hata bila kuuza tanesco we can do it.Kinachotakiwa ni akili kubwa
 
Lakn serikali na mashirika mengine ya umma ndo wadaiwa sugu wa mabilioni ya bill za umeme. Lakini wasiwasi mkubwa ni ukiritimba wa kubinafisisha maana kuna kuwini au kuumia kwa katiba na sheria hizi zilizopo, maana watu wanamifano ya huko nyuma ndani ya tanesco.
Na viongozi wa serikali ndo wanalazimisha shirika kuingia mikataba mibovu kwa masirahi ya wanasiasa.
 

I hear your concerns.

Mashirika kama CRDB, NBC yalifufuka sababu ya ubinafsishwaji.

Serikali na hayo mashirika mengine hawalipi sababu wanaiona Tanesco kama mwenzao, washika dau hawawezi vumilia huu upuuzi kama likibinafsishwa.

Tanesco inapoteza karibu 16% ya umeme wote inaozalisha, hii haikubaliki hata kidogo ila wao wanaona kawaida. Ndo maana tunasema ubinafsishwaji utaongeza ufanisi.

Kuingia mikataba mibovu is a different story ila kwanza tukubaliane kwamba inabidi Tanesco ibinafsishwe.
 
Du. Wewe noma. Umepamtia kweli kweli huyu jamaa. Ni starter ya gari kweli kweli. Ametumwa kuanzisha.
 
hili jizi January Makamba litauza kila kitu pale huko Nishati.
 
Nchi ya watu zaidi ya millioni 60 kwa nini tuwe na shirika moja umeme huduma ambayo ni muhimu sana katika maisha na uchumi wa nchi, serikali kwa ruzuku zake na TANESCO hawana uwezo wa kuhudumia nchi nzima, tuache sekta binafsi iingie ifanye kazi ya uzalishaji na usambazaji, cha muhimu tuweke utaratibu mzuri tuu tupate umeme na wao wapate faida zao, tuache ujinga
 
Kuna nchi nyingi tu serikali zinamiliki makampuni na mashirika na yanafanya vizuri. Tanzania kubinafsisha shirika kama Tanesco siyo wazo zuri. Libaki kuwa serikalini.
 
Hii ni monopoly marketing.

Supplier anahodhi vyanzo vyote vya uzalishaji wa nishati, tukiruhusu ubinafsishaji umeme utakuwa bei juu sana.

Hakuna mbia atakayeuza umeme wa bei nafuu kuliko Tanesco.

Muhimu ni kuboresha shirika,kuziba mianya inayopwaya.
 
Pengine mwenye kufikiria kubinafsisha shirika kama Tanesco ndiye anatakiwa aache ujinga. Najua kama kawaida ya wabongo kutotafakari na kuangalia mambo kwa kina ndiyo utamaduni wetu.
 
Sasa mbona Tanesco anauziwa Umeme au mimi sielewi?...kama Tanesco anauziwa umeme alafu anauza kwetu!!!..Alafu unasema hawa watu binafsi watatuuzia bei juu!!!..Hebu tafakari kidogo nadhani hujui hata shirika letu linauziwa umeme na kutuuzia sisi
 
Hebu Fikiria kama tusinge binafsisha TBL au TCC hata hizi NBC,NMB na CRDB unadhani tungekua wapi?!!...Najua mnaogopa kupoteza ajira nyingi ambazo mlikua mnapata bila vigezo lakini tukitaka Tanesco ijiendeshe Kwa ufanisi na kupata Faida Partner ni muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…