Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Sekta binafsi imejenga na kuendesha miundo mbinu na uzalishaji wa umeme dunia nzima, kwanini unafikiri kwa TZ haiwezekani?
Kwanini wasijenge sasa ? Hizi story za kupewa Tanesco huoni zinakwenda against na unachosema
Mkuu Private Ownership ni for Profit always kwahio in the end chochote kitakachopatikana lazima gharama iongezeke ili watu wapige faida..., Ukiongelea efficiency kwamba huenda Private ndio itafanya vizuri (kama wafanyakazi ni hao hao lazima kuna njia mbadala ya kuwafanya hao watu wawe efficient)

Nakuacha na kisa kimoja kilichotokea California baada ya Kampuni ya Energy (ENRON) kuruhusiwa ku-trade umeme kama stock..., kilichotokea ni watu kuzima mitambo ya umeme kwa makusudi ili bei ipande na kushuka na wao kupiga pesa...

Sio kwamba sipendi free trade bila monopoly (actually I love it) ila wawekezaji waje wazalisha umeme wanavyopenda ila distribution ibakie Tanesco unless they can do it better, safely and efficiently..., Kuna maeneo mengi sana hayajafikiwa na umeme kwanini wasianzie huko na modal zao na uzoefu wao? Kwanini walitolee tamaa hili shirika ambalo lipo tayari? Ukizingatia baada ya Bwawa la Nyerere tutakuwa na Umeme wa Kumwaga...., why now na sio kipindi kile ambapo kina Dowans na Symbion walikuwa wanafanya yao ?
 
Siku zote penye profit ndio kazi kwa bidii inafanyika ni asili ya binadamu hiyo,hata watoto ukiwaambia wafanye kitu fulani ukaahidi zawadi good chance utapata matokeo mazuri, profit mbele tuache mambo ya bure
 
Mbona hauongelei ttcl na Tls,na viwanda vya nguo, yalibinafishishwa tulipata nini? Mpaka juzi Magufuri ndiye alikuja kufufua, private sector ni kwaajili ya faida tu sio uduma,akina Makamba kama wameshindwa kazi bora wajiuzuru tu,sio kuanza kuuza mali za Watanganyika
 
Tatizo kwa sheria za Tanzania sekta binafsi hairuhusiwi ni TANESCO tuu yenye monopoly 100%, unaweza kuzalisha umeme na kuwauzia TANESCO lakini sio wananchi na wanakupangia bei, if you are for free market..thats not free market
Wapelekee watu Solar, Huko Bush au hata mtaani uone nani atakupangia bei...., unless otherwise unataka kutumia miundombinu ya Tanesco au unataka kusambaza miundombinu yako utuletee madhara ya kutuunguza na kutuchafulia miji
 
Kumbe unaujua ukweli eeh basi tu mnajitoaga ufahamu.
 
Siku zote penye profit ndio kazi kwa bidii inafanyika ni asili ya binadamu hiyo,hata watoto ukiwaambia wafanye kitu fulani ukaahidi zawadi good chance utapata matokeo mazuri, profit mbele tuache mambo ya bure
Nikubaliane nawe tena kuhusu hiyo 'dhana ya profit'. Kwani 'profit' imezuiwa huko Tanesco?

Mkuu, usitafute majibu mepesi mepesi kwenye hoja nzito kama hizi. Piga akili zaidi ya ulivyofanya hapo.
 
Magufuli kafufua nini?!!..
 
Idea yako ya semi monopoly for serious investor wont work, na for profit hakuna ubaya na ndio kinachotakiwa haswa ili investors wawe motivated kuweka pesa zao, michezo michafu kama ENRON ipo popote pale lakini nafikiri unajua kilichowakuta baada ya hapo,monopoly ya TANESCO ndio tatizo la sekta ya umeme TZ
 
Ujiandae kununua unit 1 kwa tzs 500+
 
Kabla ya Mwinyi na hata sasa na bado tutaendelea kulipa Madeni ya Tanesco!!...
Madeni yapi? wakati mikataba ya Agreco na Simbion na lPTl,na Makampuni yaliyokuwa yanainyonya tanesco mikataba yote iliisha awamu ya 5? tanesco wamepiga kazi mpaka sasahivi wamebakiza vijiji kama 2000 kumaliza Nchi mzima,leo hii mnaanza kusema ibinafishishwe! Makamba na kizazi cha chote kilaniwe kama mpango wao utafanikiwa.
 
Hiyo Gas na Maji nikuongezee na Upepo bado huwezi kuendesha shirika
Unamaanisha nini ?

Upepo sioni impact yake wala sidhani kama tunahiitaji

Mpaka sasa Hydro Tanesco wanatoa total ya 562MW; Gesi na Diesel ni 796MW; Jumla ni kama 1,600 MW

Sasa mradi wa Nyerere ukiisha ni expected kutoa 2100MW; Sasa hapo utaona mwenyewe hata hao so called wawekezaji labda waje watusaidie kununua baadhi ya hizi MW na kuwauzia nchi jirani
 
Wazo la kubinafsisha tanesco achilia mbali ttcl ni wazo zuri sana kwa mtu anaethnk po+ . Ni vzur kwakua kwasasa hio unayosema kunatija kuendeshwa chni ya serikali ni Big NO. Hapa tuangalie tuu namna nzuri ya ubinafsishaji, mwekezaji sio lazima atoke nje, pia tuweke mfumo mzur wa kudhibiti wizi, uhujumu wa shirika na mfumo mzur utakao mpa bei nafuu ya units mwananchi.
Wewe unahofu tuu kwa mfumo wa sasa wa uwekezaji kuwa tunaweza kupigwa,, YES tunaweza kuibiwa but best b4 investing tufanye tafiti na uchunguzi kutoka nchi zlizoruhusu mashirika binafsi yalivowekeza Kwenye umeme apa mabarozi wanahusika sana kama watajitambua.
My take: tanesco ibaki mmiliki wa sources of energy na muuzaji wa energy hio kwa mainvestors ambao wao watafanya kazi kubwa upande wa distribution.
Hapa tenda itolewe na pia serikali isimamie vigezo na tija katika kuwanufaisha watumiaji wa mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…