Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Tunaposikia ya Makamba na Zitto kutaka kubinafsisha TANESCO, tukumbuke yaliyofanyika TTCL

Sekta binafsi imejenga na kuendesha miundo mbinu na uzalishaji wa umeme dunia nzima, kwanini unafikiri kwa TZ haiwezekani?
Kwanini wasijenge sasa ? Hizi story za kupewa Tanesco huoni zinakwenda against na unachosema
na serikali badala ya kutoa pesa kwa TANESCO kila siku inaweza kutoa ruzuku kwa wananchi moja kwa moja mfano hiyo 27K tunajua sio bei halisi, hapo serikali inaweza kusaidia ili mwekezaji alipwe market price...ninapoishi market ya umeme yote ni private sector 100% na sijawahi kuona umeme umekatika for the last 20 years na umeme ni bei rahisi sana
Mkuu Private Ownership ni for Profit always kwahio in the end chochote kitakachopatikana lazima gharama iongezeke ili watu wapige faida..., Ukiongelea efficiency kwamba huenda Private ndio itafanya vizuri (kama wafanyakazi ni hao hao lazima kuna njia mbadala ya kuwafanya hao watu wawe efficient)

Nakuacha na kisa kimoja kilichotokea California baada ya Kampuni ya Energy (ENRON) kuruhusiwa ku-trade umeme kama stock..., kilichotokea ni watu kuzima mitambo ya umeme kwa makusudi ili bei ipande na kushuka na wao kupiga pesa...

Sio kwamba sipendi free trade bila monopoly (actually I love it) ila wawekezaji waje wazalisha umeme wanavyopenda ila distribution ibakie Tanesco unless they can do it better, safely and efficiently..., Kuna maeneo mengi sana hayajafikiwa na umeme kwanini wasianzie huko na modal zao na uzoefu wao? Kwanini walitolee tamaa hili shirika ambalo lipo tayari? Ukizingatia baada ya Bwawa la Nyerere tutakuwa na Umeme wa Kumwaga...., why now na sio kipindi kile ambapo kina Dowans na Symbion walikuwa wanafanya yao ?
 
Wazo zuri kabisa.

Lakini nami naomba nikuulize jambo moja.

Hivi kwa nini Tanesco na mashirika mengine ya uma hayawezi kufanya kazi vizuri ili wananchi wafaidike na matokeo ya kazi zao?

Mkuu naomba ueleze hapa sababu unazozijua wewe ambazo zinafanya haya mashirika yasifanikiwe, kiasi kwamba uone kuwa ni muhimu "turuhusu mashirika huru ya umeme" (sijui una maana gani na "mashirika huru"?
Siku zote penye profit ndio kazi kwa bidii inafanyika ni asili ya binadamu hiyo,hata watoto ukiwaambia wafanye kitu fulani ukaahidi zawadi good chance utapata matokeo mazuri, profit mbele tuache mambo ya bure
 
Inaonekana unaamini serikali inaweza kufanya kazi nzuri kuliko private sekta, lakini kwa mifano halisi tumeona tayari hawana uwezo huo, TBL,NMB,Sigara,CRDB etc walishindwa kabisa na makampuni yalikuwa yanaelekea kufa,watu binafsi baada ya kuyanunua yamekuwa makampuni makubwa yanayolipa kodi kubwa na kuajiri maelfu ya watu na hata DSE yapo, mimi nasema uza Tanesco na kila kitu chao kiwe private 100% wenye ujuzi wao sio politicians wafanya kazi yao
Mbona hauongelei ttcl na Tls,na viwanda vya nguo, yalibinafishishwa tulipata nini? Mpaka juzi Magufuri ndiye alikuja kufufua, private sector ni kwaajili ya faida tu sio uduma,akina Makamba kama wameshindwa kazi bora wajiuzuru tu,sio kuanza kuuza mali za Watanganyika
 
Tatizo kwa sheria za Tanzania sekta binafsi hairuhusiwi ni TANESCO tuu yenye monopoly 100%, unaweza kuzalisha umeme na kuwauzia TANESCO lakini sio wananchi na wanakupangia bei, if you are for free market..thats not free market
Wapelekee watu Solar, Huko Bush au hata mtaani uone nani atakupangia bei...., unless otherwise unataka kutumia miundombinu ya Tanesco au unataka kusambaza miundombinu yako utuletee madhara ya kutuunguza na kutuchafulia miji
 
Wakati Magufuli anaonyesha kiburi cha madaraka kwa kuhujumu upinzani mlikuwa mnachekelea kuwa ccm imeimarika.

Leo wamebaki CCM wenyewe na hawataki kukosolewa, matokeo yake chain ya wapigaji inaanza kurudi ndio mnalialia.

Acha hao wahuni warudi kwenye ulaji, na wauze kila kitu kwa bei ya kutupa ili siku nyingine mjue balance of power maana yake ni nini.

Akina Januari na wahuni wenzenu uzeni hiyo TANESCO bei ya kutupwa ili mliokuwa mnafurahia siasa na chaguzi za kishenzi mjifunze.
Kumbe unaujua ukweli eeh basi tu mnajitoaga ufahamu.
 
Siku zote penye profit ndio kazi kwa bidii inafanyika ni asili ya binadamu hiyo,hata watoto ukiwaambia wafanye kitu fulani ukaahidi zawadi good chance utapata matokeo mazuri, profit mbele tuache mambo ya bure
Nikubaliane nawe tena kuhusu hiyo 'dhana ya profit'. Kwani 'profit' imezuiwa huko Tanesco?

Mkuu, usitafute majibu mepesi mepesi kwenye hoja nzito kama hizi. Piga akili zaidi ya ulivyofanya hapo.
 
Mbona hauongelei ttcl na Tls,na viwanda vya nguo, yalibinafishishwa tulipata nini? Mpaka juzi Magufuri ndiye alikuja kufufua, private sector ni kwaajili ya faida tu sio uduma,akina Makamba kama wameshindwa kazi bora wajiuzuru tu,sio kuanza kuuza mali za Watanganyika
Magufuli kafufua nini?!!..
 
Kwanini wasijenge sasa ? Hizi story za kupewa Tanesco huoni zinakwenda against na unachosema

Mkuu Private Ownership ni for Profit always kwahio in the end chochote kitakachopatikana lazima gharama iongezeke ili watu wapige faida..., Ukiongelea efficiency kwamba huenda Private ndio itafanya vizuri (kama wafanyakazi ni hao hao lazima kuna njia mbadala ya kuwafanya hao watu wawe efficient)

Nakuacha na kisa kimoja kilichotokea California baada ya Kampuni ya Energy (ENRON) kuruhusiwa ku-trade umeme kama stock..., kilichotokea ni watu kuzima mitambo ya umeme kwa makusudi ili bei ipande na kushuka na wao kupiga pesa...

Sio kwamba sipendi free trade bila monopoly (actually I love it) ila wawekezaji waje wazalisha umeme wanavyopenda ila distribution ibakie Tanesco unless they can do it better, safely and efficiently..., Kuna maeneo mengi sana hayajafikiwa na umeme kwanini wasianzie huko na modal zao na uzoefu wao walitolee tamaa hili shirika ambalo bado lipo ? Ukizingatia baada ya Bwawa la Nyerere tutakuwa na Umeme wa Kumwaga...., why now na sio kipindi kile ambapo kina Dowans na Symbion walikuwa wanafanya yao ?
Idea yako ya semi monopoly for serious investor wont work, na for profit hakuna ubaya na ndio kinachotakiwa haswa ili investors wawe motivated kuweka pesa zao, michezo michafu kama ENRON ipo popote pale lakini nafikiri unajua kilichowakuta baada ya hapo,monopoly ya TANESCO ndio tatizo la sekta ya umeme TZ
 
Chochote kilichobinafsishwa Kwa ufasaha kinafanya vizuri sana!!!...NBC,NMB,CRDB unajua kwanini umeme unaleta shida kila siku?.. Shirika hili la Tanesco halina mshindani ndio maana hata ufanisi ni sifuri!!!..Unajiuliza kwanini Taasisi kama hii ambayo ina vyuo vyake inashindwa kuwa na weledi kwenye kuhudumia wananchi?!!.. Tanesco lazima wabinafsishe tukitaka twende mbele lakini kama tutaendeleza huu utumbo hakika siku nchi itakua kiza yote na hakuna wakusema!!
Ujiandae kununua unit 1 kwa tzs 500+
 
Kabla ya Mwinyi na hata sasa na bado tutaendelea kulipa Madeni ya Tanesco!!...
Madeni yapi? wakati mikataba ya Agreco na Simbion na lPTl,na Makampuni yaliyokuwa yanainyonya tanesco mikataba yote iliisha awamu ya 5? tanesco wamepiga kazi mpaka sasahivi wamebakiza vijiji kama 2000 kumaliza Nchi mzima,leo hii mnaanza kusema ibinafishishwe! Makamba na kizazi cha chote kilaniwe kama mpango wao utafanikiwa.
 
Hiyo Gas na Maji nikuongezee na Upepo bado huwezi kuendesha shirika
Unamaanisha nini ?

Upepo sioni impact yake wala sidhani kama tunahiitaji

Mpaka sasa Hydro Tanesco wanatoa total ya 562MW; Gesi na Diesel ni 796MW; Jumla ni kama 1,600 MW

Sasa mradi wa Nyerere ukiisha ni expected kutoa 2100MW; Sasa hapo utaona mwenyewe hata hao so called wawekezaji labda waje watusaidie kununua baadhi ya hizi MW na kuwauzia nchi jirani
 
Kuna mashirika ya Serikali kutokana na wajibu wake ni kama idara za Serikali. Yanatakiwa yagharamikiwe na hazina kuu. Yanafanywa mashirika ili kuweza kudhibiti matumizi na kwamba iwepo tija.

Ukitaka kugeuza TANESCO liwe la kibiashara moja kwa moja kwanza utapata muwekezaji gani? Lazima awe wa nje na atakua na nguvu gani ya kisiasa nchini? Yeye atataka faida tu na umeme ndio roho ya uchumi wa nchi.

Sisi tunamlenga nani kuhusu maendeleo? Raia wa kawaida au wawekezaji kutoka nje? Lazima umeme utakua bei mbaya kwa raia wapiga kura na ndio mfarakano utaanzia hapo.

Hii mambo ya kubinafsisha sijui asili mia 20 TANESCO ni ile ile habari ya kubinafsisha TTCL. Wajanja wakawagawia wahindi hisa za TTCL kwa bei ya bure wakati Serikali ishawekeza mabilioni. Kisha wajanja kushirikiana na wahindi wakakwapua celltel kampuni ya TTCL ya simu za mikononi.

Ikawa wahindi wameshika jikoni TTCL wakikamua hela za umma kwa ruzuku za Serikali eti ni wabia wa TTCL. Magufuli akaja kuwafukuza wahindi na kuirejesha kampuni yake ya mkononi kwa kuhakikisha serikali inapewa hisa stahiki.

Sio kila anayejidai ana uthubutu ana uwezo au nia nzuri. Mashirika kama TANESCO au TTCL sio ya kuwekwa sokoni kama njuku.

Wanaoweza kuyaendesha kwa kufikia malengo yake kwa nchi kama Tanzania hakuna. Ni watanzania gani utawashawishi kuwekeza tanesco?

Hivi unaweza mshawishi mtu awekeze kwa gereza. Gereza linaweza kua mradi wa kibiashara? ..sina hakika wala sijaona. Lakini si lazima magereza yawepo? Kuna mambo lazima yawe jukumu la serikali. Ndio maana kuna kodi.

Tukikubaliana na uhuni huu wa january na zitto akijidai mpendekezaji wa hoja tunaona yale ya TTCL na ule mradi wa umeme wa makaa kule Songwe mbeya uhuni ule wa simon group kuhusu uda na kwingine.

La kufanyika ni uongozi imara wa kisiasa usiyokua na mchezo kudhibiti mashirika makubwa ya umma kuhakikisha hakuna ubadhirifu na inakwepo tija.
Wazo la kubinafsisha tanesco achilia mbali ttcl ni wazo zuri sana kwa mtu anaethnk po+ . Ni vzur kwakua kwasasa hio unayosema kunatija kuendeshwa chni ya serikali ni Big NO. Hapa tuangalie tuu namna nzuri ya ubinafsishaji, mwekezaji sio lazima atoke nje, pia tuweke mfumo mzur wa kudhibiti wizi, uhujumu wa shirika na mfumo mzur utakao mpa bei nafuu ya units mwananchi.
Wewe unahofu tuu kwa mfumo wa sasa wa uwekezaji kuwa tunaweza kupigwa,, YES tunaweza kuibiwa but best b4 investing tufanye tafiti na uchunguzi kutoka nchi zlizoruhusu mashirika binafsi yalivowekeza Kwenye umeme apa mabarozi wanahusika sana kama watajitambua.
My take: tanesco ibaki mmiliki wa sources of energy na muuzaji wa energy hio kwa mainvestors ambao wao watafanya kazi kubwa upande wa distribution.
Hapa tenda itolewe na pia serikali isimamie vigezo na tija katika kuwanufaisha watumiaji wa mwisho.
 
Back
Top Bottom