Tunapouliza Halima Mdee kafanya nini Kawe kwa Miaka yake 10 tujiulize na Sisi kwa 'Kujipendekeza' Kwetu kwa Mamlaka kama 'Wadau' kumetusaidia nini?

hivi kazi ya mbunge ni ipi jamani!!!

maana tunaombwa kura za urais na watu walioshindwa majukumu ya ubunge.
 
We hujui kuwa kuna pesa nyingi zilitengwa lakini. Halima akawa anashinda mahakani bila kuzifuatilia zisaidie watu wa kawe?

Angezifuatilia Makonda maana ni mkoa wake. Halima alikuwa anashinda mahakamani kwani yeye ni mzee wa mahakama? Jiwe alidhani akiagiza Halima abambikiwe kesi ndio watu wa kawe watashindwa kupambanua hujuma na utendaji? Ama huko Kawe kiongozi ni Halima Mdee tu, hakuna madiwani, mkuu wa wilaya, mkurugenzi nk? Siasa za kizee hazikutoi dogo.
 
Chagu, Rais hawezi kuzungumza kwa utani. Kauli ya Rais ni sheria, amri ya Rais inafuatwa na utii. Unapowaambia wananchi shauri yenu na Bwege wenu !! Kweli inaingia akilini. Unawasimanga wananchi na taa za barabarani kisa hawakuichagua Ccm ?! .

Umemsikia mwingine naye anasema askari wao akiharibu risasi 3 bila shabaha awajibishwe sembuse na risasi 16 ?!. Huu ni ulevi wa madaraka.

Chagu, majimbo mangapi yaliopiga hatua kwa sababu tu yapo Ccm ?. Mengi ya hali mbaya sana eg misungwi, solwa, kishapu nk . Wakati mwingine afadhali na yale yanayoongozwa na wapinzani.
 
Mbona unaenda mbele unarudi? Kwa hiyo unakubali hata mbunge wa upinzani anaweza kuleta maendeleo.
Ndio maana unasema majimbo kama Solwa na kishapu yapo nyuma kimaendeleo. Lakini kuhusu kauli ya maa Samia mnaitafisiri vibaya. Alichomaanisha ni kuwa haiwezekani askari apige risasi 16 alafu mtu awe hai. Hao watakuwa maaskari ambao hawana mafunzo kama wa Tanzania kwa hiyo labda ni wakora tu.
Kwa hiyo Jaduong unataka kuamini rais anaweza akazuia shule au Zahanati isijwngwe kisa tu mbunge ni wa upinzani? Acheni propaganda za kitoto.
 
Huyu anachosema ndicho anamaanisha
 
Hivi mbunge huwa ana "vote" ama huwa anakusanya kodi katika jimbo lake? Kama jibu ni hapana hili swali "Halima Mdee kafanya nn kwa miaka 10 katika Jimbo la Kawe msingi wake ni nini?
Kwahiyo HAKUNA haja ya kuwa na mbunge???
 
@Paschal mayalla
 
Duuuh! umemaliza! sijui siku hizi mzee anafikiria kwa kutumia nn? hivi ni kweli Mwaafrika akizeka na uwezo wa kufikiri unapungua!
 
Alichofanya Halima Mdee hakina tofaiti kimaendeleo ya vitu na alichofanya Mwigulu, Ndugai, Mwakyembe, Makamba, Nape, Majaliwa. Atleast Halima alionesha kwa vitendo kuyataka maendeleo halisi na kupigania haki na utawala bora. Hata hivyo wana kawe wa Mwenge, Masaki, Mikocheni O-bay hawana shida ya barabara maji wala umeme. Shida yao ni haki, uhuru, demokrasia
 
Bila unafiki kama Halima Mdee atafanikiwa kurudi basi this time ashughulikie mambo ya jimboni.

Ntangolea kwa upande ninaoishi. Tegeta Nyuki Stand, Barabara ya Nyuki kwenda Bahari Beach, Mkandarasi yupo site mwaka wa 7 sasa kwa barabara ya km 2.

Kuna migogoro mi 2 mikubwa. Tegeta Magereji na Wazo vs Wakazi wa Cha Simba. Hii migogoro kama imelala hivi na Wananchi wameendelea kujenga na kuzaliana.

Kuhusu Magereji waliambiwa wakae ila mwenye eneo alishinda kesi mahakamani. Kwa sasa mwenye eneo yupo kimya kutokana na uongozi wa Magereji kujipendekeza kwa Mkuu Mkoa Mstaafu hadi kufikia kutengeneza magari ya Jiji bure.

Ukishinda tafadhali njoo ututatulie hizi sintofahamu.

Sent from my POT-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…