Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Maisha ni safari ndefu na changamoto nyingi..!Hofu nyingi na kukata tamaa kwingi..!
Na ni jambo la kawaida kibinadamu kukumbana na nyakati ambapo imani ya maneno haitoshelezi kukabiliana na hofu za maisha.
Mara nyingi tunashindwa kumtegemea Mungu kwa sababu tunamfahamu kupitia simulizii na mahubiri tu badala ya kuwa na uhusiano wa karibu wa kibinafsi naye.
Pia, tabia yetu ya kutaka matokeo ya haraka na kutegemea akili zetu wenyewe inapotawala, tunajikuta tukizidiwa na mazingira magumu na kuanza kusahau ahadi zake.
Hata hivyo mpendwa Ili kuvuka kutoka kwenye imani ya nadharia na kuingia kwenye utegemevu halisi, ni muhimu kusoma na kutafakari Neno lake ili kujenga uhakika wa moyo, kukua kiimani na kujengeka kiroho.
Tunapaswa pia kubadilisha mfumo wetu wa sala kwa kukabidhi changamoto zetu kwake na kumtegemea yeye tuu!
kukumbuka matendo yake ya nyuma ya uaminifu, na kuchukua hatua za utii huku tukiacha matokeo mikononi mwake.
Jaribu kukumbuka alikuvusha kwenye mangapi hata uone hili hawezi kukuvusha!?
Nichukue nafasi hii toka moyoni kukuombea na kukutia moyo.. Ni kazima ukumbuke ya kwamba. hili nalo litapita.. Usiku hata uwe mrefu vipi KUTAPAMBAZUKA
Na Muumba wetu hawezi kukupa jaribu lisilo na suluhu
Jipe moyo utayashinda..❗❕ Yana mwisho vumilia...💪🏿