Hebu Tuangalie Faida Zitokanazo na Kuwa na Wavuti ya Kampuni
1. Kuwafikia watu wengi zaidi.
Kama tulivyoona, kwenye watu kumi, mmoja anatumia internet, je hutaki kuwa wa kwanza kumshawishi huyo mtu mmoja atumia biashara yako? Kwa kuwa na wavuti utawafikia sio tu wale walio karibu yako, balo pia hata watu walio maili elfu na elfu.
2. Kuvutia wateja makini
Chukulia mfano wewe una duka la nguo, wateja wengi wangependa kupata taarifa juu ya mzigo mpya, mapunguzo nk bila hata kuja dukani kwako. Kwa kuwa na wavuti, ni dhahiri utavutia sana wateja makini ambao hupenda kupata taarifa za kina kabla ya kununua bidhaa. Wavuti inakupa wasaa wa kujieleza kwa undani juu ya huduma au bidhaa zako.
3. Kujenga uhusiano wa karibu na wateja.
Je umewahi kujiuliza, ni wateja wangapi ambao huwa marafiki zako baada ya kutumia / kununua bidhaa yako? Je unatumia njia zipi kudumisha uhusiano kati ya mteja na mtoa huduma? Wanazuoni husema, biashara itakayodumu ni ile tu iliyofanikiwa kujenga uhusiano mzuri na wateja wake. Kwa kuwa na wavuti, sio tu utaweza kupata maejesho juu ya ubora wa huduma yako, bali pia utaweza kudumisha mawasiliano kati yako na mteja, kumbuka mawasiliano ndio hudumisha uhusiano.
4. Kufanya biashara moja kwa moja.
Katika dokezo lango moja kwenye Facebook, niliwahi kuandika " Goodbye IT, welcome Digital Business", wengi hawkuelewa nini nilimaanisha hadi pale nilipokuja kufafanua, na kuna waliochanganya na hii huu mfumo wa digitali. Kwenye makala hii niliposema Digital Business nilimaanisha kutumia IT kama biashara ndio tunachokiita digital business.
Ukweli ni kuwa, Watanzania wengi wamekuwa wagumu na bado hawaamini kama kuna uwezekano wa kufanya biashara moja kwa moja online. Hii inawezekana ni kutokana na kasumba yetu ya kuogopa kuanza hadi pale tunapoona mtu amefanikiwa.
Ukweli ni kwamba, tunaweza kuuza na kununua moja kwa moja online, tena ukizingatia Tanzana ni nchi yenye watumiaji wengi wa simu za mkononi ambazo pia huwawezesha watu kulipia kwa kuhamisha pesa. Hivyo kwa kutumia huduma hizi, unaweza kufanya bishara moja kwa moja. Chukulia mfano wamiliki wa migahawa, maduka ya urembo nk. Wavuti inaweza kuwasaidia watu hawa kupanua na kuboresha wigo wa huduma zao.