Tunatoka mbali na Mungu huinua

Tunatoka mbali na Mungu huinua

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Wakuu nimekuja tu hapa kutia Moyo wapambanaji wote waliokata tamaa.

Leo kwa mara ya kwanza nimeamka kutoka kwenye nyumba niliyojenga mimi.

Ni miaka 10 ya jasho na damu hatimaye jana nimehamia.

Mungu ni mwema, tuendeleze mapambano; kwa wale mliofanikiwa zaidi Mungu azidi kuwapandisha, kwa wale tunaopambania Kombe tusikate tamaa kuna siku yaja.

Kwa sasa naweza sema nami niko na maisha ya kawaida; usafiri, makazi na familia, na zaidi AFYA NJEMA
Nimetoka nyumbani kwa mara ya kwanza nikiwa na 15 yrs, hadi leo nami nimekua na kwangu

Mungu awabariki.
 
Mkuu hongera sanaa sio mchezo ukiona tuliko toka kwa kweli mimi nakuelewa vizuri....nakumbuka miaka ya 90s nilikua nasoma shule moja ya private watoto wote walikua wanaletwa na magari kasoro mimi naomba lift au napanda daladala, ila tangu niwe 25yrs sijawahi kukosa gari mbili au tatu nyumbani kwangu.........nina miaka sijapanda dala dala au basi za mikoani, tumkumbuke sanaa MOLA wetu tumetoka mbali.
 
KUMBUKUMBU LA TORATI 8 : 11-20

Kum 8:11-20​

Kum 8:11-20 SUV​

Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako. Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.
 
Amina ukiomba utafunguliwa wengi hatuombi tunapamban mpk malaik wanatushanga tulivyo wajing wakati riziki Mungu anayo anasubiri uombe akupatiee
 
Roho za korosho zitakwambia pesa ulizojengea nyumba ni za dili au connection...!?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work
Hapana mkuu.

Ni mapambano ya kutoka tamaa; nimemaliza chuo miaka 10 iliyopita.

Nyumbani ilikua hali mbaya kupindukia nikapambana kupasafisha; nashukru Mungu nilimakiza nyumba ya wazazi wangu kabla ya kujenga mimi (wengine wanaweza kebehi hapa) ila kwangu mzee wangu ni my number one hero. Alinipambania sana; Mungu endelee kumpa afya njema miaka mingi zaidi.

Nimemaliza chuo nikakutana na madeni ya mzee ya riba za kausha damu; nilipambana kuyalipa madeni yale kwa zaidi ya miaka mitatu; Mungu ni mwema nikayamaliza.

Mungu akanijalia uvumilivu na changamoto za mtaani, sikukata tamaa, nikaanza kupambana kufuta hali mbaya ya umaskini mkali wa nyumbani.

Mungu mkubwa baada ya kumaliza nyumbani nikaanza kujipambania; na leo nimeamka kwangu; watoto wakicheza na familia wakiwa na afya njema.

Tusikate tamaa, tuendelee ku-push popote tulipo, najua changamoto ni nyingi na baadhi ya watu hawapendi kuona wengine wakipiga hatua moja mbele, ila tusiwaogope; TUPAMBANE NAO.

HAKUNA KUSHINDWA KIZEMBE
 
Mkuu hongera sanaa sio mchezo ukiona tuliko toka kwa kweli mimi nakuelewa vizuri....nakumbuka miaka ya 90s nilikua nasoma shule moja ya private watoto wote walikua wanaletwa na magari kasoro mimi naomba lift au napanda daladala, ila tangu niwe 25yrs sijawahi kukosa gari mbili au tatu nyumbani kwangu.........nina miaka sijapanda dala dala au basi za mikoani, tumkumbuke sanaa MOLA wetu tumetoka mbali.
Hongera sana mkuu.

Wazazi/walezi huwa wanajitoa sana kwetu.

Ni Mungu wetu wa pili duniani.

Harakati ziendelee, tupige vita UMASIKINI, UJINGA NA UCHAWA.
Milango ya mishemishe izidi kufunguka
 
KUMBUKUMBU LA TORATI 8 : 11-20

Kum 8:11-20​

Kum 8:11-20 SUV​

Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako. Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.
Ujumbe wako umenibariki.
Nausoma nikiwa nafuatilia ibada kuopita Hope Channel.
Ubarikiwe
 
Hongera sana mkuu.

Wazazi/walezi huwa wanajitoa sana kwetu.

Ni Mungu wetu wa pili duniani.

Harakati ziendelee, tupige vita UMASIKINI, UJINGA NA UCHAWA.
Milango ya mishemishe izidi kufunguka
Mkuu ntakua mtu asie shukuru nikianza kulalamika kwa Mungu, nimepata kila Baba angu alicho kua nacho na kumzidi wakati nikiwa na umri mdogo,.....jambo mihimu ni kutojisahau uliko toka na kujua unako elekea na kukemea majigambo.
 
Njoo hapa kijiweni kwa mangi tujipongeze mkuu; niagize balimi ngapi?
FB_IMG_1724565658911.jpg
 
Back
Top Bottom