Na ukiona hawaijui ununio then jua hata hela ya kununua nyumba hio watakua hawana.
Hiyo conclusion ni hatari kibiashara! Ni hatari kwa sababu Ununio sio mtaa bali ni kitongoji, na kwa maana hiyo Ununio ni kubwa!!
Mtu anayeweza kuifahamu Ununio yote ni mkazi wa miaka mingi wa Ununio na sio anayeenda Ununio mara moja moja au mpita njia labda kama unataka kusema wenye hela wote wanakaa Ununio!
So, utakuwa sahihi endapo tu wenye hela wote wanakaa Ununio!!
Na hata huyo anayeifahamu Ununio yote bado atataka kufahamu Ununio sehemu gani!
Kwa mfano tukichukulia pale ilipo Shule ya Kiislamu na kule liliko Soko la Samaki... zote si zipo Ununio zile?! Hivi unaamini maeneo haya mawili yanaweza kuwakilisha interests sawa za mnunuzi?!
Tuache Ununio na twende sehemu ambayo majority watakuwa wanaifahamu!
Tukisema Makao Makuu ya Simba Sports Club yapo Kariakoo na Msikiti wa kwa Mtoro upo Kariakoo tutakuwa tumekosea?!
Unaamini interests zilizo yalipo HQ ya Simba SC ni sawa na kule kwa Mtoro?!
Ukitangaza unauza nyumba Kariakoo utamshangaa mtu atakayeuliza Kariakoo sehemu gani?!
Let's be serious bhana! Mi mtu hata akinitangazia kijijini kwetu anauza nyumba lazima nitataka kufahamu ni sehemu gani; seuze Ununio!!