Tunavyojidanganya kuhusu mapinduzi huko Sri Lanka

Tunavyojidanganya kuhusu mapinduzi huko Sri Lanka

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2013
Posts
749
Reaction score
875
Salaam wakuu,

Hivi majuzi kumetokea vurugu huko nchini Sri Lanka baada ya wananchi kutoka kila nyanja ya maisha kuingia ikulu ya Raisi na makazi ya Waziri Mkuu kuwataka kujiuzuru na hadi wakati huu bado wananchi wanaendelea kukalia makazi na ofisi hizo hadi pale viongozi hao watakapo jiuzuru.

Kwa picha ya kawaida tunaweza sema wale ni wananchi ndio waliofanya au wanaotaka kuitoa madarakani Serikali ila ukweli ni kwamba nyuma ya pazia ni kuna mkono wa mfumo na idara za usalama au nguvu toka mataifa ya nje. Wengi mataifa ya Afrika wanajidanganya kuwa hata wao kuna siku wanaweza fanya kama walivyofanya wananchi wa Sri Lanka ukweli ni kwamba kamwe haiwezi tokea.

NB: Ukiona Rais anapinduliwa au anauliwa ujue kuna mkono wa Idara a Usalama au mataifa ya nje.
 
Vyovyote iwavyo, iwe kwa msaada wa hayo mataifa yanayo twshwa kila aina ya uozo, au kwa msaada wa vyombo vya ulinzi na usarama wa nchi husika. Wakisha pindua watanufaika Nini?
 
Mimi nimebukua kinoma na nimeona kwa macho yangu na kutembea mtaani kwa nchi 13 za mabara matatu ila nikatoka na theory moja tu "theory of population" , haya yaliyopo kwetu kwasasa ni kutokana na aina ya binadamu tuliopo hapa bongo na hulka zetu au tuseme "population composition" iliyopo ambayo imekaririshwa upumbavu wa "zidumu fikra za Nyerere", iliyojazwa utii wa kijuha kwa viongozi hata wawe wabovu na mizigo mengine mashangingi ya mjini na mahuni ya bongofleva , population yetu iliyojaa uoga wa kijinga eti ukikaidi na kuandamana utapigwa tu sababu stoo kuna mabomu na virungu!!si mtupige mtuue kabisa mridhike, population iliyojazwa upumbavu kuwa mkubwa hakosei na hakosolewi , nchi iliyojaa ujinga wa "nenda urudi mwezi ujao eti tutafute faili lako", nchi iliyojaa upumbavu wa "tumekusikia tutalifanyia kazi" , lini? Sijui wanafundisha mzungu mmoja yuko bomani anatawala mkoa mzima yaani mtoto ajifunze kuwa mzungu ni bora kuliko mtu mweusi!! shame on taasisi ya ukuzaji mitaala!!

Haya yote yataisha in 50 years to come hapo hawa watawala wengi "wanaonyanyua mabega" na kuongea kibabe wakiwa tayari huko mavumbini Allahu Aaalam of course labda nasisi pia tutakuwa skeletons tayari sababu shida tangu utotoni sasa life span ya mwafrika akitoboa 80 huwa kachoka sana.
Mazee mengi yanayoliibia Taifa letu yana 60+ years yako "jioni" kabisa! Mazee haya yamejaa kule Masaki na Oysterbay sijui Msasani ukiyatembelea home unacheka stori zao kutawala nchi huku yako hoi kwa uzee!

Naamini wanangu dot com school bus English medium hawamjui Nyerere wala ujamaa sijui mkoloni, kizazi hicho kikifikia utu uzima 50 years to come wamebaki wenyewe tu mazee yote mafisadi yamededi patachimbika, hawa hawatakubali tozo na ugumu wa maisha lazima wataenda kuogelea Magogoni na kubanika wale tausi!

Ni kweli wazee na vijana tuliopo sasa ya Sri Lanka hapa bongo ni stori tu hatuwezi kufanya kama wao!

Time , uzee na kifo ni kiboko ya mafisadi!!
 
Ndoto za vijana wa vijiweni wengi wenye sifa kama za upande nisiopenda kuutaja hapa wana mawazo finyu kuhusu utawala, mambo yanatofautiana kwa mbaaali sana wanayotaka kulinganisha,

ilikuwa rahisi Kumpindua Nyerere, Mkapa na Magufuli lakini siyo Mwinyi, Kikwete wala Samia, japo na nilio wataja waliokuwa rahisi kupinduliwa ni kwa sababu ya Loss of political ventilation, NAO ISINGEKUWA RAHISI KWA ASILIMIA ZAIDI YA 50 Maana hatujafika wafanya hivo hatua waliyofikia.

mode ya kulinda usalama ni tofauti namsifu samia Kila wilaya wapo watu 1260 politely ambao wapo na shughuli zao za kawaida ila wakifanya kazi ya serikali kwa weledi na wengine hawajuani.

Mpango mwingine ni wa kuweka vituo bubu vya usalama kila mita 500 ndani ya majiji na miji pia kuweka nyumba kadhaa kusiko na miji zikifanya shughuli nyingine tofauti kumbe ni mama Huyu kaweza hapo ....

Britanicca
 
Umejenga hoja nyepesi sana nilivyoona tittle nikajua humu kuna madini kwelikweli lakini umeniprove wrong,wale ni wananchi wa Sli Lanka waliochoshwa na ugumu wa maisha hakuna mkono wa mtu wala nini,unataka kutwambia kwamba hadi suala la nchi kukosa mafuta kabisa kuna mkono wa mtu?
 
Hata wao wamesema walioruhusiwa kuingia mule ikulu ni wale ambao si waleta fujo
 
Back
Top Bottom