Tunavyojidanganya kuhusu mapinduzi huko Sri Lanka

Tunavyojidanganya kuhusu mapinduzi huko Sri Lanka

Lavit kuishia kuandika hvo pekee pana hitimisha ile kauli ya wahenga kuwa NYANI HALIONI KUNDULE.kama mtoa mada si mzima basi we mchangia mada shuja nondo zako tuone utimamu wa ubongo wako.
 
😁😁😁
image32.jpg
 
Umejenga hoja nyepesi sana nilivyoona tittle nikajua humu kuna madini kwelikweli lakini umeniprove wrong,wale ni wananchi wa Sli Lanka waliochoshwa na ugumu wa maisha hakuna mkono wa mtu wala nini,unataka kutwambia kwamba hadi suala la nchi kukosa mafuta kabisa kuna mkono wa mtu?
bro usipinge sana,kila kitu kinawezekana hapa duniani.yawezekana walifanya wao lakini lazima tujihoji maswali kadhaa.
Mfano,unafikiri maafisa usalama wote kweli walikuwa hawapati mishahara mpaka wambadilikie vile.Inafikirisha asee!
 
Hilo mbona lipo wazi. Mapinduzi ya umma hufanikiwa ikiwa vyombo vya ulinzi vitawasapoti wananchi kwa namna moja au nyingine (mgomo baridi). Kwa mfano, vyombo vya ulinzi kutotuliza maandamano. Rais akiona hivyo, lazima akimbie.

Huko Sri Lanka nchi imefilisika, hivyo hakuna aliyesalama kuanzia mwananchi wa kawaida mpaka askari.

Sasa, usidhani haiwezi kutokea Afrika. Inaweza kutokea sana tu ikiwa nchi imefilisika hadi hakuna hela za kuwalipa mishahara askari. Unafikiri askari hawataweka mgomo baridi ili rais atoke madarakani? Unaona kwa sasa haiwezekani kwa sababu askari wanalipwa mishahara.

Nakumbuka katika uchaguzi wa jimbo la Nyamagana (Mwanza), kulikuwa na mvutano wa kutangaza matokeo kati ya Wenje na Masha. Wanachama wa CHADEMA walijazana nje ya geti la kuingia ndani wakitaka Wenje atangazwe. Nilisogea pale kujua nini kinajiri. Cha ajabu lakini kawaida, kuna askari alikuwa analinda geti akawa anawaambia wanachi wakomae tu mpaka kieleweke ila wasifanye fujo. Sababu kubwa ya askari kugomea kuwatawanya wananchi kwa mabomu ni kutokana na Masha kuwadharirisha kwa kuwatukana askari alipokuwa waziri wa mambo ya ndani. Nimesahau kuna kauli aliizungumza.

Tuombee Tanzania isifilisike. Nchi ikifilisika inakosa utulivu, hata kama wananchi wake ni wajinga kiasi gani.
 
Back
Top Bottom