Tunavyosema mkataba una dosari muelewe, oneni ufafanuzi wa CCM hapa na ndio wamesema wanaelimisha watu

Aliadimika labda alikuwa busy kuandaa Makala ya Kila Jumapili🤣🤣

Ana vurugu maono huyu kakaangu. Either ni mbaya kwamaana ya taratibu zilizopo za kisheria kama Katiba, Manunuzi, na michakato ya kibunge au Ni Mzuri na umefuata kanuni na sheria.
 
Dubai ni nchi?
 
Hv umewahi kuckia kua BAHARI imekauka? Ndio mkataba utakua umefikia kikomo.
 
Yes CCM wanasema kweli, na huu ndio uelimishaji umma wenyewe kuhusu hii IGA. IGA sio mkataba, ni makubaliano tuu, mkataba ni HGA bado, utakuwa ni mkataba mzuri.
P
Mzee bahasha saivi zinaenda kwa wakosoaji, bado unasifia tu ?
 
MATOKEO YA MKATABA WA MILELE KATI YA ESSAU NA YAKOBO KWA VIZAZI VYAO VYOTE!

Madhara ya mkataba kati ya Essau na Yakobo yalikuja kuonekana baadaye baada ya Essau kupoteza kabisa haki zake zote za kiutawala, kiuongozi, kiuchumi, kidiplomasia na kisiasa. Chanzo cha mkataba ule ilikuwa ni tamaa ya Essau ya kupata pesa ya kufanyia shopping, kula nyama choma na kunywa supu ya pweza.

Baada ya Yakobo kugundua kuwa Essau alitaka sana apate hela ya matanuzi na supu ya pweza, aliweka sharti la kuandikiana mkataba. Lakini kwa kuwa akili ya Essau ilikuwa katika kupata vile vitu na jinsi atakavyowalingishia wenzake wa Mesopotamia, hakuweza hata kuwa makini kuangalia vipengere vya mkataba na wala yeye hakuona shida mkataba kuandikwa na Yakobo.

Baadaye alipokuja kushtuka akakuta mkataba ulikuwa hauna ukomo - ulikuwa ni wa milele na kuwa Yakobo alikuwa amejimilikisha kila kitu. Lakini Essau alipotaka kubadili vile vipengere vibaya ndani ya mkataba, Yakobo alikataa lakini hata Mahakama ya rufani chini ya Mzee Isaka ilisema kuwa mkataba ule hauvunjiki. Mkataba ule ulipora haki zote hata za vizazi vya Essau katika nyanja zote - kidiplomasia, kiuchumi, kiutawala, kisiasa, nk (Mwanzo 25).

Wataalamu wengi wa Biblia wanakubaliana pia kuwa uzao wa Yakobo ndilo taifa la Israeli na uzao wa Essau ndilo taifa la Jordan. Je, kama hiyo ni kweli kuhusu historia ya mataifa hayo mawili yaliyo jirani, unayaonaje mahusiano ya nchi hizo mbili na hasa ushawishi wa kila nchi katika jumuiya ya kimataifa kisiasa, kiuchumi, kijeshi na kidiplomasia?

Uliwahi kusoma kisa cha Essau na Yakobo kwa jicho la mkataba? Unafahamu kuwa mikataba yote inayohusu rasilimali inahitaji umakini sana kwa kuwa mtu akikabidhiwa rasilimali haziachii kirahisi? Unafikiri ni kwa nini Yakobo aliandika mkataba mwenyewe bila kumshikirisha Essau?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 22 Julai 2023; 07:08 am.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajulikana hata nikiwa mdogo nimekutumia 10 years because of you.. na wengineo malegend Pascal Mayalla
it's true it's not fair at all

Just imagine, haka kaghorofa changu pale kwa mtogole, hiyo room ni self, ili kuzuia water overflow, public toilet nimeiweka underground, wale jamaa wa sensa ya makazi wameandika ina two floors!. REA waliponifungia tuu umeme wa gridi, imekuwa ni majanga, deni limekuja 240,000 eti ni deni la nyuma la nyumba!. Nikawaambia basi ondoeni umeme wenu, nitatumia vibatari, sasa ndio najiandaa kufunga sola!.
P
 
Yes CCM wanasema kweli, na huu ndio uelimishaji umma wenyewe kuhusu hii IGA. IGA sio mkataba, ni makubaliano tuu, mkataba ni HGA bado, utakuwa ni mkataba mzuri.
P
Nakuona mwanasheria uchwara, umeona jana mahakamani mawakili wa serikali wamesema kuwa ule ni mkataba. Acha njaa.
 
Yes CCM wanasema kweli, na huu ndio uelimishaji umma wenyewe kuhusu hii IGA. IGA sio mkataba, ni makubaliano tuu, mkataba ni HGA bado, utakuwa ni mkataba mzuri.
P
Mheshimiwa P hembu tuache basi kidogo, heshima yako ni kubwa sana, hili suala likaushie tu.
 
Nakuona mwanasheria uchwara, umeona jana mahakamani mawakili wa serikali wamesema kuwa ule ni mkataba. Acha njaa.
Issues za kisheria sio issues za nani kasema nini, ni points of law, sheria inasema nini!. Kama sheria inasema the age of the majority ni miaka 18, na under 14 ni minor, ukitoka na under 14, hata akiridhia!, ni ubakaji na unakula 30!.

Sheria imeweka sifa za mkataba, ile IGA, haina sifa hizo, hivyo yale ni makubaliano tuu, ndio maana tumeishangaa serikali yetu, Bunge letu na wanasheria wetu vilaza!.
If you have time karibu mitaa hii
 
Wewe ni mwanasheria uchwara, ile haina sifa ya kuitwa IGA, jaribu kuficha ushamba wa kisheria kwa kutafuta IGA zilizowahi kusainiwa na nchi nyingine ulinganishe na ule upuuzi ambao wewe na Dr Msukuma na Nape mnauita IGA.
 
Msichoelewa ni nini? Mbona Watanzania wagumu hivi? Huu mkataba unao ukomo kama walivyofafanua hapo juu.

Wanamaanisha kwenye Bandari ikitokea maji yakakauka kabisa permanently au watu/wateja wakaacha kabisa kutumia Bandari ndio mwisho wa mradi. Hivyo ukomo upo, acheni kuchochea.
 
[emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…