Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
- #221
Hayo hayakufanywa na vikosi vya mauaji vya kisiri. Walikuwa TISS ambao kila mtu aliwajua. Sasa kama KIkwete aliwatumia TISS vibaya katika suala la Ulimboka haihalalishi uundaji wa kikosi cha Wasiojulikana, kikosi rasmi kisicho rasmi. Na pia Nyerere, kama unavyosema katika mazingira yale ya chama kimoja Nyerere alitumia mamlaka yake kuwakamata watu waliopinga serikali na waliwekwa gerezani "kihalali"Enzi za Nyerere kulikuwa na upinzani unaojulikana kikatiba?. Walikuwepo wanasiasa walioteswa, kumbuka magazeti yalikuwa ni ya serikali, hakukuwa na free media kama leo hii.
Kina Ulimboka waliofanyiwa ukatili ilikuwa ni awamu ya JPM?.
Kombe aliyepigwa risasi licha ya kunyoosha mikono kusalimu amri ya kukamatwa, ilikuwa ni awamu ya JPM?.
Kambona aliyelazimika kuishi uhamishoni Uingereza, ilikuwa ni awamu ya tano?.
Inabidi uwe na akili za mwendawazimu kulinganisha kikosi cha Wasiojulikana na mambo ambayo yalifanywa na mtu kama Nyerere dhidi ya watu waliopinga serikali katika siasa za chama kimoja. Wakati huo hayo yalikuwa mazingira ya uhaini. Upinzani wa sasa ni uhaini? KItendo gani cha kihaini kimefanywa na Ben Saanane, Lissu? Upinzani upo upo kisheria. Sasa kwa nini umfanyie udhalimu mtu anaekupinga na kukukosoa kisheria? Kama amekutukana mpeleke mahakamani sio umuundie kikosi cha Wasiojulikana kitakachomshughulikia kisiri.
Haikuwa siri kina Kambona kutafutwa na serikali, kina Kamaliza, Bibi Titu, Mapalala, kuwekwa ndani.Hata jeshini tuliimba Kambona aliagiza Chipaka na Kamaliza pindueni nchi mkiweza. HUo ulikuwa uhaini.