Tunawezaje kuzuia double agents, inazidi na itazidi kuwa changamoto

Hili jambo la Viongozi wetu kuwa karibu au na mahusiano Na double agent Ni hatari sana. Mwezi huu January nimekutana Na hii ngozi nyeupe Na nikiwa naongea naye akanitajia contacts kibao za viongozi wetu wanao taka kumnyandua...Na anayajua mambo Mengi ya huko Zanzibar...wanamuomba ufafhiri wa kujenga shule bila kujua Ni hohe hahe Kama Yule wa β€œ mama Samia Nipe uraia” nikachezee taifa stars toka Hemel Hempstead...
Viongozi wa enzi za kifimbo ndio walio kuwa serious Na haya mambo ya Agent, lakini sio hawa wa siku hizi...
 
Nafahamu kuna wengine wachache wameuchukulia uzi huu in a negative way, wala hauko hivyo, niliyoyasema ndiyo kweli yenyewe msiyotaka kuisikia,
Leo hii hata nikikuambia uvuke boda hapo uende Kenya, ukashangae mpaka leo hatuna ubalozi wa kueleweka tumepanga ghorofani tena upande mmoja wa floor [emoji24], nayo utakataa, halafu unategemea ufanye kazi kwa weledi,
Wakuu tuisadie nchi yetu, safari bado ni ndefu sana, tuache u much know na tamaa za mali, mali huisha lakini nchi itabaki, ukielezwa kitu fikiria kwann umeulizwa siyo kubishana
muwe na jumapili njema ndugu zangu.[emoji120]
 
Ngozi ipi hiyo mkuu
 
Ila binadamu kwa namna tulivyojawa na husuda unaweza kukuta maelezo ya kwenye namba 1 na 2 yote hayana maana ila mlengwa wa mleta mada ni huyo "Kumbikumbi" aliyewekwa namba 3 ili tu kumharibia.
It seems so
 
Sisi sio watu wa bidii sana. Zamani ndio tulikuwa na cha kuficha hasa mipango ya wapigania Uhuru wa ukanda wa SADC, makazi yao, majina yao, future yao.
Tuna nini cha kuficha sasa? Hata viongozi sioni kama tunawaandaa.
Tuna nini cha kupelekwa Kenya au Rwanda?
Hatupangi ushawishi dhidi ya serikali za nje. Tuna nini cha kuficha?
Tunafanya ujasusi wa kisasa utakaousadia nchi?
Vitu tunavyovifanya vingi ni vya kawaida ambavyo havihitaji double agents ila observation ya kawaida tu na trend reading.
Chombo cha kulindwa nchi hii ni CCM as party na zile organ zake.
Ujasusi wa CCM unatakiwa kuwa imara kuliko ujasusi wenyewe wa ngazi ya Taifa.
CCM inatakiwa kutunza siri kuliko hata inayotunzwa katika ngazi ya kitaifa.
CCM inatakiwa kutunza mifumo kuliko kawaida.
Mipango ya CCM ndio mipango ya Tanzania.
 
Kati ya vitu ambavyo nchi yetu na walio kwenye nafasi za uongozi vimekosekana.
1. Ukosefu wa Uzalendo
2. Uadilifu na utawala bora.
3. Miiko ya utumishi
Mambo haya yanachochea kutumia yeyote kwa vyovyote wakati wowote ili mradi tu mtu huyo afanikiwe kuwa sehemu ya upigaji kwahiyo wageni wanaweza kuwa recruited kama wapambe waleta taarifa au vyovyote
Pia watu wananunulika ukitaka kujua kuwa iko hivyo angalia vyama vya siasa huyu alikuwa huku ghafla bin vuu yuko kule. Kwahiyo watu wako tayari kuwa chochote kama kuna chochote kitu.
Mipaka ya uongozi wala maadili hayapo yaani kila mtu ni kambale hii haipo.
Mi sijawahi kumkubali yule mswahili wa dar kwa kweli nauna uso wake uko kwenye maigizo tena ya wazi kuwa eti mpenda taifa. Tunaweza kusema tuna nini ambacho hawakijui spying sio lazima iwe kwa kivita kiuchumi au kiutamadani na jambo baya kuliko ni pale utamaduni wenu unapohujumiwa huo ndio utu wetu unaweza kujenga mifumo bora ya kiuchumi na kiulinzi.
 
Leo hii hata nikikuambia uvuke boda hapo uende Kenya, ukashangae mpaka leo hatuna ubalozi wa kueleweka tumepanga ghorofani tena upande mmoja wa floor [emoji24], nayo utakataa, halafu unategemea ufanye kazi kwa weledi,
Nimecheka kama mazuri vile! Kwahiyo UBALOZI WA TANZANIA umepanga OFISI YA UBALOZI kule KENYA πŸ‡°πŸ‡ͺ πŸ™ŒπŸΌπŸ˜‚
 
Mkuu licha ya umasikin wetu ila elimu yetu ni duni sana. Yawezekana tukawa miongoni mwa nchi zenye mifumo mibovu ya elimu.
Kenya ni maskini sana lakini elimu yao inawafichia aibu .
Bahati mbaya sana mpaka kufikia sasa watawalavktk nchi hii tu hawapendi wanachi wake waelimike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…