Me too
JF-Expert Member
- Feb 9, 2015
- 7,388
- 9,333
- Thread starter
- #101
Ewalaaaa nimekupata vizuri mkuuu,,,,, yaani umedadavua njema mno
Ila nnaukakasi kuna kitu umenisangaza uncle,,, at I Adam hakuwa mtu wa kwanza? Unamaanisha alikuwepo juma, aly, muda, zawadi n.k? Ijapokuwa ni nje ya mada hapa umenikanganya asee?
Na ile laana mkaijaze dunia inamaana hukumbuki?
Unataka kuniaminisha walishajazanaga?
Ila nnaukakasi kuna kitu umenisangaza uncle,,, at I Adam hakuwa mtu wa kwanza? Unamaanisha alikuwepo juma, aly, muda, zawadi n.k? Ijapokuwa ni nje ya mada hapa umenikanganya asee?
Na ile laana mkaijaze dunia inamaana hukumbuki?
Unataka kuniaminisha walishajazanaga?
Mkuu kitu cha kwanza unachohitaji kujua ni Adamu hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa hapa duniani, jambo hili limechukuliwa kimakosa na watu wengi sana kwamba Adam alikuwa ni mtu wa kwanza kuumbwa.
Pia unatakiwa ujue kwamba sio kila andiko la Biblia au vitabu vitakatifu kama Qur'an laweza kuchukuliwa kama lilivyo (literally) , kuhusu tunda alilokula Adam haina maana ni tunda la dhahiri kama pera, chungwa nk, la hasha. Tunda katika lugha ya kiroho ni matokeo yatokanayo na matendo ya mtu, mfano mtu mwema huzaa matendo mema na mtu mbaya huzaa matendo mabaya, hivyo mti ni sawa na mtu na matunda ni sawa na matendo, hivyo Adam alikatazwa na Mungu kushiriki matendo mabaya ya watu wabaya wa zama hizo, kumbuka Adam hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa bali yeye alikuwa mtu wa kwanza kuwasiliana na Mungu na watu wengine waliomzunguka katika jamii aliyokuwa anaishi wengi wao walikuwa waovu kama Ibilisi.
Hebu tusome jinsi Nabii Yesu (as), bingwa wa kauli za mifano, anavyojenga hoja ya mti na matunda na mwisho akatoa ufafanuzi wake; katika (Luka 6:43-45) Yesu anasema:-
Mti mzuri hauzai matunda mabaya wala mti mbaya hauzai matunda mema, kwakuwa kila mti hujulikana kwa matunda yake, kwakuwa watu hawavuni matini kutoka kwenye miba wala hawavuni zabibu kutoka kwenye-----.
Hapo sasa utaona Yesu kafafanua nini maana ya mti na matunda.