Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Hakuanza leo, alianza akiwa shule na aliendelea hivyo hivyo kabla ya kuwa Mbunge, aliendelea hivyo hivyo baada ya kuwa Mbunge na anaendelea hivyo hivyo baada ya kuporwa ubunge kwa hila.
Hakuanza leo...alianza akiwa mzima wa afya, aliendelea hivyo akiuguza majeraha yaliyotokana na kumiminiwa risasi zaidi ya 30 na anaendelea hivyo hivyo pamoja na mwili kujaa makovu ya risasi.
Hakuanza leo...alianza akiwa kijana na aliendelea hivyo akiwa mwanasheria mdogo, aliendela hivyo hivyo akiwa Rais wa Wanasheria na leo anaendelea hivyo hivyo akigombea urais wa Tanzania!
Ndugu zangu Watanzania, tukimwacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni mgombea gani wa Urais aliyekuwa na historia kama ya Mh. Tundu Antiphas Lissu? Ni mgombea gani alipitia heka heka alizopitia Mh. Tundu Antiphas Lissu mikononi wa utawala kandamizi unaotumia vyombo ya dola kunyamazisha upinzani?
Ndugu zangu Watanzania, hebu tujikumbushe na kujiuliza:
- Ni mgombea gani mwenye jeuri ya kusimama mbele ya wananchi na kuwaahidi uhuru na usalama wao kama katika utawala wake wananchi hao waliishi kwa hofu?
- Ni mgombea gani mwenye jeuri ya kusimama mbele ya wananchi na kuwaahidi haki na usawa kama wakati akiwa madarakani wananchi waliporwa hovyo mali zao?
- Ni mgombea gani mwenye jeuri ya kusimama mbele ya wananchi na kuwaahidi umoja na mshikamano kama wakati wake wananchi walibaguliwa kiitikadi, kikanda na kikabila?
Pamoja na hayo kumbukeni...
Mh. Tundu Antiphas Lissu hasimulii aliyosikia kuwakuta waliotumia uhuru wao wa kidemokrasia kuwakosoa walioko madarakani, hapana, anasimulia yaliyomkuta yeye katika harakati za kutetea uhuru, usawa, haki na utawala unaoheshimu sheria.
Mh. Tundu Antiphas Lissu hasimulii aliyosikia kuwakuta waliothubutu kupinga utawala huu jinsi walivyotekwa, kuteswa na kupotezwa, hapana, anasimulia yaliyomtokea yeye mikononi vyombo rasmi vya dola na visivyo rasmi vinavyodaiwa kutojulikana.
Huyo ndiye Mh. Tundu Antiphas Lissu yule yule wa siku zote...NI YEYE!