Tundu Lissu, acha kumshambulia Hayati Magufuli

Tundu Lissu, acha kumshambulia Hayati Magufuli

Na huo ndio ukweli,magufuli ndio rais aliyekipenzi cha watanzania wengi zaidi ukimtoa baba wa taifa,kasolo wale tu aliowashughurikia.
Kupendwa kwa Magufuli ni dalili kuwa brainwashing yake ilisambaa sana.Lazima watu wapewe dozi ya elimu ili kuwaondoa na brainwashing hiyo.

Tusipomsema Magufuli mtataka Mkapa asisemwe, Madudu ya Kikwete yasisemwe pindi akifa,na madudu ya Samia yasisemwe pindi akifa.

Tunakataa precedence hiyo ya kufunika kombe mwanaharamu apite eti kisa muovu kafa
 
Ni kweli, anapaswa kuchagua adui wa kumshambulia kwa umakini. Kwa hali mbaya iliyopo sasa hivi nchini watu wengi wanamkumbuka JPM.

Strategically he should stop attacking Magufuli kwani marehemu kwasababu ya utawala mbovu wa Samia, Magufuli anakumbukwa sana!! Samia anashindwa hata kumaliza miradi alioachiwa ; imebakia porojo tu ya "kazi iendelee" ya kuuza nchi!
To ignore Magufuli's supporters is to commit political suicide! Tunaona hata Samia sasa anajipendekeza kwa wafuasi wake kwa teuzi anazofanya hivi sasa!!! Kama atafanikiwa that remains to be seen.
 
Siyo Lisu tu bali wengi wetu tutaendelea kumsema kwa mabaya yake aliyotufanyia

Kama ccm watamsema vibaya waacheni wafanye hivyo lakini nyie vyama vingine hamtafaidika na strategy hiyo!
 
Kinachotakiwa ni kuwaunganisha Watanzania wote wa dini zote, makabila yote, kanda yote nyuma ya Agenda inayokubalika na wote.

Kupigania Bandari, katiba mpya, kuiondoa CCM madarakani.

Naona (Sauti ya Watanzania), Dr Slaa, Mwambukusi, Askofu Mwamakula, Mbatia wanaweza kuishinda CCM. Wako zaidi kimkakati na wanaeleweka kirahisi na wengi. Wanahitaji jukwaa kubwa kuwafikia Watanzania wengi

Wamesema wazi wako tayari kuungana na vyama vyote, wasio na vyama, dini zote na wasio kanda zote kupigania Maslahi mapana ya Taifa hata kujitolea maisha yao.
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, ni hatari kubwa mno kuendelea kumshambulia Hayati Magufuli.

Pamoja na mapungufu machache ya kibinadamu ya Hayati Magufuli wakati wa utawala wake, asilimia kubwa ya Watanzania walimpenda mno na bado hajatoka mioyoni mwa Watanzania wengi.

Hata hivyo, kuendelea kumshambulia mtu asiyekuwepo inasaidia nini?

Je, hiyo si sawa kabisa na kupambana na kivuli?

Ndugu zangu wa CHADEMA mnafeli wapi nyie?
Kumshambulia Magufuli ni kujitafutia kufeli kisiasa.
 
Ni mwendawazimu tu na mpumbaf ndio anaweza kukejeli kazi iliyofanywa na huyu mzee.
Ikiwa ,
1. kuvunja mikataba ya kifisadi ya madini na Bandari ambayo tunaona sasa ikipigiwa debe.

2. Kujenga bwawa la umeme pamoja na kupigwa vita ikiwemo kunyimwa fedha,

3. Kuzuia mifumuko ya bei za bidhaa hovyo kama chakula,mafuta n.k

4. Kuzuia utoroshwaji madini ikiwemo kuanzisha masoko ya madini nchi nzima.

5. Kurudisha nidhamu jwa watumishi, sasa tunaambiwa 45% ya ma Dc hakuna wanalolifanya.

Kama haya na mengine mengi aliyoyafanya sio ya kishujaa,mbona watangulizi wake walishindwa? , hata mama ameshafeli kwwnye mambo mengi tu, ni lipi basi kwako angelifanya lingekuwa la kishujaa?
So na wewe ni mnyonge? 1.5 tr iko wapi?
 
Back
Top Bottom