Tundu Lissu, acha kumshambulia Hayati Magufuli

Tundu Lissu, acha kumshambulia Hayati Magufuli

Huyu jamaa ana ugonjwa unaitwa Histrionic personality disorder au tuseme attention seeking behaviors
Ni wa kumpuuza tu
 
Lissu ni activist material! na sio Political Material

Akipanda jukwaani na kichaa pia kinapanda!

Nilimshangaa kumsikia akisema kuwa kuna hifadhi ya mzungu ina ukubwa wa 6,000,000sq kms.

Sasa wanapanga kumshitaki ili awasafishe.

Hifadhi kubwa 6a wanyama nchini ni Nyerere 50sq kilometers.

Vyanzo vya Lissu sijui huwa anavipata wapi?
Kama uliwahi kuishi vijijini huhitaji sana kujiuliza kuhusu Lissu mkuu , anachokifanya anakijua hapo ni kwamba alikuwa anatafuna unyasi ulainike then aingize shimoni yule mdudu ang'ate unyasi alafu avute harka mdudu atokee nje apigwe jua afe,.

Ukitaka kujua hili angalia wamiliki wa kampuni walipojitokeza na kutaja idadi za heka wanazomili tena wanasema wamepewa na kijiji tangu lini kijiji kikampa mwekezaji ekari zaidi ya laki na kitu ? Hapo Lissu amepata ushahidi kamili sasa waende mahakamani sasa watajua hawajui
 
Naicjukia CCM toka moyoni lakini Ukweli usemwe CHADEMA haitakuja kuingia ikulu. Sio Mbowe wala genge lake watakuja kuona ikulu labda labda labda.... Waache kupambana na Hayati Magufuli.
 
Eti Hayati, yaani Jiwe unamwita hayati[emoji848] Hapo hapo eti alikuwa na mapungufu madogo na mwisho unamaliza kuwa alipendwa na Watanzania. Kweli nimekosa jina la kukupa kwani uko huru kutumia kichwa chako upendavyo
Na huo ndio ukweli,magufuli ndio rais aliyekipenzi cha watanzania wengi zaidi ukimtoa baba wa taifa,kasolo wale tu aliowashughurikia.
 
Ukweli ni kwamba watanzania wengi bado wanamkumbuka sana Magufuli na huwaelezi chochote na ukichanganya na ugumu wa maisha unavyozidi wanafikiri Baba Magufuli angekuwepo kungekuwa na unafuu

Hii issue tu ya mafuta wanaamini Magufuli angesema neno tofauti na sasa mama abdul kajikalia kimya 😁 anajipakia zake 💄💋 anaingia zake ofisini muda wa kutoka ukifika anatoka na hamna la kumfanya nyie pigeni kelele sijui hamna mafuta sijui nini hana mpango mpambane na hali zenu
 
Na huo ndio ukweli,magufuli ndio rais aliyekipenzi cha watanzania wengi zaidi ukimtoa baba wa taifa,kasolo wale tu aliowashughurikia.
Mh. Tundu Antiphas Lissu, tafadhali endelea kupigilia hapo hapo kwenye mshono. Mwaka 2020 hatukuwa na uchaguzi bali uchafuzi. Kipenzi cha watu hahitaji vyombo vya dola kuiba kura kushinda uchaguzi. Angalia matakataka yaliyojaa bungeni hivi sasa.
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, ni hatari kubwa mno kuendelea kumshambulia Hayati Magufuli.

Pamoja na mapungufu machache ya kibinadamu ya Hayati Magufuli wakati wa utawala wake, asilimia kubwa ya Watanzania walimpenda mno na bado hajatoka mioyoni mwa Watanzania wengi.

Hata hivyo, kuendelea kumshambulia mtu asiyekuwepo inasaidia nini?

Je, hiyo si sawa kabisa na kupambana na kivuli?

Ndugu zangu wa CHADEMA mnafeli wapi nyie?
Sio kila binadamu ni mwenye Hekima 😅🙏🙏
 
Ni kweli, anapaswa kuchagua adui wa kumshambulia kwa umakini. Kwa hali mbaya iliyopo sasa hivi nchini watu wengi wanamkumbuka JPM.
Adolf Hitler bado anasemwa kwa ukatili wake miaka mingapi imepita? Itakuwa Magufuli juzi tu? Herode aliyemsulubisha Yesu anasemwa miaka mingapi imepita? Itakuwa Magufuli juzi tu?
 
Spana za Lissu zinahitaji uvumilivu, Lissu sio mtu wa kuchagua Battles yeye anachakakaza haangalii sura wala feelings za kibwengo yoyote.
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, ni hatari kubwa mno kuendelea kumshambulia Hayati Magufuli.

Pamoja na mapungufu machache ya kibinadamu ya Hayati Magufuli wakati wa utawala wake, asilimia kubwa ya Watanzania walimpenda mno na bado hajatoka mioyoni mwa Watanzania wengi.

Hata hivyo, kuendelea kumshambulia mtu asiyekuwepo inasaidia nini?

Je, hiyo si sawa kabisa na kupambana na kivuli?

Ndugu zangu wa CHADEMA mnafeli wapi nyie?
Kuua watu sio mambo machache.
 
Naunga mkono hoja, mtu huna sababu kumshambulia mtu anbaye hawezi kujitetea tena nashauri aache kabisa maana huko aliko, alikasirika ni anamshutua tuu YEYE, na mtu anaitwa fasta dakika sifuri!.

Ni kweli, alitenda mema mengi makubwa mazuri kuliko mabaya na maovu yake, na kabla hajatwaliwa alitubu, akasalishwa sala ya toba, akapakwa mafuta ya Krisma, hivyo dhambi zake zote za hapa duniani, zikaondolewa na zikasamehewa na Mungu mwenyewe!.

Saa hizi hivi tunavyozungumza hapa, sii wengi wanajua mahali alipo sasa, sisi wenzenu tuliojaaliwa kujulishwa tunaomba tuwaeleze kupitia Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
Hata Ben,azeory nk, hawakuweza kujitetea lkn waliliwa na chatu.
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, ni hatari kubwa mno kuendelea kumshambulia Hayati Magufuli.

Pamoja na mapungufu machache ya kibinadamu ya Hayati Magufuli wakati wa utawala wake, asilimia kubwa ya Watanzania walimpenda mno na bado hajatoka mioyoni mwa Watanzania wengi.

Hata hivyo, kuendelea kumshambulia mtu asiyekuwepo inasaidia nini?

Je, hiyo si sawa kabisa na kupambana na kivuli?

Ndugu zangu wa CHADEMA mnafeli wapi nyie?
Alipendwa na watanzania gani yule maku.aliokuwa anawateka ? Alopokonya dola? Alolea sabaya? Alieqmuru apewe kilema asie na hatia? AU hujui kuna watu waliliwa tako kwa amri yake?
 
Siasa zinabadilika kwa kasi sana, adui yako asubuhi, ni rafiki yako jioni kadhalika rafiki yako mchana, usiku anaweza kuwa adui yako. Ni ngumu sana kuelewa wakati gani Tundu Lisu anazungumzia machungu yake kama mtu ( binafsi) na machungu ya chama chake au tuseme ya ''wananchi''

Upepo wa kisiasa ulivyo sasa hauruhusu Tundu Lisu 'kumsimanga'' Mhe. Magufuli ( anayedaiwa wakati wa Rais wake kumjeruhi), wala hauruhusu yeye kumtukana au kumbeza Rais wa nchi Mhe. Samia Suluhu kwasababu yeye ndio kamtoa korokoni ya ughaibuni.

Nchi imegawanyika, kuna idadi kubwa ya watu wanampenda bado Magufuli, na pia kuna idadi kubwa sana wanaompenda Mhe. Rais. Kwa kuwabananga wote wawili ( Hayati Magufuli na Mhe Rais), CHADEMA hawaongozi idadi yoyote ya wafuai zaidi ya kuwapoteza.

Tundu Lisu aache kuongelea machungu yake, aeleze mbadala wa yale anayoyaona hayafai, atueleze CDM watafanya vipi tofauti. Pia CDM pamoja na Tundu Lisu waache kuwa watu wa mihemko ( reaction) dhidhi ya serikali ( Katiba mpya, Wamasai Ngorongoro na suala la Bandari)

Watengeneze majibu ya kisera namna watakavyoshughulikia matatizo ambayo serikali imekwama au inapata changamoto. Mfano, wao wana njia zipi za kuendesha bandari, namna gani watafanya bei ya mafuta Sinza iwe sawa na Misenyi etc.....sio kila siku kutafuta siasa za confrontations.

Halafu kwa ushauri tu warudisheni tu akina Halima, watu wote wenye akili wanafahamu nini kilifanyika....
 
Ndugu yangu Tundu Lissu, ni hatari kubwa mno kuendelea kumshambulia Hayati Magufuli.

Pamoja na mapungufu machache ya kibinadamu ya Hayati Magufuli wakati wa utawala wake, asilimia kubwa ya Watanzania walimpenda mno na bado hajatoka mioyoni mwa Watanzania wengi.

Hata hivyo, kuendelea kumshambulia mtu asiyekuwepo inasaidia nini?

Je, hiyo si sawa kabisa na kupambana na kivuli?

Ndugu zangu wa CHADEMA mnafeli wapi nyie?
Siyo Lisu tu bali wengi wetu tutaendelea kumsema kwa mabaya yake aliyotufanyia
 
Back
Top Bottom