Tundu Lissu achukua fomu kugombea Makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa

Tundu Lissu achukua fomu kugombea Makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa

Waganga wa gamboshi mmepewa smartphone mnakuja kufanya majaribio ya kuzitumia humu jf
Chacha Wangwe (RIP) = Tundu Lisu?

Kazi kweli kweli na Serikali ilikuwepo, Sasa tutaona kama ya kale yanaweza kujirudia.
 
Hata hii habari ya Lisu kugpombea umakamu inahitaji independent verification. Mwanzoni kulikuwa na fanfare leo utasikia Lisu kesha kata iketi ya kuja Tanzania, kesho utasikia Septemba 7 anatua...Hii ya kurejea kimyakimya kuna jambo kubwa nyuma yake, a Mbowe kaamua kucheza na aliki za watu kama alivyozoea.

Wakati Slaa amejiondoa Chadema, Mbowe alisema yuko likizo. Taarifa nilizonazo zisizo na chembe ya mashaka ni Lisu kuungana na Zito ACT wakati wowote baada ya kurejea nchini. Watch this space.
Wewe endelea kuwatch utawatch mpaka mwisho wa dunia
 
Ukiweka wewe nyumbani kwako imetosha
So anachukua kwa sababu Pro Safari kaamua kutogombea, angekuwa anagombea asingechukua. Yaani kupokezana uongozi hadi mtu aliyeshika uongozi aamue kuacha mwenyewe duuh. Hii ndio hasara ya kuwa na katiba isiyoweka ukomo wa uongozi.
 
Kwanini sio uwenyekiti zile hisia za uwenyekiti ndio sababu ya risasi imepata jibu RIp Wangwe!
WanaJF

Habari za hivi Punde ni kwamba Jabali la kisiasa Tanzania na Afrika Tundu Antipas Lissu amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa na tayari amekwisha jaza fomu na kuzirejesha.

Akihutubia mkutano mkuu wa Kanda ya Kaskazini hivi Punde,Mwenyekiti wa chama Taifa Freeman Aikael Mbowe ameeleza kuhusu tukio hilo la kishujaa alilofanya Tundu Lissu.

Mbowe amesema Makamu Mwenyekiti wa sasa Professor Abdallah Safari ameomba kupumzika na hivyo Lissu ameona ni wakati muafaka kwake kuomba nafasi hiyo.

Wakati huo huo, Freeman Aikael Mbowe amekubali maombi ya vijana nchi nzima ya kugombea tena nafasi ya Mwenyekiti Taifa na amerejesha fomu yake kwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa.

Akirejesha fomu hiyo huku akishangiliwa kwa mayowe na wajumbe wa mkutano mkuu Kanda ya Kaskazini Mbowe amesema alichukua muda mrefu kutafakari ombi hilo la vijana na alikuwa na nia ya kutogombea tena nafasi hiyo.Hata hivyo amesema alirudisha moyo nyuma baada ya kutizama imani kubwa waliyo nayo wanachadema kwake na kuona akikataa maombi yao itakuwa ni kuwasaliti.

Akizungumzia yaliyotokea katika uchaguzi Kanda ya Pwani Mbowe amesema amesikitishwa na mambo ya uongo yanayoandikwa na baadhi ya watu na akasema kwenye mambo haya ya uchaguzi huwezi kuzuia ajali za kisiasa.Hata hivyo amewahakikishia watanzania kwamba Mhe Sumaye anahitajika ndani ya Chadema kama walivyo wanachama wengine na amesema yaliyotokea yatamalizwa kwa upendo na nidhamu ya hali ya juu ndani ya chama.
 
Democrasia iliyo ndani ya CDM hata mbowe mwenyewe haielewi. Ni wapuuzi Wachache tu wanaoweza kuamini kuwa Chadema Ni chama Cha democrasia ya kweli.

How comes Mtu anashangiliwa tu na wachaga wenzie wa Kanda ya kaskazini anajiona anafaa kuongoza chama hiki mpaka atakapochoka.. what kind of this shit?.
Mbowe hayo mayoe Umekuja Hadi huku kwetu kusini ukayasikia je umeenda magharibi mwa Tanzania ukayasikia au ndo kuthibitisha Ile kauli ya Chadema Ni chama Cha Wachaga.

Soon Naiona Chadema inavyoenda kugawanyika Kama ilivyotokea kwa CUF. Kwa wasio elewa siasa usisumbue akili yako kunielewa Ila kwa wanao ijua siasa bila shaka utakuwa umeelewa Nini namaanisha kuhusu yajayo.

Na napenda tu kuwakumbusha nyie vyama vya upinzani Mfumo huu mnaoutumia kupata viongozi wenu wa ndani ya chama hata serikali itakuja Iutumie huohuo kupata viongozi wake na Hakuna mtu atakaepata nguvu ya kuhoji maana yeye mwenyewe atakuwa mfano tosha.
Tutegemee tu Uchaguzi wa Ndio/Hapana unarudi kwa kasi katika serikali hapo karibuni.
The future is incomplete.
 
Kumbe anaweza kuja kujaza form za uongozi kwenye Chama chake, lakini hawezi kuja kwenye kesi zinazomwandama na kukamilisha ushahidi wa kesi yake ya kushambuliwa? Mazingaombwe ya Chadema huwezi kuyafahamu? Priority yao ni nini? Kuwafurahisha wanaowalisha? Je TL aliingia kweli Tanzania? Sheria za ukimbizi hazikubaliani na raia kurudi kwenye nchi aliyokimbia kwa sababu mbalimbali, Nini hasa TL amekubaliana na wafadhili wake? Je, TL yupo salama zaidi Nairobi?
Crap
 
Hiyo nafasi ya makamu mwenyekiti ilipaswa kupewa mzanzibari Ina maana Chadema sio Chama Cha kitaifa Tena ? Ni Cha Tanzania bara tu?
Sio bara tena ni chama cha wachaga tu huyo nyavu zinamuhusu
 
Magufuli nina uhakika atawaua wote.
Na sasa hivi anajitoa kwanza kwenye vyombo vya haki za binadamu vyote
Kwani yy hafi? Si ana nyama na damu tu? Hakim wa waki ataamua wala ucjali ingekuwa kufa kwa mtu anapanga mtu basi leo Lisu tungeshamsahau
 
amesema amesikitishwa na mambo ya uongo yanayoandikwa na baadhi ya watu .... amewahakikishia watanzania kwamba Mhe Sumaye anahitajika

eti mambo ya uongo yanayoandikwa na baadhi ya watu...

SUMAYE mwenyewe katamka kwamba kafanyiwa figisu Pwani baada ya kuandikwa na gazeti moja kwamba kachukua fomu za Uenyekiti, ambazo amekiri ni kweli alichukua... na kwamba demokrasi ndani ya CHADEMA si kama alivyodhani iko. Kama Mbowe anamstahi Sumaye amstahi lakini asiwaandame waandishi...
 
Katika hili waandishi wasilaumiwe, tatizo ni sumaye sanasana, anaamini demokrasia mdomoni, akishindwa haitaki tena.
 
PROF. ABDALLAH SAFARI AMEONA MBALI SANA!

Kiuhalisia CDM inazama. Mtu makini hawezi kukubali kuendelea kukaa katika jahazi linalozama na hasa naodha akiwa ni yule yule aliyeingiza jahazi katika dhoruba.

Ikifika hapo, Wajanja huwa wanawahi maboya na kupiga mbizi nje ya jahazi.

Ndicho alichokifanya Prof. Abdallah Safari.
Hivi safari kaisaidiaje chadema? Kimkakati.
 
Democrasia iliyo ndani ya CDM hata mbowe mwenyewe haielewi. Ni wapuuzi Wachache tu wanaoweza kuamini kuwa Chadema Ni chama Cha democrasia ya kweli.

How comes Mtu anashangiliwa tu na wachaga wenzie wa Kanda ya kaskazini anajiona anafaa kuongoza chama hiki mpaka atakapochoka.. what kind of this shit?.
Mbowe hayo mayoe Umekuja Hadi huku kwetu kusini ukayasikia je umeenda magharibi mwa Tanzania ukayasikia au ndo kuthibitisha Ile kauli ya Chadema Ni chama Cha Wachaga.

Soon Naiona Chadema inavyoenda kugawanyika Kama ilivyotokea kwa CUF. Kwa wasio elewa siasa usisumbue akili yako kunielewa Ila kwa wanao ijua siasa bila shaka utakuwa umeelewa Nini namaanisha kuhusu yajayo.

Na napenda tu kuwakumbusha nyie vyama vya upinzani Mfumo huu mnaoutumia kupata viongozi wenu wa ndani ya chama hata serikali itakuja Iutumie huohuo kupata viongozi wake na Hakuna mtu atakaepata nguvu ya kuhoji maana yeye mwenyewe atakuwa mfano tosha.
Tutegemee tu Uchaguzi wa Ndio/Hapana unarudi kwa kasi katika serikali hapo karibuni.
The future is incomplete.
Kwa sasa angalau demokrasia ya maigizo chadema wako Mbele kuliko ccm. Kwa sasa ccm kugombea uwenyekiti had uwe rais. Ukitaka kujua demokrasia ya ccm ya kijinga chukua fomu ya kumpinga magu now.muulize membe
 
Back
Top Bottom