Uchaguzi 2020 Tundu Lissu afafanua sera ya CHADEMA ya uhuru, haki na maendeleo ya watu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
*Does it make any sense?*

Kuhusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.

Na TUNDU Lissu
16.09.2020
Mbeya.

Andiko hili limetolewa kama ufafanuzi malalamiko ya CCM juu ya hoja za Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.
Pia linafafanua juu ya maendeleo ya upendeleo katika utawala wa Rais Magufuli (nyumbani kwao chato na kukwepa kwenye upinzani) na pia linafafanua ahadi zangu kwa Kanda ya Nyasa kwa ujumla: juu ya uzalishaji wa kilimo; ujenzi wa viwanda; kuimarisha biashara kusini na Nchi Jirani (Zambia, Malawi, Congo and Zimbabwe) kupitia Kanda hii.

Maelezo yake

1. CCM wamekuwa wakilalamika sana kuwa tunapotosha wananchi juu ya uhuru, haki na maendeleo ya watu. CCM kupitia mgombea Wao, Katibu Wao Mkuu, na viongozi wengine wanadai nchi hii tayari iko huru na kuwa hakuna shida ya haki na maendeleo yanafanywa ipasavyo hadi imeingia uchumi wa kati.

A. Uhuru
Tunapaswa kuonesha tofauti ya Uhuru wa Bendera wanaousema wao CCM na ule tunaomaanisha. Sisi tunataka Uhuru kamili kutenda na kushiriki mambo muhimu ya jamii, uchumi, siasa na mengineyo.

Tunaposema Uhuru kwa vyombo vya habari tunamaanisha vyombo vya habari kutoa taarifa, kufanya uchunguzi na kuhoji mapungufu wanayoona bila kutishwa, kuonewa na kufungiwa. Utekwaji waandishi habari kama Azory Gwanda au kuuawa kwa David Mwangosi sio Uhuru wa habari wala Uhuru kwa waandishi habari. Unawezaje kusema kuna Uhuru endapo mtu akimkosoa kiongozi anaishia jela au kutekwa, kupotezwa au kuuawa? Mfano: Ben Saanane; Azory Gwanda; Mdude Nyagali, Alfonce Mawazo nk. Ni Uhuru gani ambapo mawazo yanapigwa rungu baadala ya kujibiwa kwa hoja?

B. Haki.
Haki ina sifa nne: itambulike, itendeke, ionekane ikitendeka na itendeke kwa wakati. Tanzania ya magufuli kila kitu ni dili. Ukikamatwa hujui hatima yako mpaka upate upendeleo wa polisi. Dhamana imekua hiyari ya watawala. Mamlaka zinatumia vibaya sheria na kanuni za uendeshaji nchi kuwakandamiza watu wasiowapenda na kuwapendelea wengine.
Mfano: Kama wahujumu uchumi Seth, Rugemalila na wenzake walisota rumande bila dhamana kwa tuhuma za uhujumu uchumi; imekuwaje Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola aachwe mitaani kwa kosa hilo hilo? Tena mshirika wake Andengenye ameteuliwa na kupewa nafasi ya kuongoza jamii?

Je, kuna haki gani kwa wakulima kupangiwa mahali na wakati wa kuuza mazao yao (Eti kwa kisingizio nchi itapata njaa) wakati wazalishaji bidhaa viwandani hawapangiwi na serikali?

Je ni haki wananchi kupangiwa viongozi na Tume ya uchaguzi kama ilivyokuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na hii engua wagombea wa Chadema na vyama vingine vya upinzani kwenye uchaguzi huu?

C. Maendeleo ya watu.
Hapa tunataka kutofautisha ujenzi wa miradi, miundombinu na majengo bila kuzingatia mahitaji ya huduma na watu kwenye kutatua changamoto zao.

Mfano: Ujenzi wa uwanja wa Ndege Chato. Ambako hakuna hata Ndege moja inayotua kupeleka au kutoa abiria au bidhaa kwenda popote. Mabilioni ya fedha yametumika bila faida huku *Mradi wa umwagiliaji Igurusi* ukiwa umekwama. Zilihitajika shs bilioni 2 tu kukamilisha ule ujenzi ambao wakulima wa mpunga 4,200 wanateseka wakiwa na hekta 12,991 wamebaki kutegemea maji ya mvua. Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa Halmashauri zote nchini zimekosa fedha za kukamilisha miradi ya kilimo. Haswa ya umwagiliaji. Halmashauri ya Same imeongoza kwa kupata shilingi sifuri tangu 2015 hadi 2018/19.

Tunaongelea matumizi ya fedha nyingi kwa mabilioni kujenga bomba la gesi kuhamisha toka Mtwara hadi Dar wakati ingeweza kujenga kiwanda cha kuzalisha umeme hukohuko Mtwara na zile fedha zingesaidia kujenga njia za kusafirisha umeme na zaidi ya 60% zingewekezwa kwenye mahitaji mengine ya vipaumbele ikiwemo kumalizia miradi 21 ya umwahiliaji wilaya ya Mbarali ambapo mashamba ya mpunga zaidi ya hekta 32,000 zinaathirika kwa kukosa maji ya uhakika.

Tunamaanisha matumizi ya mabilioni ya fedha kujenga daraja la Oysterbay baharini wakati barabara zinazohudumia watu, wazalishaji na huduma toka Mbeya kwenda vijijini; kuunganisha Mbeya na mikoa jirani ni changamoto.

Unaongelea flyover za DAR es salaam wakati zaidi ya 75% ya barabara za mikoani ni za udongo tu. Wilaya kama ileje ndio imesahaulika kabisa.

2. Maendeleo ya upendeleo.
Rais magufuli na CCM yao wamekuwa wakijinasibu “maendeleo hayana chama”.

A. Amesikiwa mara kadhaa sasa akiwaambia wananchi wasichague wapinzani kwa kuwa hatowaletea maendeleo. Tena anawaita hao kuwa watoto wa mama wa kambo. Sasa ile dhana kuwa maendeleo hayana chama hapa ina maana gani?

B. Ujenzi wa kijiji cha Chato ni mfano wa kutosha. Uwanja wa ndege. Hifadhi ya wanyamapori wakati hawapo na imebidi wasafirishwe toka kwengine. Ujenzi wa tawi la CRDB mpaka sasa linahudumia wateja 15-20 kwa mwezi. Uwepo wa mataa barabarani hakuna magari( baiskeli na punda). Sasa wanapanga kujenga uwanja wa kimataifa wa michezo; wakati hakuna hata timu ya kijiji!

C. Mipango ya halmashauri sasa imesahaulika. Kila kitu utasikia RC amepewa fedha za ujenzi wa shule, au Tulia foundation wakati Madiwani na halmashauri ndio wenye watu na wataalam na mipango ya maendeleo kila mahali nchini. Au mmesikia ile miradi ya ujenzi wa ofisi za walimu na vyoo vya shule aliyopewa Makonda ilivyofeli DAR es salaam?

*Umetupwa wapi ule mfumo wa mgawanyo wa fedha za maendeleo kwa kutumia mahitaji na idadi ya watu kila wilaya? (Formula based allocation of development resources?)*

3. Ahadi zangu kwa Kanda ya Nyasa
Mahitaji ya Kanda kwa ujumla: uzalishaji wa kilimo; ujenzi wa viwanda; kuimarisha biashara kusini na Nchi Jirani (Zambia, Malawi, Congo and Zimbabwe) kupitia Kanda hii.

A. Kanda hii ndio tegemeo la uzalishaji wa chakula nchini. Mpunga, Mahindi na Maharage huzalishwa kwa wingi. Mazao mengine kama ndizi, viazi na matunda yapo ya kutosha.
Chadema itahakikisha inajenga mazingira bora zaidi kwa wazalishaji kuongeza uzalishaji, tija na kujipatia tija katika kilimo chao.

Hii ni pamoja na kuruhusu Biashara Huru ya chakula. Acha wakulima wauze kulingana na soko na faida. Tutawawezesha wakulima kuuza nje ya nchi na hata kuwapatia uwezeshaji katika gharama za kutafuta masoko na kuingia mikataba tukilenga haswa nchi jirani za Zambia, Congo, Malawi na Zimbabwe. Tutawaunganisha na Sudan Kusini na wahitaji wengine.
Itapobidi tutawajengea uwezo wakulima kuuza wenyewe mazao yao yakiyochakatwa.
Mambo ya marufuku za Biashara kwenye kilimo na mifugo itakua historia.

B. Biashara ukanda wa kusini.
Nyasa ndio kiunganishi muhimu na nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Congo na hata Angola na nchi zengine kusini mwa Afrika.

Tunatambua jukumu kubwa la wafanyabiashara wetu kuongeza mapato yao, kujiimarisha kiuchumi na kuchangia uchumi na kipato cha nchi. Kuna kodi na mapato mengi kupitia biashara mipakani na au usafirishaji.
Hata hivyo kwa sasa kuna vikwazo vingi sana kwenye Biashara hii. TRA, uhamiaji na polisi wamekuwa kizingiti kwa wafanyabiashara wetu kiasi cha kulazimisha kufanya biashara ya magendo.
Sisi tutajenga urafiki, tutawawezesha na kuwajengea mazingira mazuri wafanya Biashara wetu; kuwatambua na kuwasaidia wanapokwama kibiashara nje ya nchi. Tutaanzisha mfumo wa mafunzo kwa wafanyabiashara wetu wa mipakani na kuwezesha kutatua shida wanazozipata wakiwa nje ya nchi. Kuanzia wakati huo Mfanya Biashara wa Tanzania anapopata shida akiwa nje ya Tanzania atachukuliwa kama mtumishi wa umma aliyekwama huko. Litakuwa ni jukumu la serikali yangu kuhakikisha anapata haki yake kwa haraka na tija.

C. Ujenzi wa viwanda kanda ya Nyasa.
Tutawezesha ujenzi wa viwanda vya kimkakati Kanda hii tukilenga mahitajiya jamii, mahitaji ya biashara na nchi jirani na kuongeza ajira. Ile hali ya vijana wengi kulazimika kwenda mikoa mingine kutafuta ajira na bidhaa za kuuza nchi jiarani itakwisha au kupungua. Tunataka Kanda hii nayo iuze bidhaa zake za viwandani kwenda kanda nyengine na nje ya nchi.
Tutaanza na ujenzi wa kiwanda cha chuma Liganga na kuendeleza Kiwira. Tutaimarisha mgodi wa makaa ya mawe na uzalishaji saruji. Saruji ya Mbeya ilikuwa ya kimataifa sana kwa miaka mingi.

Sambamba na haya tutaimarisha mtandao wa barabara zinazounganisha vijiji na maeneo ya kibiashara mipakani.

Kwa muitikio wa wapigakura ambao hawaletwi na malori, wasanii maarufu ama ushawishi wa fedha. Ama kwa hakika CDM wanakwenda kuitwaa dola ambayo walipokwa kwa hila ushindi wao ule wa uchaguzi wa 2015.

Ngome kuu za CCM zimetikiswa kwa kishindo kikuu. Nani alitegemea Rukwa na Katavi zingetii na kutambua ukweli wa hoja za Lissu. Kwa kadiri kampeni zinavyoendelea ndivyo ambavyo watu wanafunguliwa macho na kuutambua ukweli.

Mbio za mwenge ziliwapumbaza wapiga kura wengi kwa masharti ya kishirikina, lkn kwa mwaka huu hazikuwapo tena. Ndege wa kifahari aina ya tausi alifanyiwa tambiko ktk ikulu ya Magogoni, lkn pasipo kujua ushirikina huo wamekiuka masharti na kuelekezwa kusiko stahili.

Hiki ni kimbunga, wana CCM mjiandae. It is now more than too late.
 
]Mpaka raha
IMG_20200918_171042.jpeg
 
View attachment 1573680

View attachment 1573683

View attachment 1573737
Kwa dozi hii ccm hawatoki
 
Back
Top Bottom