Tundu Lissu afichua sababu ya Magufuli kukutana na Wapinzani Ikulu bila CHADEMA

Angekuwa Mwanasheria mku wa serikali kiboko
 
KWENYE UKURASA WA MBELE WA GAZETI LA MWANANCHI LA LEO 24/03/2020 NIMEONA JIWE LIPO JUU YA JIWE. NILIWAHI KUAMBIWA KUWA MTU AKISEMA 'NIPO JUU YA MAWE' MAANA YAKE HALI YAKE NI MBAYA
 
Mimi hapo TL sijamuelewa anataka nini kwenye muungano wa vyama vya upinzani yani UKAWA. Kama kuungana ni mhimu mbona wakati wa kuunda kambii rasmi ya upinzani Mh.Mbowe hakuchagua hata mbunge moja kama Waziri kivuli kutoka vyama vya upinzani vingine alichagua tu wa Chadema wakati UKAWA walishikamana ktk uchaguzi wa 2015.
 
Unahakina?nadhani baada ya uchaguzi aliwachagua pia wapinzani wengine waliounda ukawa,kama akina Mbatia,sema nadhani mambo yameharibika baada ya CUF kuhujumiwa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo anamuita MH Rais, badara ya Dikteta uchwara! Mda sasa umeongea.

Chadema cyo chama cha siasa ni chama cha vurugu.
 
 

..wahenga walisema " mti wenye matunda ndio unaorushiwa mawe."

..na kwa hapa Tz mwanasiasa wa upinzani mwenye weledi na uwezo ndiye anayeshambuliwa na kutukanwa zaidi na serikali na ccm.

..kilichomponza TL mpaka wakajaribu kumuua ni umahiri wake ktk kujieleza na kujenga hoja, pamoja na rekodi yake ya muda mrefu ya kutetea wanyonge na rasilimali za nchi yetu.

..hali hiyo iliwasumbua sana baadhi ya watu na wakaona hakuna njia bali kumfuta kabisa TL ktk uso wa dunia.
 
Nyamsusa JB,

Sidhani kuwa utaeleweka na wengi hapa!

Kwa sababu Magufuli na Lissu ni 'diametrically' tofauti kabisa...; lakini mimi nilivyokuelewa ni hivi:

Magufuli angeachana na haya mabaya ya kuminya haki za watu, na kutotii sheria na Katiba, lakini akaendelea na juhudi zake za kuhimiza kazi kwa kila mmoja wetu katika wigo wa sheria zetu, na akawa mkali, mbogo kabisa kuhusu mali za taifa letu zitunufaishe sisi...

Na kwa upande wa pili, Tundu Lissu akasimamia haki zetu, na taratibu zote za kufanya mambo yetu ndani ya sheria tulizojitungia sisi wenyewe.

'Combination' hiyo ingekuwa ni ya kipekee sana kuwahi kutokea Tanzania (leo nadiriki kusema hili).

Kwa sababu, hata Mwalimu hakubahatika kumpata 'counterpart' kama hii ambayo Magufuli angeweza kuipata.

Ni mawazo tu.
 
Upo sahihi kabisa, Magufuli angeliona hili angepata watu sahihi kuleta Mapinduzi ya Uchumi na kuyasimamia kwa dhati. Tanzania bado inahitaji watu wa kaliba ya The Greater Lissu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…