Nyamsusa JB,
Sidhani kuwa utaeleweka na wengi hapa!
Kwa sababu Magufuli na Lissu ni 'diametrically' tofauti kabisa...; lakini mimi nilivyokuelewa ni hivi:
Magufuli angeachana na haya mabaya ya kuminya haki za watu, na kutotii sheria na Katiba, lakini akaendelea na juhudi zake za kuhimiza kazi kwa kila mmoja wetu katika wigo wa sheria zetu, na akawa mkali, mbogo kabisa kuhusu mali za taifa letu zitunufaishe sisi...
Na kwa upande wa pili, Tundu Lissu akasimamia haki zetu, na taratibu zote za kufanya mambo yetu ndani ya sheria tulizojitungia sisi wenyewe.
'Combination' hiyo ingekuwa ni ya kipekee sana kuwahi kutokea Tanzania (leo nadiriki kusema hili).
Kwa sababu, hata Mwalimu hakubahatika kumpata 'counterpart' kama hii ambayo Magufuli angeweza kuipata.
Ni mawazo tu.