Hii ni habari iliyoandikwa na gazeti la MWANANCHI la leo.
Wakati ni habari iliyotarajiwa ifurike maoni mitandaoni kinyume chake ni kama vile haipo kabisa.
Hata mimi humu nimei post mara ya kwanza ikafutwa na sijui kama hii mara ya pili haitafutwa.
View attachment 2036038
Toka Maktaba :
02 December 2021
Bunge la Ulaya / EP / EU
Brussels, Belgium
Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya, yakataa ripoti ya EESA kuhusu Tanzania, Bunge la Ulaya lataka Tanzania ichukuliwe hatua.
Mwenyekiti David James McAllister MEP akakumbushia barua yake aliyoandika kuwaonya wataalamu wa Umoja wa Ulaya
EEAS About the European External Action Service (EEAS) mwaka jana mwezi November 2020 kuhusu "kuubeba" utawala dhalimu usiofuata haki za msingi za kibinadamu. Akiwasilisha Ripoti, mmoja wa wataalamu wa
EEAS Ms.
Rita Laranjinha EEAS: High Representative Josep Borrell announces senior appointments | Press Club Brussels Europe alinukuu taarifa ya EEAS ilisema kuna maendeleo 'makubwa' nchini Tanzania mbali ya changamoto ndogo ndogo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya akakumbushia hicho kinachoitwa 'changamoto ndogo ndogo' kwa hakika ni kikubwa na hakipaswi kutupiliwa mbali ikiwa watu wanakamatwa ovyo, kutupwa mahabusu, kufunguliwa mashtaka, kutishiwa haki ya kuishi n.k mambo ambayo ndiyo msingi mkubwa wanaousimamia Umoja wa Ulaya wakati wa kutoa msaada kwa nchi yoyote ulimwenguni
EEAS - European External Action Service - European Union External Action
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge la Ulaya amesema mfano wataalamu hao je wameweza kukutana ndani ya Tanzania na mwenyekiti wa CHADEMA au makamu mwenyekiti wa CHADEMA? Ambao ni viongozi wa chama kikuu cha upinzani, mmoja akiwa rumande kwa kesi ya kutunga huku mwingine akiwa uhamishoni Belgium halafu wataalamu hao wanasema ni changamoto ndogo ndogo?
Pia kuna raia wanaoshiriki siasa Tanzania wenye mtizamo mbadala walio wanachama, wapenzi na wafadhili wazalendo wa KiTanzania wanabaguliwa kushiriki ktk vyombo vya maamuzi ngazi zote, wanaoozea ktk jela mbalimbali Tanzania au biashara zao kuhujumiwa je hayo ni mambo madogo ? Amehoji David James McAllister mwenyekiti huyo makini wa kamati ya Bunge la ulaya.
Hivyo amewataka wataalamu hao waliotumwa na bunge la Umoja wa Ulaya kuwabebeleza watawala wa Tanzania kuacha ukandamizaji, kujitathmini kama wanataka kulimwa barua nyingine kali ya karipio kuhusu ripoti yao iliyozua maswali mengi ndani ya Bunge la Ulaya na miongoni mwa wabunge wa Bunge hilo la Ulaya mwaka 2020 na vivyo hivyo pia mwaka huu mwezi November 2021 inayojadiliwa na Kamati hiyo ya Bunge la Ulaya.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge la ulaya amewataka wataalamu hao kuja na majibu mujarabu ya kuibana serikali ya Tanzania kwa kuwa inatumia misaada ya Umoja wa Ulaya itokanayo na kodi za raia wa nchi wanachama zinazoamini katika utawala bora, haki za binadamu kulindwa na demokrasia hivyo haiwezekani nchi viongozi wa nchi walio wakandamizaji kama wa Tanzania kufaidi jasho na nguvu wa walipa kodi wa Ulaya wanaoamini katika uhuru, haki na Maendeleo ya kweli ya watu ktk demokrasia inayozingatia utu.
amesema yeye na wajumbe wabunge wa kamati ya mambo ya nje wanajiandaa kupendekeza hatua "kali" dhidi ya utawala unaoendekeza udhalimu waziwazi na kwa kificho.
David James McAllister mwenyekiti wa Kamati Ya Bunge la Ulaya ya Mambo ya Nje anasema mbali na ripoti hiyo ya wataalamu wake pia wanapata habari kupitia balozi za Marekani, Canada , Uingereza na balozi wa nchi wanachama wanaohudhuria kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya tuhuma nzito za kupikwa dhidi ya Mbowe na wenzie 3, na kesi hiyo ni kichekesho dhidi ya Umoja wa Ulaya na raia wa wa Umoja wa Ulaya ambao wote wanaamini ktk haki mbele ya sheria, demokrasia na kutokuwepo ugandamizaji wa haki za kibinadamu za aina yoyote.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge anataka kuona wataalamu hao wanakuja na mkakati gani wa kuibana serikali ya Tanzania inapotaka misaada na mikopo, kwani sasa siyo muda tena wa
maongezi / dialogue yasiyo na kikomo kuhusu hali hii mbaya ya kisiasa nchini Tanzania, bali ni wakati wa Umoja wa Ulaya kufanya
matendo kwani muda wa maneno umekwisha, ili ujumbe uwaingie watawala dhalimu.
David James McAllister political career started in 1998 becoming a Member of the State Parliament of Lower Saxony (until 2014) in Germany. He was also the Mayor of his hometown Bad Bederkesa from 2001-2002, Secretary-General of the CDU in Lower Saxony from 2002-2003, and Chairman of the CDU Group in the State Parliament from 2003-2010. He was Party Chairman of the CDU in Lower Saxony from 2008-2016. He served as Prime Minister of Lower Saxony from 2010 till 2013. Member of the CDU Executive Committee since February 2014. MEP since July 2014. Since November 2014 Vice President of IDU (International Democrat Union). Since October 2015 Vice President of the EPP (European People's Party). In the European Parliament, McAllister is Chair of the Committee on Foreign Affairs, substitute member of the Committee on International Trade and the Sub-Committee on Security and Defence, member of the Delegation for Relations with the USA and the Delegation for Relations with the NATO Parliamentary Assembly and substitute member of the EU-Serbia Stabilisation and Association Parliamentary Committee
Umoja wa Ulaya - EU
02.12.2021
Umoja wa Ulaya ni muungano wa kisiasa na kiuchimu kati ya mataifa 28 yaliyoko hasa katika bara la Ulaya. Jumuiya hiyo ina wakaazi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 508.
Umoja wa Ulaya unaendesha shughuli zake kupitia mfumo wa taasisi zilizo juu ya mataifa na maamuzi yanayofikwia baina ya serikali za mataifa wanachama.
Taasisi hizi ni:
- Bunge la Ulaya,
- Baraza la Ulaya,
- Baraza la Umoja wa Ulaya,
- Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya,
- Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya,
- Benki Kuu ya Ulaya na
- Mahakama ya Ukaguzi.
Bunge la Ulaya linachaguliwa kila baada ya miaka mitano na raia wa Ulaya
Source :
Umoja wa Ulaya - EU | DW | 01.12.2021