PreGE2025 Tundu Lissu ahojiwa kwa makosa ya uhaini na kutoa taarifa za uongo, agoma kutoa maelezo Polisi

PreGE2025 Tundu Lissu ahojiwa kwa makosa ya uhaini na kutoa taarifa za uongo, agoma kutoa maelezo Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Leo Aprili 10, 2025, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mwanasheria Tundu Lissu amehojiwa kwenye na Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa makosa mawili ya Uhaini na kutoa taarifa za Uongo. Pia Lissu hajatoa maelezo yoyote isipokuwa taarifa zake binafsi pekee.

Polisi wamesema watampandisha mahakamani punde wakikamilisha taratibu zinazotakiwa

Pia soma: Pre GE2025 - John Heche: Nimepata taarifa za kuaminika kuhusu mpango wa kumkamata Tundu Lissu kwa Kumbambikia Kesi ya Uhaini

View attachment 3298983
Kitaeleweka tu hata huko mahakamani
Akikataa kitu aliongea credibility yake itaanguka hadi zero

Hao anawaambia no reform no election kama walimsikia akiongea hicho anashitakiwa nacho kama walimsikia live akakikana msiwe na hofu watajitenga naye akisema sikusema wakati alisema

Polisi songeni Mbele mburuzeni mahakamani huko ndiko hiyo minyumbu inatomfuata blindly mtaifungua macho

Wajue wanahangaika na tapeli la ubelgiji

Vyombo vya habari vyote jaeni mahakamani kusikiliza kauli yake ili ku inform public accordingly sababu mli mrecord kabla akiongea huo uhaini wake mna clips zake

Msikose mahakamani ku record alichoongea na anachojitia kuongea baada ya kuburuzwa mahakamani

Njia ya mwongo fupi
 
Hawa jamaa wanatafuta kwenda kujidharirisha tu huko mahakamani. Waachane na mambo ya mahakamani dhidi ya harakati za kisiasa.
 
Anaanza kupita njia za Mbowe zile ambazo Doctor Silaha alisema anakasirishwa sana na wanaosema Mbowe sio gaidi.Jamani tuweke akiba ya maneno,tumuombee tu ili wenye maamuzi ya kuwapa watu kesi wasimpe kesi ngumu Lisu.
Wana nunua mda ila mda ukifika watu wasipo sema mawe yatasema Lisu akiwa ndani naona nivizuri zaidi kuliko akiwa nje akiwa ndani wao watakuwa wanamuhakikishia usalama wake kwa asilimia mia na atakuwa anaendeleza mapambano vizuri zaidi No reform no Election sijaona swala la uhaini hapo ,wahaini ni wale wanaoteka watu ,wanao iba kula wanao Engua wagombea halali kwenye uchaguzi,wanaokataza mawakala wawapinzani wasiingie kwenye vyumba vya uchaguzi hao ndiyo wanapaswa wafunguluwe kesi ya uwaini lakini wakimfungulia Lisu kesi ya uwaini watawasha moto mkali sana wataweka watu wengi sana ndani na kuwauwa kwasababu watanzania safari hii hawatakubali ujinga.
 
Zipi sasa!!
Mkutano wenu wa hadhara huwo ambao hamkusomba watu kwa malori.
20250410_155441.jpg
 
Leo Aprili 10, 2025, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mwanasheria Tundu Lissu amehojiwa kwenye na Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa makosa mawili ya Uhaini na kutoa taarifa za Uongo. Pia Lissu hajatoa maelezo yoyote isipokuwa taarifa zake binafsi pekee.

Polisi wamesema watampandisha mahakamani punde wakikamilisha taratibu zinazotakiwa

Pia soma: Pre GE2025 - John Heche: Nimepata taarifa za kuaminika kuhusu mpango wa kumkamata Tundu Lissu kwa Kumbambikia Kesi ya Uhaini

View attachment 3298983
Agome asigome Sheria itachukua mkondo wake
 
Back
Top Bottom