Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aifuta CCM Morogoro

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aifuta CCM Morogoro

Leo niliwepo hapa Morogoro katika kiwanja cha Mashujaa kumsiliza Lissu,huyu jamaa Mungu kamjalia kujenga hoja na anapozungumza nashawishika kumsikiliza kila neno.Yuko tofauti na washindani wake.Alichoongea pale Morogoro leo imekuwa gumzo.Wakati tunarudi nyumbani nimewasikia watu wakisema CCM safari hii sasa basi.Watanzania wengi wameumizwa na utawala huu kwa namna tofauti tofauti
 
Tofauti kubwa kati ya kampeni za uchaguzi za Tundu Lissu na zile za yule wa CCM ni kwamba, kwa Rais Mtarajiwa Tundu Lissu wapigakura hutaka kuzisikia sera mbadala, wakati kwa yule huenda kwa matarajio ya kuwaona wasanii maarufu wa Bongo fleva.

Hii ndiyo maana mikutano ya Rais Mtarajiwa hujaa watu wazima ambao wanajitokeza kwa hiari yao wenyewe. Wakati kwa bwana yule ni mwendo wa kubeba mamburura kwa malori na wanafunzi walolazimishwa na walimu wao ambao pia wamelazimishwa kuwalazimisha kufanya hivyo.
Saharavoice
Njoo huku uelimike mkuu
 
Sio ya uongo ila amecheza na angle ili picha ionekane anavyotaka yeye . kwa wapiga picha wanalijua hili ,pia ame crop na kuondoa vitu ambavyo hakutaka vionekane
Hahahaha mavi yanakutoka
IMG_20200911_212606.jpg
 
Sisi tunaotembea tembea vijijini ukisoma baadhi ya uzi humu unabaki unacheka tu,
Mtu amekaa bar anakula balimi zake akishapata stim anaanzisha uzi

Nimetoka morogoro vijijini inaitwa morogoro mashatiki

Mbunge na madiwani wote wamepita bila kupingwa na wananchi awana hata hamasa ya uchaguzi

Uchaguzi wa 2015 kulikuwa na diwani mmoja tu wa upinzani akitokea ACT kata ya kiloka kijiji cha tomondo na kungwe
Mwaka huu yule diwani kaunga mkono juhudi karudi ccm kapita bila kupingwa

Hivi tunavyo ongea karibu madiwani wote wa ccm wamepita bila kupingwa
Kifupi mkoa wa Morogoro upinzani ZIRO..

Kilichoandikwa humu ni porojo..soma potezea ...matembele wametuzidi..
Pumba
 
Sasa hizo picha ndo kufuta CCM morogoro? Au hiyo kanzu na baraghashia ndo kufuta CCM Moro?
Ajabu Sana.
Hivi Lissu anafikiri anaweza kuwalaghai waislamu kwa kuvaa kanzu na kofia kila Ijumaa? Nafikiri Lissu hajui imani ya uislamu! Hata, figisu figisu za mabeberu wameshindwa kujua imani ya usilamu ikoje, sasa huyu Lissu anaona anaweza kuwahadaa simply kwa kuvaa kanzu na balaghshia kila ijumaa! Uislamu siyo maigizo hata kidogo - alijue hilo na asije akajikosesha kura zao kwa kukebehi dini yao.
Mbona sijamuona akivaa kama singasinga!
 
Ukitaka kujua watu wana mapenzi gani n.a. timu iwe Simba au yanga angalia uwingi wa uvaaji nguo za timu kwenye uwanja

Tofauti ya mikutano ya CCM na Chadema ni kuwa CCM inahudhiriwa na wanachama wengi wakiwa wamevaa nguo za CCM Chadema wanaohudhuria ni wasiojulikana ni Chama gani

Huoni zile tshirt za Chadema ushahidi kuwa wanaohudhuria ni wapita njia waliokuja th kumshangaa Lisu

Kwa mtizimo ukitizama picha zote za mikutano ya Chadema wavaa Tshirt za Chadema ni wa kumulika na tochi ni kama hawapo kabisa

CCM mikutano yake unaona wazi kuwa waliofurika wengi ni wafia chama sio wapita njia Chukua picha zote za uzinduzi wa Chadema na za CCM utaona hilo tofauti wazi bila chenga
Watu wanakusanywa, wanapewa pesa na manguo ya ccm wanaambiwa wavae, then wanasombwa na malori kwenda kwa mikutano ya ccm.. na siyo wanachama!
 
Leo niliwepo hapa Morogoro katika kiwanja cha Mashujaa kumsiliza Lissu,huyu jamaa Mungu kamjalia kujenga hoja na anapozungumza nashawishika kumsikiliza kila neno.Yuko tofauti na washindani wake.Alichoongea pale Morogoro leo imekuwa gumzo.Wakati tunarudi nyumbani nimewasikia watu wakisema CCM safari hii sasa basi.Watanzania wengi wameumizwa na utawala huu kwa namna tofauti tofauti
Wewe umeumizwaje bwashee?!
 
Hivi Lissu anafikiri anaweza kuwalaghai waislamu kwa kuvaa kanzu na kofia kila Ijumaa? Nafikiri Lissu hajui imani ya uislamu! Hata, figisu figisu za mabeberu wameshindwa kujua imani ya usilamu ikoje, sasa huyu Lissu anaona anaweza kuwahadaa simply kwa kuvaa kanzu na balaghshia kila ijumaa! Uislamu siyo maigizo hata kidogo - alijue hilo na asije akajikosesha kura zao kwa kukebehi dini yao.
Mbona sijamuona akivaa kama singasinga!
Lissu anavaa kanzu kama ishara ya kuheshimu dini ya uislamu, anavaa kanzu kuonesha kuwa atakuwa kiongozi wa dini zote sio wakristo tu, anavaa kanzu kuonesha anaguswa na madhira wanayofanyiwa waislamu wa nchi hii hasa masheikh waliopo magerezani.

Kama imekuuma tulia tu dawa ikuingie. Huyu ndo Tundu Lissu kipenzi cha Mungu na Watanzania.
 
Back
Top Bottom